Njombe: Wawili wasakwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linawasaka watuhumiwa wawili ambao wanadaiwa kuwa ni majambazi na kuhusika na uvamizi na mauaji ya wafanyabiashara wawili uliotokea Mtaa wa Kambarage Agosti 29 mwaka huu mkoani Njombe.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi, John Imori wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa.

Amesema waliofariki dunia kutokana na uvamizi uliofanywa na majambazi hao ni Golden Luoga (34) na Faraja Luoga (40).

Amesema wakazi wa Mkoa wa Njombe wanatakiwa kuwa watulivu wakati jeshi hilo wakiendelea na msako wa kuwapata majambazi hao.

"Baada ya kuvamiwa pale ndani ndugu hao wote wawili walijeruhiwa na risasi na wakati walipelekwa hospitali siku hiyo hiyo 29 Agosti usiku. Faraja Luoga alifariki kabla ya kufikishwa kwenye hospitali yetu ya wilaya," amesema Imori.

Amesema Golden Luoga yeye alikuwa amejeruhiwa upande wa ubavu wa kulia lakini alikuwa anaendelea vizuri ila siku jana 31 Agosti alihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Amesema mpaka saa tano usiku hapo jana alikuwa anaendelea vizuri lakini alfajiri ya leo Septemba 1, 2023 ndipo wakapata taarifa kuwa naye amefariki.

Wakati hayo yakiendelea jeshi hilo limeendelea kujiimarisha kwa kuwekeza mafunzo kwenye nguvu kazi ya maofisa wa polisi mafunzo ambayo wanaeleza kuwa yatasaidia kukabiliana na vitendo vya kihalifu.

Baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi waliohitimu mafunzo hayo Tubone Mwakijale na Mary Kweka wamesema wako tayari kukabiliana na wahalifu wa usiku na mchana.

"Nitoe rai kwa hao wahalifu wanaojihusisha na vitendo hivyo ambavyo siyo sahihi na haramu kwa mujibu wa sheria za nchi hivi sasa tunarudi," amesema Mwakijale.

MWANANCHI
 
Nimetoka wiki hii mkoa huo nilikua kidugala nikapita ilembula Lutheran hospital nikarudi makambako na baadae iringa then Dar.
 
Back
Top Bottom