Kima mdogo
JF-Expert Member
- Sep 17, 2011
- 303
- 46
Wanandoa hawa walikutana na wakiwa na hali duni kimaisha, wakaoana na kujaliwa kupata mtoto 1 wakike,kadri siku zilivyoenda MUNGU akawajalia wakafanikiwa kimaisha na wanamiliki mali kadhaa,miaka 7 ikapita mke akabeba mimba kwa bahati mbaya mimba ikatoka, akamweleza mama mkwe wake hapo ndo matatizo yalipoanza,Mama mkwe na Mume wakaanza kumsengenya kuwa hazai,mama mkwe akafikia hatua ya kusema mwanae aoe mwanamke mwingine,Mke akawa analia na Mungu kila siku,Siku 1 mama mke akaja akamkuta mke huyo anaumwa akasema wala haumwi ni mamizimu ya huko kwao,huyu dada aliumia sana kwani hajui uchawi wala mizimu akamweleza mumewe maneno aliyoongea mama yake,mume kumuuliza mama yk akakataa katakata na kudai kuwa mwali wake kamsingizia ili asije kwa mwanae, kwa bahati nzuri Mke akapata ujauzito mume wake akaanza kumnyanyasa,kumtukana na kumnyima hela ya matibabu kwa shinikizo la mama yk kuwa alimsingizia, mke huyu akawa analia kila siku hali iliyomletea matatizo makubwa madaktari wakamzalisha mtoto wa miez 7