TTCL home Internet Installation Manual

JITU BANDIA

JF-Expert Member
Feb 5, 2023
2,680
6,025
Habarini wakuu, poleni na majukumu. Moja kwa moja kwenye mada.

Ni hivi, Shida yangu ni hii nna imani tuna ma IT gurus wengi kwenye haya maswala humu. Mimi niko mkoa wa X wilayani Y, huku niliko kuna mnara wa TTCL na inatoa huduma.

Sasa niliongea nao kuhusu kununua router na kufanyiwa installation. Wamekuja jana kukagua eneo nililopo na wameuona mnara uko karibu kama mita 180_230 hivi tokea mahali nilipo, wakasema pako Sawa kabisa!

Shida inakuja hivi mimi ni mgeni kidogo kwenye hivi vitu, wananiambia sijui GHARAMA ya router, sijui radio na kuunganisha ni 500,000/=

Nimeogopa kupigwa maana walikuwa kama 6 kwenye gari yao maana naona kama ni parefu mno kulinganisha na nnavyofikiri, kulinganisha bei ya router yenyewe.

Naweza kupata mchanganuo wa vitu vinavyohitajika hapa, GHARAMA zake, Ili kufungwa home internet.

Na kama naweza kuvinunua kwao tu ama nje ya hapo? Na je naweza fanya installation mwenyewe kwa kufuata manual!?

Ntashukuru nikisaidiwa kwa hili. Na je hizo GHARAMA ni rafiki kwa experience Yenu wakuu huku mkoani Mara?

Asanteni....

Cc Chief-Mkwawa Mwl.RCT IT Guru na wengineo msaada please...

Natanguliza shukrani wakuu Maguru wa hizi mambo.
 
Kama ni fiber mwaka jana walitoa tangazo kuwa wanafanya free installation.

Ila sasa changamoto ni kuwa hata uwafate mara ngapi hawaji kukufungia.

Itokee tu labda upo katika eneo ambalo lina mchanganyiko wa watu wengi kama centre au ushuani hapo ndio watakuja kirahisi.

Ila kama ni huku Gomzi au Chanika utakesha.

So kama wamesema 500,000 halafu ukiangalia mazingira unaona sio ya centre basi we wakubalie tu kama hiyo pesa unaimudu.
 
Huku ni mkoani mkuu, wilayani center kabisa karibu na mnara wao, Sidhani kama ni fiber, maana fiber ni mijini huko kama Dsm
 
Hapa naumiza kichwa na voda router yao ni 615000 kifurushi ni 120k
 
Super kasi mbona nayo ni free installation hata humu wapo ambassador kibao na matangazo yao?
Labda ile ya postpaid tena nayo kuna malipo ya awali pia kutegemea na ni ya home au ofisi

kama unayo hiyo post kuna free installation nitag man nione
 
Mkuu hiyo 500K router halaf vifurushi ndo kama hivi vya kwenye simu au unapata kama vile vya fiber na copper waya yan ukinunua hiyo router kwa 500K wanakupa vile vya unlimited?
TTCL zote Copper na Fiber Router na installation ni bure kabisa hulipi hata sh 10, na ni unlimited.

Sema kunakua na uhaba wa router hasa hio Copper (adsl) muda mwingi router zimeisha hivyo inabidi ununue mwenyewe, hao mafundi sasa ndio wanakudalalia. Ila kiuhalisia hizo router hazina thamani ya laki 5. Vyema ukanunue mwenyewe dukani.
 
Habarini wakuu, poleni na majukumu. Moja kwa moja kwenye mada.

Ni hivi, Shida yangu ni hii nna imani tuna ma IT gurus wengi kwenye haya maswala humu. Mimi niko mkoa wa X wilayani Y, huku niliko kuna mnara wa TTCL na inatoa huduma.

Sasa niliongea nao kuhusu kununua router na kufanyiwa installation. Wamekuja jana kukagua eneo nililopo na wameuona mnara uko karibu kama mita 180_230 hivi tokea mahali nilipo, wakasema pako Sawa kabisa!

Shida inakuja hivi mimi ni mgeni kidogo kwenye hivi vitu, wananiambia sijui GHARAMA ya router, sijui radio na kuunganisha ni 500,000/=

Nimeogopa kupigwa maana walikuwa kama 6 kwenye gari yao maana naona kama ni parefu mno kulinganisha na nnavyofikiri, kulinganisha bei ya router yenyewe.

Naweza kupata mchanganuo wa vitu vinavyohitajika hapa, GHARAMA zake, Ili kufungwa home internet.

Na kama naweza kuvinunua kwao tu ama nje ya hapo? Na je naweza fanya installation mwenyewe kwa kufuata manual!?

Ntashukuru nikisaidiwa kwa hili. Na je hizo GHARAMA ni rafiki kwa experience Yenu wakuu huku mkoani Mara?

Asanteni....

Cc Chief-Mkwawa Mwl.RCT IT Guru na wengineo msaada please...

Natanguliza shukrani wakuu Maguru wa hizi mambo.
Achana nao spidi yao sio nzuri vuta hawa
 
Attachments

  • Screenshot_20230805-214907.jpg
    Screenshot_20230805-214907.jpg
    105.7 KB · Views: 17
Back
Top Bottom