Treni laacha watu 1000

Oct 2, 2011
61
12
Treni lenye route ya stesheni mpaka Ubungo maziwa likiwa na mabehewa sita limewaacha abiria zaidi ya 1000 waliokua wakisubiri kupanda katika kituo cha kamata.abiria hao ambao wengi wao wametokea kariakoo wamesubiri treni hilo kwa muda wa Saa nzima treni limekuja toka stesheni likiwa tayari limejaa.nimeongea na baadhi ya abiria wamesema kuna umuhimu mkubwa wa mabehewa kuongezwa.nadhani TRL wamepiga mahesabu madogo sana.
 
Hayahayaa Dr mwakyembe kazi ni kwako kula vichwa hvyo laki nne mnaikosa hivi hivi kwa siku,je kwa mwaka sh ngapi mnapoteza?
 
Hii ni changamoto nyepesi kwa hatua alikofikia. Nashauri waite mabehewa yalikuwa yanafanya safari za mwanza ili kuongeza nguvu wakati wa asubuhi na jioni walau behewa 10 hadi 12. Ni mwanzo mzuri sana Mwakyembe
 
Kwani linauwezo wa kuchukua abiria wangapi kwa Waikati mmoja.?

Abiria wapatao 80 kwa behewa. Treni ina mabehewa matano hadi sita kwa hiyo safari moja inaweza kubeba abiria zaidi ya 400 na karibia 500 mkuu... mwanzo mgumu, ni changamoto ya kufanyiwa kazi kwa kweli.
 
Hii ni changamoto nyepesi kwa hatua alikofikia. Nashauri waite mabehewa yalikuwa yanafanya safari za mwanza ili kuongeza nguvu wakati wa asubuhi na jioni walau behewa 10 hadi 12. Ni mwanzo mzuri sana Mwakyembe

Huyu ndio Dr. wa kweli, ameonyesha kiwango cha usomi wake kwa vitendo na sio kuningíniza usomi wake ukutani. Amekula ngómbe hatashindwa mkia.
 
Watu 1000 wachache sana. dar ina wakazi million 5

sio wote 5 mil..wanaishi UBUNGO CHAMUHIM LAZIMA RELI ZIWE 2 THE TREN KILA DAKIKA 20 IJE NYINGINE HAPO KIDOGO ITASAIDIA KUPUNGUZ kelo waonge na NSSF waongezee mtaji kwani gharama zitarudi mapema
 
Inaelekea Mh. Mwakyembe amekurupuka kwa nia ya kutafuta umasrufu. Town train gani ikishapita usubirie masaa! Si ndio watu badala ya kuwahi kazini watachelewa zaidi!

Halafu town train zenyewe za kuchakachua kwa kuokoteza na kuunga unga. kwa nini wasiokoteze na kuunga mengi yapite kila baada ya robo saa?

Any way miongoni mwa mafisadi angalau Mwakyembe ameonyesha ubunifu, tumuunge mkono labda siku nyingine atakuja na town train za ukweli badala ya kuendeleza mfumo wa uchakachuaji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom