Ttcl waja na kasi mpya, bei mpya na mfumo mpya wa malipo ya unlimited broadband

Akthoo

JF-Expert Member
Nov 5, 2007
998
1,015
Kwa wale wapenzi UNLIMITED BROADBAND leo nimeinasa hii:-

"Napenda kuwafahamisha kua TTCL imefanya marekebisho ya huduma zake za broadband zisizo na kikomo (unlimited packages) katika maeneo yaliyotajwa hapo chini. Promotion hii inajulikana kama NDUKI PROMOTION. Katika promotion hii neno NDUKI limetumika ili kumaanisha kitu chenye KASI kubwa kuliko vingine, kwa mfano mchezaji wa mpira wa miguu akipiga shuti lenye kasi kubwa inajulikana kwa lugha ya kimpira kua amepiga NDUKI kubwa, mwanariadha akikimbia kwa kasi kubwa pia inajulikana kama mkimbiaji huyo hua anatoka NDUKI.

Faida za NDUKI BROADBAND:

Miongoni mwa faida za NDUKI BROADBAND ni kama ifuatavyo:


  • Kumekua na ongezeko la kasi (speed)
  • Kumekua na punguzo kubwa labei (kwa mwezi)
  • Mfumo wa kulipia umebadlika kutoka mwezi kwa mwezi (kalenda month) kua siku 30 toka mteja aongeze salio.
  • Mteja anapata connection kwa siku thelathini (30) toka siku aliyoongeza salio.


Vifurushi:

Huduma hii imegawanywa katika vifurushi mbalimbali kulingana na mahitaji na ladha (demand and taste) ya wateja wetu kama ifuatavyo:


  1. 256 kbps – NDUKI Bronze (30,000/-)
  2. 512 kbps – NDUKI Silver (60,000/-)
  3. 1Mbps – NDUKI Gold (100,000/-)
  4. 2Mbps – NDUKI Diamond (200,000 )

Lengo la internet isiyo na kikomo

  1. Kumwezesha mteja kutumia internet yake kwa siku thelathini (30) bila kukatika
  2. Kumwongezea mteja hali ya kutumia na kuridhika
  3. Kuongeza kasi ya internet
  4. Kuwavuta wateja wengi wadowadogo na wa majumbani

Faida kwa wateja


  1. Intaneti ya bei nafuu kuliko zote Tanzania. Vifurushi vya gharama ya chini kwa mwezi mzima.
  2. Wigo mpana zaidi wa uchaguzi wa vifurushi vya mwezi (siku 30) kulingana na mahitaji ya mteja
  3. Huduma ya Intaneti yenye ubora na ufanisi wa hali ya juu
    1. Kasi ya ajabu
    2. Intaneti ya uhakika
    3. Kupakua (download) taarifa kwa muda mfupi
    4. Intaneti isiyo na kipimo cha matumizi kwa bei ile ile kwa mwezi mzima (siku 30)
    5. Waweza kuongeza muda wa matumizi ya siku 30 wakati wowote.
    6. Husaidia kupanga bajeti ya matumizi ya intaneti kwa mwezi.

Vipengele muhimu kwa mteja:


  1. NDUKI BROADBAND haina KIKOMO CHA MATUMIZI.
  2. NDUKI BROADBAND ina KASI KUBWA kuliko internet zote nchini
  3. BEI ya NDUKI BROADBAND kwa mwezi imepunguzwa
NDUKI BROADBAND ndio internet yenye UHAKIKA wa kumwacha mteja akiwa ameungainishwa kwa mwezi mzima (siku 30)."
 
Umezungumzia ".... maeneo yaliyotajwa.." lakini hukuyataja. Ni maeno yapi hayo inapopatikana hiyo Nduki???
 
Source Tanzania Telecommunications Company Website Home

BB_Swa.jpg
 
Nakesha nikiomba mashirika kama TTCL yapate vichwa kama NHC ilivyompata Nehemia Msechu. ...Turudi kwende mada.

Kampeni si mbaya na jina linakolea kichwani japo baadhi huchukulia NDUKI kama mkimbio wa kukurupuka na kuzimika ghafla. Nina walakini maana hiyo hiyo ikapachikwa katika kampeni yenu.

Pili, picha mnayotaka kupata machoni mwa wateja wenu ni MBIO, WEPESI, KASI,......... Nionavyo kifurushi cha 256 kbps ambacho mmekibatiza - NDUKI Bronze kitaondoa maana ya NDUKI ama sivyo mmedhamilia kutoa tafsiri mpya ya NDUKI kuwa ni POLEPOLE, MWENDO WA KONOKONO, n.k hata kifurushi cha 512 kbps hakiwezi kuleta au kubeba maana mnayotaka kuchora vichwani mwa wateja wenu.

Ushauri wangu:
Key word ya NDUKI ibaki kwa kifurushi cha 1Mbps na 2Mbps. Badala ya kuthamanisha kwa vito tofautisheni kwa maneno NDUKI na NDUKI KALI
 
sasa mkuu kaa umeikamata hyo si ungetumegea full details, au ungetuwekea link. asante mkuu
 
Ukiiba mke wa mtu na kufumaniwa kama Mwigulu unatoka NDUKIIIIII....

Kama wanafikiri bado tunanunua internet kwa 5 digits (30,000) basi wataizika kampuni yao. wenzao airtel kitu cha 4 digits (2,500) unakamata 400MB ambazo mwezi nzima unakamulia mtandao. Unipe unlimited access kwani nina internet cafe, na usiku nikilala na unlimited yangu nayo inalala. Nipe kitu limited but cha bei poa
 
Source ni TTCL Makao Makuu; SAMORA av.
Watatoa matangazo kwenye MEDIA anytime from today.
 
Hebu TTCL WAJIPANGE HIZO MODEM ZAO MAENEO KIBAO HAPA DAR HAZIFANYI KAZI..NETWORK IKO LOW ILE MBAYA MFANO UKONGA,TABATA,KITUNDA,BUZA,YOMBO,G/MBOTO HATA SASATEL WANAWASHINDA. TTCL JIPANGENI, ONGEZENI MINARA HAPA DAR.
 
Hizi bei bado hazipo kiushindanii, zimekaa kisanii zaidi labda wawabambikie watu wa huko sirikali hao wengi wao hata hawajui nini kinaendelea dunia hii wanawaza kutomis zile check up za india za yale magonjwa yao
 
Na banjuka bado ipo? Ila dah customer care ya ttcl inabidiitathiminiwe upya
 
Back
Top Bottom