Tsh. 35m itanifikisha hatua gani kwa nyumba ya aina hii?

Size: 9m x 10m
Fence : 20m x 20m
Kiwanja tambarare
Self room 1
Bedroom 1
Dining
Sitting room
Kitchen
Public toilet
Paving blocks nje

Karibuni wakuu.
Tafuta ramani nikutengenezee boq kwa garama ndogo sana au hata km ramani huna naweza kukutafutia

Ujenzi una taratibu zake. Lazma uanze design stage jinsi room zinavyokaa na ukubwa wake ndo utapata makadirio halisi baada ya kupata BOQ. Uzur wa kuwa na BOQ utapata wastani wa makadirio ya garama kuanzia material mpk ufundi kwa stages mbali mbali. Kazi kwako ni kuangalia hela yako itafika stage gani na utapata picha nzima ili nifike stage flani nitahitaji garama gani na material kiasi gn kwa bei gn

Hizi ndio taratibu za ujenzi dunia nzima ukifwata taratibu huwez kukwama au kupata hasara ya ajabu ajabu mahali. Tatizo tunataka magumashi. Ndo maana hata watu wanapigwa na mafundi unaambiwa sehemu kuna hitaji mifuko 50 ya cement wakt ni sehemu ya mifuko 20 au ndoo za rangi 30 badala ya 15 fundi anakupiga kwa sbb we hujui unalolifanya na unakurupuka tu hata useme unanunua material ww atakupiga kwa kukupa hasara ya kununua material nyingi ili apate nafac ya kukuibia. Njia pekee ni wewe kuelewa mahitaji ya nyumba yako unampa kutokana na nn kinachohitajika kwa stage gn
 
Size: 9m x 10m
Fence : 20m x 20m
Kiwanja tambarare
Self room 1
Bedroom 1
Dining
Sitting room
Kitchen
Public toilet
Paving blocks nje

Karibuni wakuu.

Kwa 35m utahamia kabisaa, ila ondoa fence na paving, kitakachobaki, malizia fence, paving mwisho.
 
Inategemea na manjonjo katika umaliziaji!!
Mfano mdogo gharama za kuweka madirisha ya aluminum au gril ni pesa tofauti.

Kuweka "tales" au kupaka rangi sakafu ni pesa tofauti.

Upauaji nao unagharama tofauti kulingana materials na bei ya fundi
 
Inategemea na manjonjo katika umaliziaji!!
Mfano mdogo gharama za kuweka madirisha ya aluminum au gril ni pesa tofauti.

Kuweka "tales" au kupaka rangi sakafu ni pesa tofauti.

Upauaji nao unagharama tofauti kulingana materials na bei ya fundi
Lakini kuna standard price range ya bei ya ufundi mfano kujenga tofali moja la block range price tshs 300 mpk 500 kutegemea na halali na mahali na km unajenga gorofa au nymba ya chini hizi ni bei za tanzania nzima haijalishi uko masasi, katavi, au dar es salaam
 
Baada ya kujifunza mambo kadhaa kutokana na makosa kwenye ujenzi,nakushauri uanze na fence.
Makadilio ni tofali 2000-2500
Nondo 15
Cement 25 NK. Makadilio pamoja na geti sh 7m

Then Anza ujenzi wako.
Msingi na jamvi 5m
Boma zima 5m
Kuezeka hapa inategemea unapandisha bati kwa mita ngapi kwenda juu,makadilio tuweke pamoja blandaling 7.5m
Magrill ya milango na madilisha 1.5
Plasta 2.5
Tyler's 6m

Haya ni makadilio ndugu yangu,yanaweza kuongezeka kidogo au kushuka kidogo,muhimu sana hakikisha unaisimamia mwenyewe mwanzo mpaka mwisho.
Umuhimu wakuanza na uzio Kwa karne tulionayo upe kipaumbele, binadamu tumekosa utu now day's.
All the best chief
 
Size: 9m x 10m
Fence : 20m x 20m
Kiwanja tambarare
Self room 1
Bedroom 1
Dining
Sitting room
Kitchen
Public toilet
Paving blocks nje

Karibuni wakuu.
Simple finishing bila fence kama kiwanja flat na mchanga hununui.
 
Kwa 35m utahamia kabisaa, ila ondoa fence na paving, kitakachobaki, malizia fence, paving mwisho.
Hawezi kuhamia bila kuwa na maji.
Mfumo wa maji safi na majitaka (kumbuka kuna chumbaa self) utamgharimu 6 to 10m.
 
Kuna vitu kwenye ujenzi havisemwi ila vinakula pesa.
1. Shimo la Maji taka.
2. Gharama za Ufundi.. Boma, plasta,Paa, Tiles, ragi nk nk
3. Maji, kumwagia maji, kifusi cha Backfilling, Kushindilia boma, mbao za kumwagia beams, Ununuzi wa kokoto, vibarua wa kujaza vifusi nk nk.
4. Kubwa kuliko Ulipe fundi anatokomea bila kuonekana site ametoroka kazi.
Sometimes tulipe kodi za Wenye nyumba wetu bila usumbufu jamani. Kujenga ni pasua kichwa.
 
Back
Top Bottom