Tuache Wivu kwa Nehemia Mchechu

Status
Not open for further replies.
Kwa hio shirika linajenga nyumba kwa watu "MATAJIRI"

Asilimia 95 ya watanzania ni MASIKINI

Hizo nyumba zina Umuhimu gani kwa wananchi?

Halafu...Mchechu aliomba jkazi NHC sema alibebwa na Luhanjo...sio kwamba alifuatwa

CBA Bank ndipo alipotoka....CBA bank haijawahi kuwa na mradi wa kujenga Nyumba

Come to Basics....Huwezi kulipa wakurugenzi mashahara zaidi ya Rais...Never.....Sio kwenye Public sector
 
Mchechu anastahili huo mshahara.. Kama serikali inaona huo mshahara ni ghali kuliko perfomance yake watafute DG wakumlipa laki 8 anayepga dili za M100 kwa mwezi..
Hivi unadhani hiyo milioni 35 itamzuia mwizi kuiba? Mwenye tamaa ni mwenye tamaa tu, hawezi kutosheka!
 
Watu wana wivu tu na mchechu. Hata rais ana wivu na mchechu.

Watu kibao wanalipwa zaidi ya mchechu ila hawaongelewi. Mchechu yamemkuta hayo kisa tu alikua team lowassa.

Yule mama wa tanzania investment centre anakula 38+m, na wengine wa dawasco,tpdc,tcra,rea nk ila hawaguswi.

Ni wivu tu kwa mchechu. Sioni sababu ya kumuonea wivu mchechu.
Kwani kafanywaje hyo mchechu
 
Nimekuwa nafuatilia mjadala hasa wa Rais Mtukufu bwana Magufuli kuhusu mishahara ya watumishi kuwa mikubwa.

KIMSINGI Nadhani rais ana nia njema ya kujenga moyo wa uzalendo kwa watu ili watangulize maslahi ya Taifa kwanza na yao binafsi yaje baadae.

Tatizo langu nikwamba watu wengi tumejikita zaidi kumshambulia Nehemia Mchechu CEO wa NHC. Eti tu kwa kiwango tunachokiita kikubwa cha mshahara wa M35. Wengi wetu hatuzungumzii Mchechu alikutoka alikuwa analipwa 26M.

Na alianza project ya kujenga nyumba akiwa kwenye taasisi yake ya zamani. So serikali iliona atafunika NHC zaidi kwasababu ni wazi shirika lilishakuwa kinapumulia mipira.

NHC kifupi ikishakaribia kufa Bwana Mchechu hakuomba kazi NHC serikali ilimfuata. Mchechu amefanya kazi kubwa sana NHC ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzo. Mchechu anastahili kulipwa zaid ya hapo

issue hapa si wivu ni kwanza kwanza kabisa shirika halipo kwa ajili ya mlalahoi lipo kwa ajili ya watu wenye uwezo malengo ambayo ni tofauti na yale ambayo shirika lilipaswa kutekeleza.pia si kweli shirika lilikuwa kaputi mm nimefanya kazi kwenye shirika hilo wakati makongoro mahanga ni mkrugenzi wa shirika na baadaye liliendeshwa na aliyekuwa mkurugenzi wa ewura haruna masebo.wakurugenzi wote hao waliweka maslahi ya wananchi mbele.mchechu iwe iweje hawezi kupokea shs.35m hii haikubaliki.kwani yeye anaspcial skills gani ambayo watanzania wengine hawana.
Na wala serikali haikumfuata mchechu bali aliwekwa pale na mkuu wa kaya hata interviews hakufanya hivyo alibebwa tu sababu tu alikuwa karibu na mkuu wa kaya.
hivyo JPG lazima alikalie bango hilo usawa kwa killa mtanzania kuwa na maslahi yanayofanana na uchumi wetu ni muhimu sana si watu kujichotea tu fedha za walipa kodi.hoja zako hapo juu hazina mantiki ni nani mwananchi wa kawaida ameweza kununua hivyo vibanda vya NHC.na hivyo tunadanganywa vya bei nafuu je zikijengwa bangaloo zitauzwa bei gani?ni vema mshahara wa mchechu ukaangaliwa upya kwani shirika ni la wananchi na si la mchechu

NHC ni shirika la 3 now kwa Ubora wa mashirika ya Nyumba africa lakwanza NHS ya SA yapili Ethiopia na Tatu Tanzania. Sasa mnataka huyu kijana wa watu afanye nini? Watu wanaongea hoja ya nyumba za NHC kuwa za bei kali sio za watu wa hali ya Chini.

Thats true but we have to know kwamba Sera ya NHC haijawahi kuwa na sera hiyo ya nyumba za bei nafuu kwa watu wa Hali ya Chini. Hakuna mahala popote NHC iliwekwaa kwaajili ya kujenga makazi ya Wanyonge.

So kama kuna watu tunahitaji NHC iwe ya wanyonge ni kuwakumbusha watunga Sera wetu wakabadili sera ya NHC kuacha kujiendesha kibiashara. Mchechu hata kwa hako ka M30 anatuhurumia tuu.

Wenye vyeo kama chake huko kwenye taasisi aliyotoka sasa hivi wanakula mpaka M75. Ifike mahali tusisukumwe kwa wivu pekee juu ya Mchechu tuache wivu tumuache afanye kazi.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi wako wa kina....haya ndio niliyokuwa nayataka na sio bra bra.....

Kwa mujibu wa maelezo yako( kama ni kweli) basi nami naungana na wadau wanaopinga mshahara wa huyo bwana.....kama hicho ndicho anachoizalishia serikali....
Kwanza huyu bwana uliyem'quote ameanza kumpiga vita Mchechu humu tangia ameteuliwa kuongoza hilo shirika... Na kama pesa anazouza nyumba anaenda kulipa madeni huoni ndio vizuri?? Ili shirika siku moja liwe dept free na mauzo yawe faida kwa shirika na serikali...

Kwamfano umekopa Million 100, ukajenga nyumba 10 za million 10 kila moja, ila kila nyumba ikikamilika unaiuza kwa million 20, ukianza kuuza moja moja unarudisha pesa ya mkopo, zikifika nyumba 5 tayari utakuwa ushalipa mkopo wote na faida ni hizo nyumba 5 zilizobaki... Sasa sijui Mchechu mnampinga kwa lipi...
 
izi kasumba tuu, wapo wataalam zaid yake wanaoweza kufanya iyokazi, mtu anakinga milioni na kwa siku!! Apunguziwe mshahara asee umezidi
 
Mleta mada.nadhani ndio unamuharibia huyu DG wa nhc. Ungekaa kimya criticism yote hii isingekuwepo. Housing market iko kwenye burble na ita.burst muda si mrefu au.imeisha burst. Uliza nyumba ngapi wameuza mpaka sasa. Low income earners ndio wenye shida na.nyumba lakini wao hawajui which customer atanunua nyumba kwa wingi. Usitegemee kawe na moroco hata kigamboni wakaja kuishi waafrika wengi.
 
Kwanza huyu bwana uliyem'quote ameanza kumpiga vita Mchechu humu tangia ameteuliwa kuongoza hilo shirika... Na kama pesa anazouza nyumba anaenda kulipa madeni huoni ndio vizuri?? Ili shirika siku moja liwe dept free na mauzo yawe faida kwa shirika na serikali...

Kwamfano umekopa Million 100, ukajenga nyumba 10 za million 10 kila moja, ila kila nyumba ikikamilika unaiuza kwa million 20, ukianza kuuza moja moja unarudisha pesa ya mkopo, zikifika nyumba 5 tayari utakuwa ushalipa mkopo wote na faida ni hizo nyumba 5 zilizobaki... Sasa sijui Mchechu mnampinga kwa lipi...
Watu hawapingi utendaji kazi wa mchechu bali wanapinga kiwango anacholipwa wanadai hakiendani na kile anachozalisha kwa serikali....
 
Tena hiyo ndogo sana... Mchechu anastahili kulipa Million 70 kama wanavyolipwa DG wengine...
Hasara aliyotuingiza Mchechu tutakuja kuiona baadaye. Baada ya majipu ya mafisadi, wauza unga na wakwepaji kodi kutumbuliwa, mtanzania yupi kwa sasa atakuwa na uwezo wa kununua hizo nyumba? Anatumia gharama gani kurusha matangazo ya kutafuta wateja kwenye tv. Nyumba inayouzika kabla haijaisha hunyakuliwa. Labda wageni waruhusiwe kununua.
 
Neno TUACHE lina maana wengi nakuona wewe uliye jijumlisha na wengi ukasema tuache pengine na mheshimiwa uliye mtaja kwasababau ndani ya hotuba yake ali taja kiwango flani cha fedha kuwa mshahara wa mtu sina hakika kama ali mlenga mtu unaye taka aachwe, kwa hiyo ni aidha wewe na huyo Bwana mkubwa uliye mtaja acheni, wengi tu tuna mkubali Mchechu ungekuwa tu direct kuliko kutumia wingi kumbe una mlenga mtu mmoja.
 
Ninachoka kwa mjadala huu na wa aina yake ambao umekuwa ukifanyika katika mitandao mbalimbali huku ndani ya JF ukijirudia mara kwa mara kwa kuwa ni wa kumzungumzia mtu.

Nafikiri ingekuwa vyema kuangalia nafasi ya mtu na umuhimu wake lakini sio kutumia kigezo cha mtu kwani hata huyu anayetajwa kufanya mambo makubwa ni Binadamu tu ambaye anatajwa kama aliyefanikiwa binafasi badala ya kufanikwa kwa taasisi ikiwa ni pamoja na kuandaa watu "wengine" ambao wanaweza kufanana na "yeye" au hata kumzidi.

Si inafahamika kwamba wakati wa mwalimu waliokuwa wakilpwa zaidi kuliko watumishi wengine kwa wakati huo walikuwa Mkurugenzi mkuu wa huduma za maktaba nchini (TLS) na Makamu mkuu wa chuo kikuu cha UDSM. Sababu yake ilikuwa nini? je kulikuwa na tija? NHC au mashirika na tasisi nyingine hazikuwepo?

Badala ya kujifanya tunafahamu mengi ( ya upande mmoja) zaidi ya ndani juu ya huyu DG wa NHC tangu alipokuwa kabla ya kuingia NHC ni bora tuangalie mfumo uliomplekea hapo ambao kwao utaweka vigezxo vya nani alipwa vipi kwa nafasi gani badala ya kumuangalia mtu.
Tunayo mifano mingi ya watu tuliokuwa tukiambiwa kuwa wanafanya vizuri huko waliko ( Nje ya nchi) lakini wkija nchini hanawana tofauti au wanazidiwa na wale kwa kwenye kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mifumo yetu. Kama Net Group Solutions ilipewa uwezo wa kukata umeme hadi katika taaasisi "nyeti" na kusifiwa kwa kuongeza makusanyo ilihali wazawa wakizuia kukata umeme kwa taasisi hizo ambazo ndizo wadeni wakubwa wa Tanesco na kulauimiwa kwa kushindwa kazi ndani ya Tanesco wategemea nini?
 
Nehemiah K. Mchechu
mchechu.jpg

Nehemiah K. MchechuDirector General
Director General
Mchechu Profile
Nehemia is an inspirational and transformational business leader. He is currently leading the largest Company in East Africa with a Capital base over USD 1.2Billion. He was recruited in this job to undertake the restructuring the State Owned Corporation following his good track record in restructuring the ailing Companies. He has been able to transform the NHC from the Bureaucratic State owned Corporation to among the best performing Companies in Tanzania.

Nehemiah was the former MD & CEO of Commercial Bank of Africa Tanzania Limited before his current job, where he was at that time the youngest CEO within the Banking sector in East Africa up to the time when he moved to his current role. Nehemiah did a transformation and restructuring of the loss making Bank to Profit Making Bank within the shortest period of one year. Prior to CBA, Nehemia worked for Standard Chartered Bank Tanzania Limited, and in his last role he was an Alternative Director, Head of Global and Co-Head Wholesale Banking, during this time he was very instrumental in bringing the new second horizon products and therefore raising the number of products offering from three to twelve all under his stewardship. He has also worked for Citibank and Barclays Bank Tanzania Limited.

Nehemia sits on several Boards including KCB Tanzania Limited, and Tumaini University where he both Heads the Boards Audits Committees, He is the Chairman of the Rightway Schools Board of Directors, is also a Director & Founding member of the CEO Roundtable, a policy dialogue forum that brings together CEO’s of the top 50 companies in Tanzania. He is also saves as a Presidential appointee in two Committees under the Tanzania Business Council where he serves on the Land Development Committee and also on the Public Private Sector Partnerships. He also saves as the as a member of the National Economic Task Force Team.

Nehemiah has saved before as a board of Director in Different Institutions and member to various Task Forces and technical Committee within the Private and Public Sector. He is also a mentor and runs a leadership program for young People who want to stand high among their best peers.
 
Fikra kama zako zilijaribiwa na wajamaa wa China miaka ileeee lkn wakachemsha vibaya sana,sasa hivi jamaa wamekuwa mabepari kuliko hata Wamarekani wenyewe,huwezi kuamini kuwa China siku hizi pia kuna mabilionea,so hakuna kitu kinachoitwa usawa ktk dunia hii ndugu yangu,ndo maana tumezaliwa tukiwa tunatofautiana ktk tabia,urefu,rangi,nguvu,akili,vipaji.Haya yote yanatokea kwasababu maalum.
Nimeshangazwa unapolalamika eti jamaa analipwa mshahara mkubwa sana,sasa nyinyi mnataka alipwaje?mshaurini Magufuli ampige chini kisha amtafute DG mwingine wa kulipwa shilingi milioni 2 kwa mwezi halafu tuone hayo mashirika ya umma yatafika wapi, halafu eti mnataka kuanzisha viwanda,kwa fikra za namna hii hivyo viwanda vitakufa tena ndani ya muda mfupi maana hakuna mtu mwenye sifa stahiki za kuvisimamia viwanda akakubali kulipwa peanuts kiasi hicho,mtaishia kuwapata watu wenye shida za ajira lkn waliokosa sifa stahiki.Duniani kote successful companies huvutia brightest brains kwa kutumia handsome payments au kuwa_retain waliopo kwa kuwalipa handsomely. Acheni kuishi ktk fantasy land nyinyi wajamaa.
Mtamkumbuka kikwete, ten years mlibembea sana na matusi na kejeli juu kwa wananchi,unatetea mafanikio ya watu waliokwiba pesa za umma,arudi sasa kwenye hiyo asasi hakuna mtu atahoji,nhc ni mali ya umma,

halafu natoa maoni kwa magufuli hawa mameneja na wakurugenzi walipwe mil 2 tu na mawaziri mil 3, kwanza serikali haina pesa, pili kubana matumizi, tatu hizo ni kazi za kuhudumia jamii kama ilivyo kwa walimu na madaktari anae taka afanye huwezi kwendaa!mmetusumbua sana huku kitaa na pesa za ufisadi,

nakumbuka kisa kimoja nilikutana nacho kwa mziba pancha,wakati mimi na bargain jamaa aniuzie tairi used kwa elf 30,akaibuka yule meneja wa bank bot yeye anataka jamaa amchekie upepo matairi,basi jamaa akacheki tairi zote zikawa sawa,akamwambia tayari bosi ni elf 1 alahaulaa! Meneja anamwambia mziba pancha hii ni range wewe kupima upepo sio elf 1,akatoa elf 40 akampa jamaa huyo akasepa zake,sasa si kaniachia msala mimi kabla meneja hajafika mziba pancha alikua anaelekea kunipa tairi kwa elf 30,baada ya kupewa ile 40 kabadilika bwana ananiambi bro hili tairi mwisho elf 50 na yeye nae aka anza kunitia vijembe ananiambia braza magari haya gharama usilazimishe kama vp uza gari yaani ! Nilitoa hiyo 50
 
without detailed explanation, 35,000.000.00 is a meaningless figure. Tupeni ushahidi wa kisayansi juu ya mchango wa Mchechu kwenye hili shirika. alilikuta likoje na sasa likoje. Lilikuwa na shiling ngapi na sasa linashiling ngapi? value of the company in case the government decides to sell it today?
Je, NHC ina board? Na mshahara wa NHC unapangwa na board na siyo Managment. Management inapendekeza tu. Mbona board haitajwi popote katika lawama hizi? Je, CEO wa alikotoka Mchechu analipwa shiling ngapi now? Kama shirika ni la tatu africa. similar ceO wa nchi nyingine wanalipwaje?
MDUDU URGENCY ALITENGENEZWA NA WAPIGAJI SERIKALINI. LAKINI HIYO NI MADA NYINGINE ITAKUJA MUDA MWAFAKA.
 
Mafanikio ganiiiiii? Kwanza huyo hakufuatwa na Serikali inaonekana ulianzisha mada hii umesahau Mada iliyomhusu Mchechu humu JF pindi Jengo refu la Indira Gandhi lilipo poromoka na kuua watanzania kibao. Huyu Mchechu aliomba kazi kitambo kupitia Shirika moja la Kimataifa katika Usaili na linaloheshimika sana Tanzania na Duniani kote. Alifeli katika michakato ya usaili lakini Figisufigisu zikafanywa akapewa ulaji kwa maslahi ya watu. Hivi wewe ukipewa MAHELA na support yote kutoka Serikali tena na mihela mingine ni mideni kwa Serikali utashindwa kusimamisha mijengo? Hebu niambie Nyumba ya bei nafuu ni Mil. 60 - 80 ya vyumba 3? Halafu Viwanja anajiuzia mwenyewe. Huyu cheki bobu alizani Kijibenki alichokuwa anakiongoza ni sawa na kitu kinaitwa SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA lidude,kubwa. Matokeo yake kaingia kichwakichwa kimenuka kudadadeki... eti mshahara Mil. 35. Anakula nini? anaishi wapi? labda Dubai kila jioni baada ya masaa ya kazi anachukua ndege ya kukodi anarudi kupumzika hadi kesho yake kazini. Vinginevyo aje hapa ajustify matumizi ya Mil. 35. Jipu hili.
Acha upotoshaji, nyumba za bei nafuu ni million 35.Mara oh alifeli usahili brah brah,umejawa na fikra za kimaskini tu.
 
Nehemiah K. Mchechu
mchechu.jpg

Nehemiah K. MchechuDirector General
Director General
Mchechu Profile
Nehemia is an inspirational and transformational business leader. He is currently leading the largest Company in East Africa with a Capital base over USD 1.2Billion. He was recruited in this job to undertake the restructuring the State Owned Corporation following his good track record in restructuring the ailing Companies. He has been able to transform the NHC from the Bureaucratic State owned Corporation to among the best performing Companies in Tanzania.

Nehemiah was the former MD & CEO of Commercial Bank of Africa Tanzania Limited before his current job, where he was at that time the youngest CEO within the Banking sector in East Africa up to the time when he moved to his current role. Nehemiah did a transformation and restructuring of the loss making Bank to Profit Making Bank within the shortest period of one year. Prior to CBA, Nehemia worked for Standard Chartered Bank Tanzania Limited, and in his last role he was an Alternative Director, Head of Global and Co-Head Wholesale Banking, during this time he was very instrumental in bringing the new second horizon products and therefore raising the number of products offering from three to twelve all under his stewardship. He has also worked for Citibank and Barclays Bank Tanzania Limited.

Nehemia sits on several Boards including KCB Tanzania Limited, and Tumaini University where he both Heads the Boards Audits Committees, He is the Chairman of the Rightway Schools Board of Directors, is also a Director & Founding member of the CEO Roundtable, a policy dialogue forum that brings together CEO’s of the top 50 companies in Tanzania. He is also saves as a Presidential appointee in two Committees under the Tanzania Business Council where he serves on the Land Development Committee and also on the Public Private Sector Partnerships. He also saves as the as a member of the National Economic Task Force Team.

Nehemiah has saved before as a board of Director in Different Institutions and member to various Task Forces and technical Committee within the Private and Public Sector. He is also a mentor and runs a leadership program for young People who want to stand high among their best peers.
Mnaotilia shaka uwezo wa huyu jamaa someni hii C.V
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom