SoC03 Treni ya mizimu

Stories of Change - 2023 Competition

Nicas Athanas

New Member
May 23, 2023
1
3
Moja kati ya visa ambavyo bado vinaumiza vichwa vya watu mpaka leo hii ni kisa cha Treni Moja ya Kampuni ya Zannetti. Treni ambayo inadaiwa kupotea miaka ya 1800’s na imekuwa ikionekana kwa baadhi ya vipindi vya miaka, huku mara ya kwanza

Ikionekana miaka takriban 60 baada ya kupotea. Treni ya Zannetti, inasadikika kuwa ni moja kati ya Vitu vinavyosafiri katika muda (Time Travel). Kwa zaidi ya karne moja sasa. Vimekuepo visa vingi sana vyote vikijaribu kusimulia matukio mbalimbali yanayoihusu treni hii ya.

Zanetti. Lakini leo nimekuandalia kisa kimoja maarufu ambacho ndicho kiliipa umaarufu Treni hii ambayo imebatizwa majina mengi ikiwemo… Treni Ya Mizimu. Hii ni kwa sababu inasafiri katika Muda. Treni ya Zannetti inasadikika ipo katika safari ambayo haina Mwisho.

Historia inatuambia kwamba...Katika majira ya Joto mnamo mwaka 1911, treni iliyoitwa Zanetti yenye mabehewa matatu iliondoka katika mji wa Roma huku ikipaswa kupitia katika reli ya chini ya mlima (handaki) huko Lombardy nchini Italia. Kitu cha kushangaza ni kuwa.

Mara baada ya kuingia katika handaki hili ambalo lilikua na urefu wa takribani km. 1 treni haikutoka katika upande wa pili. Huku ikirekodiwa kuwa na jumla ya abiria 106 ambao waliianza safari ambayo hawakujua kama itakua haina mwisho. Mara baada ya mkasa huu…

Mamlaka za usafiri wa reli katika jiji la Roma walifanya juhudi za kuitafuta treni hiyo kwa kuingia ndani ya handaki hilo lakini hawakuipata. Taarifa hii haikua nzuri na iliwatia mashaka watu wengi, treni haikuonekana na haikujulikana iko wapi – handaki likafungwa…

Wakati wengi wakidhani labda taarifa zile ni za uzushi Walijitokeza watu wawili ambao walijitambulisha kua ni abiria waliokua katika treni ile ya Zannetti. Mara baada ya mahojiano ya muda…walidai kua mara baada ya kuingia ndani ya handaki lile, waliona mwanga mkali mbele yao

suala lililowafanya wao kuruka na kuitosa treni ile ambayo iliishia kupotea na isipatikane tena. Habari za kupotea kwa treni hii zikajadiliwa kwa kiasi chake kwa kipindi fulani cha muda na hatimae zilianza kusahaulika kwa waliowengi katika watu.

Lakini mwaka 1926 nchini Mexico kuna mwanafizikia mmoja alikuwa anapitia rekodi na mambo yaliyowahi kuandikwa katika miaka ya nyuma, akakutana na nukuu iliyoandikwa mwaka 1845. Nukuu hii ilieleza juu ya watu 104 ambao walikua na asili ya Italia waliojitokeza kutoka sehemu ambayo

Haikujulikana katika nchi hiyo ya Mexico, watu hawa walikua wamepotea na treni yao waliyokua safarini wakitokea huko jijini Roma, Italia. Nukuu hizi kupatikana mwaka 1926 zilizoandikwa miaka ya 1800’s zikijaribu kuelezea habari za treni ilopotea miaka ya 1910’s zilikua dhahiri

Ni ishara ya kua ile Treni ya Zannetti huenda ni kweli ilisafiri katika muda (Time Travel). Yaani ilitoka katika wakati wa sasa na kurudi katika wakati wa nyuma… ama ilitoka wakati wa nyuma na kuonekana katika wakati wa sasa, hakuna aliyefahamu.

Lakini taarifa ya mwanafizikia huyo ya miaka ya 1800’s ilieleza kuwa… Wataliano hao ambao hata hivyo walionekana kama ni watu wenye matatizo ya akili… Walihifadhiwa katika hospitali ya wagonjwa wa akili huko nchini Mexico… Kuzuka kwa habari hizi mara moja ziliifanya treni ya

Zannetti kupewa jina la Treni ya Mizimu… Sio hilo tu, ni maeneo mengi sana treni hii imeripotiwa iliwahi kufika kwa vipindi tofauti tofauti vya wakati. Moja kati ya nchi hizo ni Urusi, India na Ujerumani, Italia, Ukrane bila kusahau Romania.

Taarifa nyingi za mashahidi wanaodaiwa kuiona treni hiyo katika maeneo hayo wanasema kwamba treni hiyo mara zote imekua ikipita pasipo kutoa miungurumo ya kawaida kama treni zote. Pia madirisha katika treni hiyo yanaonekana mara zote kama pazia.

Lakini, October 29, 1955 treni ya Zannetti ilionekana ikipita huko Crimea, Urusi. Mashuhuda walioiona wanasema, ilionekana ikitembea kwenye reli ambayo haikuwepo hapo mwanzo, walishangaa kuona kuna Reli katika eneo ambalo haikuwepo hapo kabla. Treni ilipita na Ikagonga kuku.

Kisha Ikapotelea pasipo julikana.
Mwaka 1991 pia ilionekana ikipita huko Poltava, Ukraine na ilikuwa imepita tena katika sehemu ambayo hakukuwa na reli kabla, Mchunguzi mmoja wa kuchunguza mambo ya kutisha aliifuatilia treni ya Zannetti ajaribu kuchunguza na kujua chochote, Lakini Mpaka leo hii hajawahi kupatikana popote. Ni kisa cha kweli? SIJUI – Ninachojua tu ni kimeandikwa tena kwa zaidi ya Mara moja.

Kalamu Yangu imefikia Tamati.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom