TUCTA, Serikali washindwa kupatana

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013
* Hatma yasubiri maamuzi ya Waziri wa Utumishi

Na Dunstan Bahai

spacer.gif
Tuesday, 11 May 2010


MAZUNGUZO yaliyokuwa yanasubiriwa kuamua hatma ya mdai ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na serikali Jumamosi hayakuzaa matunda kwani kila upande umeendelea kubaki na msimamo wake.

Mazungumzo hayo ndiyo yalikuwa yanasubiriwa na wafanyakazi ili kujua hatma yao, huku rais huyo akiwa tayari ameweka bayana kuwa serikali yake haina uwezo wa kulipa kima cha chini wanachotaka.


Madai ya msingi ya wafanyakazi hao mbali na kima cha chini cha sh. 315,000, wanataka kupunguzwa kwa kodi kubwa inayotozwa kwenye mishahara kutoka asilimia 15 hadi 9 na marekebisho ya mafao mifuko ya pensheni.


Akizungumza jana, Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA, Bw. Nicholaus Mgaya alisema majadiliano hayo hayakufikia muafaka.


"Kila upande umemaliza mazungumzo hayo ukiwa na msimamo wake. Tumekubaliana kutokubaliana. Mapendekezo hayo ya kila upande yatapelekwa kwa Waziri mwenye dhamana ya utumishi na yeye atatoa maamuzi yake ndani ya siku 21 kuanzia siku mapendekezo hayo yalipotiwa saini na pande zote mbili," alisema.


Bw. Mgaya alisema maamuzi atakayoyatoa Waziri Hawa Ghasia, ni ama akubaliane na upande wa serikali au wa wafanyakazi au asikubaliane na upande wowote na hivyo kuyarudisha mapendekezo yake kwenye meza ya mazungumzo.


Wakati wakisubiri maamuzi ya waziri, Baraza Kuu la TUCTA litakutana mwishoni mwa mwezi huu kuyajadili.


Alisema Baraza hilo kwa kuwa ndilo lililotangaza mgomo, ndilo litakalotangaza tena kuwepo au kutokuwepo kwake.


TUCTA waliandaa mgomo wa wafanyakazi nchi nzima Mei 5, mwaka huu lakini wakiwa kwenye maandalizi ya mgomo huo, siku mbili kabla, Rais Kikwete alitumia nafasi ya kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam kuuzima na kuwatupia lawama viongozi wa shirikisho hilo kwa uongo na unafiki, tuhuma ambazo zimepingwa na kudaiwa kuwa kiongozi huyo amepotoshwa.


Katika hotuba yake Rais alisema serikali haina uwezo wa kulipa kima hicho cha chini kilichopendekezwa na TUCTA na kwamba kutokana na hali ya uchumi hata wakigoma miaka minane, serikali haitaweza kuwalipa na kwamba wakiendelea na msimamo wao huo serikali iko tayari kuwafukuza kazi wafanyakazi wote.


Hata hivyo, TUCTA walisema kauli ya Rais katika mkutano huo ililenga kuwadhalilisha na kwamba hana mamlaka kisheria ya kuzima mgomo huo bali Mahakama Kuu kitengo cha kazi pekee.
 
Wasiokuwa na kazi ndo wengi,na JK ndo anataka kura zao,sad but true,kama wafanyakazi wanaamini kuwa walimsaidia JK kuingia madarakani,then ni juu yao kumprove Mr President wrong,ambaye anaelekea kuamini kuwa their votes dont really matter neither does their influence in community.
 
Media zetu wakati mwingine zinachanganya wananchi
Lakini nafikri viongozi wa TUCTA wana buy time tu wamesha ahidiwa kipande cha keki basi wanajivutavuta ndo vile tena mgomo umepeeruka mithili ya mbayuwayu



By PIUS RUGONZIBWA, 10th May 2010 @ 12:00, Total Comments: 4, Hits: 635

THE Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA) has said that the talks with the government over the weekend on salary review for the workers in the public sector were tense but were concluded successfully.

TUCTA acting General Secretary Mr Nicholaus Mgaya told the 'Daily News' today that the Saturday talks' conclusions were duly signed by all parties engaged including the Union representatives.

"Normally such talks are give and take but at last all parties including ours signed the conclusion and we are now waiting for the responsible Minister to announce the final report and award or reject it," he said.

The government representatives in the talks were not available to give their views but according to the Labour Institutions Act of 2004, the Minister of State in the President's Office responsible for Public Service Management, Ms Hawa Ghasia, will be required to make the report of the talks public within 21 days.

Mr Mgaya said, however, TUCTA would meet today to discuss the outcome of the talks after receiving report from its representatives. Apart from the minimum wage for workers in the public sector, another agenda that dominated the talks, according to Mr Mgaya, was the issue of Pay as You Earn (PAYE) deducted from workers' salaries.

"We submitted our suggestions on the tax deducted from workers' salaries and we are proposing the tax should remain in single digit not exceeding minimum 9 per cent unlike now when it starts from 15 per cent to 35 per cent," he said.

He said despite successful talks on Saturday, TUCTA will maintain their stand on nationwide strike until Minister Ghasia announces the report of the talks.

"We will then meet to react on the Minister and give our new position on the strike," he said.

But in the new development, he said from next week TUCTA leaders will visit their members throughout the country to sensitize them on the strike and give feedback on what is now going on the ground.

The TUCTA boss said such tour had already started in Coast, Morogoro and Dodoma Regions but will now continue to the rest of the country. On the minimum wage in the private sector, Mr Mgaya said the Congress has instructed its lawyers to review and advise on the discovered discrepancies.
 
Tucta sasa yamwumbua Waziri Kapuya Wednesday, 12 May 2010 05:42 0diggsdigg

Patricia Kimelemeta

MGOGORO wa Tucta na serikali umechukua sura mpya baada ya baraza kuu la shirikisho hilo la wafanyakazi kuibuka na hoja kwamba nyongeza ya kima cha chini ya sekta binafsi iliyotangazwa na Waziri Juma Kapuya imeshusha kiwango kilichotangazwa mwaka 2007.

Kauli hiyo ya Tucta imetolewa baada ya baraza kuu kujifungia kwa siku nzima ya jana kujadili ripoti ya matokeo ya mazungumzo baina ya serikali na shirikisho hilo yaliyofanyika Jumamosi iliyopita ambayo yanatarajiwa kutoa picha halisi ya mgomo wa wafanyakazi wote ambao awali ulipangwa kuanza Mei 5.

Tucta pia jana haikuweza kutoa tamko la mgomo kwa maelezo kuwa inasubiri kuisha kwa siku 21 ambazo kwa mujibu wa sheria, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Kapuya anapaswa kutoa tamko la makubaliano yaliyofikiwa.
Shirikisho hilo limesema limeashaanza kuhesabu siku hizo tangu kuisha kwa mkutano huo wa Mei 8.

Tucta imeeleza kuwa kama waziri atashindwa kufanya hivyo katika kipindi hicho, Tucta itakuwa kwenye nafasi ya kutangaza mgomo.

Naibu katibu mkuu wa Tucta, Nicholaus Mgaya alisema jana jijini Dar es salaam kuwa baraza hilo limebaini upungufu katika baadhi ya vipengele vya ongezeko la mishahara ya sekta binafsi ambavyo vinapingana na tangazo la ongezeko la kima cha chini cha mshahara la mwaka 2007.

Kutokana na hali hiyo, Mgaya alisema Tucta ilishirikiana na wanasheria wake kupitia upya tangazo la Waziri Kapuya na kubaini kuwa halikufuata taratibu za kisheria ambazo ni pamoja na kutowashirikisha wajumbe wa bodi ya mishahara ya kisekta.

Kwa mujibu wa Mgaya, Waziri Kapuya alipaswa kutangaza kima cha chini cha mishahara baada ya kupokea ushauri na mapendekezo kutoka kwenye bodi za kisekta za mishahara ambazo ndizo zinazotoa mwongozo.

Alisema matokeo ya kosa hilo la kiufundi ni viwango vya mishahara ya sekta binafsi mwaka huu kushuka, ikilinganishwa na viwango vya mishahara vilivyotangazwa mwaka 2007.

"Tucta inapingana na tangazo la serikali la kuongeza viwango vya mishahara kwa sekta binafsi kwa sababu baadhi ya vipengele vinaonyesha wazi kuwa mishahara ya wafanyakazi imeshuka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na tangazo lililotolewa mwaka 2007," alisema Mgaya.

Mgaya alitoa mfano kuwa kiwango cha kima cha chini cha mishahara cha sekta ya viwanda na biashara cha mwaka 2007 kilikuwa Sh150,000, lakini katika tangazo la Waziri Kapuya kiwango hicho kimeshuka hadi Sh80,000.

Alisema katika tangazo hilo jipya, serikali pia imefuta baadhi ya marupurupu ya wafanyakazi wa sekta hiyo na nyingine, ikiwa ni pamoja na posho ya nyumba, chakula, likizo na usafiri.

"Mabadiliko hayo ya mishahara yanaweza kuzua mgogoro katika maeneo ya kazi, jambo ambalo linaweza kusababisha kuvunjika kwa mahusiano kazini baina ya waajiri na waajiriwa," alisema Mgaya.

"Kutokana na hali hiyo, utendaji wa kazi wa wafanyakazi hao unaweza kupungua kwa sababu wataaamini kuwa waajiri wao wanashindwa kutetea maslahi ya wafanyakazi wake."

Alibainisha kuwa migogoro mingi inayotokea katika baadhi ya maeneo ya kazi, inatokana na maboresho yasiyoridhisha ya mishahara na hivyo serikali ilipaswa kuliangalia suala hilo kwa undani kabla ya kutoa tangazo lake.

Alisema baada ya kubaini upungufu huo baraza la Tucta limeahidi kutoa tamko hivi karibuni baada ya kukaa na bodi na kupitia upya ajenda hizo mbili za nyongeza ya mishahara na mkutano wa Mei 8 ambachpo kitafanyika kesho.

"Kikao hicho kitajadili mikakati iliyoafikiwa baina ya Tucta na serikali katika kikao cha utatu cha majadiliano kilichofanyika tarehe 8 mwezi huu ambayo kwa mujibu wa sheria, Waziri Kapuya anapaswa kutoa taarifa ya makubaliano yaliyofikiwa ndani ya siku 21," alisema.
Awali mgomo wa wafanyakazi ulipangwa kuanza Mei 5, lakini ukaahirishwa kusubiri kikao cha mwisho baina ya serikali na viongozi wa shirikisho hilo kilichofanyika Mei 8.

Tucta, pamoja na mambo mengine, iliitisha mgomo huo ikidai kuwa serikali imekuwa ikipuuzia madai yao ya muda mrefu ambayo ni pamoja na punguzo la kodi inayokatwa kwenye mishahara, kuboreshwa kwa mafao ya uzeeni yanayotolewa na mifuko ya hifadhi ya jamii na nyongeza ya kima cha chini cha mishahara ya sekta zote.
 
[B said:
Mgaya alitoa mfano kuwa kiwango cha kima cha chini cha mishahara cha sekta ya viwanda na biashara cha mwaka 2007 kilikuwa Sh150,000, lakini katika tangazo la Waziri Kapuya kiwango hicho kimeshuka hadi Sh80,000.[/.

Here we go again, kumbe serikali yetu inafanya kazi kama kichwa cha mwendawazimu!
 
Back
Top Bottom