Tucta yashikia bango maandamano kupinga bei ya umeme

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,174
Tucta yashikia bango maandamano kupinga bei ya umeme
Wednesday, 19 January 2011 21:42

Patricia Kimelemeta

SHIRIKISHO la vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), limesema bado linaendelea na mchakato wa kuelimisha wafanyakazi juu ya hatua zitakazochukuliwa wakati wa kufanya maaandamano ya amani ya kupinga ongezeko jipya la bei ya umeme.

Hatua hiyo imekuja baada ya Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco) kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 18, ongezeko ambalo lilianza Januari Mosi mwaka huu.

Akizungumza na Mwananchi kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam , Naibu Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya alisema mkakati wa kufanya maandamano upo palepale.

Alisema kutokana na hali hiyo Tucta inaendelea kufanya maandalizi ya maandamano hayo ili wafanyakazi waweze kutetea haki zao.
“Mkakati wa maandamano bado upo palepale, kwa sasa tunaendela na vikao ili tuweze kufuata taratibu zilizopo kwa ajili ya kufanya maandamano yatu, lengo ni kuitaka serikali kupunguza gharama za umeme ambazo kwa kiasi fulani zinawakandamiza wafanyakazi,”alisema Mgaya.

Aliongeza kwamba maandamano yao yatafanyika nchi nzima ili wafanyakazi waweze kushiriki kikamilifu, jambo ambalo wanaaamini kuwa serikali inaweza kusikiliza kilio chao.

Alisema gharama za umeme ni kubwa, zinawaumiza wafanyakazi kwa kiasi kikubwa kutokana na kupata mishahara midogo ambayo haiwezi kukidhi mahitaji ya kila siku.

Alibainisha,kutokana na hali hiyo serikali ina haja ya kuangalia upya bei hiyo ili tabaka zote ziweze kuondoa malalamiko yao.

Tucta imepanda kufanya maandamano ya amani Januari 29 mwaka huu, kwa ajili ya kuishinikiza serikali kupunguza gharama za umeme zilizoongezwa hivi karibuni.
 
Wenye kero wasibughudhiwe..........waachwe waandamane..........Tusije tukasikia polisi wanabuni taarifa za "Kitnelijenisa" kukataza maandamano haya ya halali nchi nzima...............................................tumechoka kuonewa na hawa mafisadi.......................
 
TUCTA si wale walikemewa kama mbwa walipotaka kugoma, na kuambiwa kura zao hazitahitajika? Safari hii kweli wataweza?
 
Back
Top Bottom