Tovuti 334, akaunti za Facebook 361, Instagram 198 zafungiwa kwa kutangaza Mapenzi ya jinsia moja

Kwa tovuti sina shidaa ila hizo account za facebook na instagram ndo nashangaa wamezifunga vip...
Hapo watupe ufafanuzi, kwa sababu META wanaukubali ushoga, je TCRA walitumia mbinu gani kuwashawishi META wazifunge hizo akaunti, au unaweza kufunga akaunti za FB bila kuwashirikisha META?
 
Kuna askari magereza alishafafanua humu kwamna ni kosa kubwa sana kufanya hivyo vitendo huko Magereza
Hamna kitu hizo sheria hazitekelezeki unawafunga wanaume bila ya kuwaruhusu kufanya ngono na wenzi wao ni lazima wafirane ili kuondoa kiu.

Na pia kwa mujibu wa "ngono kinyume na maumbile" ina maana hata punyeto na oral sex pia ni makosa ya jinai?
 
Kwa tovuti sina shidaa ila hizo account za facebook na instagram ndo nashangaa wamezifunga vip...

Hawana uwezo wa kufunga account hasa hizo za twitter, facebook na instagram maana wamiliki wa hizi tovuti ni wa nchi zinazoheshimu hao mashoga. Hapo watakuwa wanadanganyana kwakuwa wengi huko bungeni hawajui kitu kuhusu tehema. Labda tovuti fulani fulani lakini sio account za watumiaji.
 
TCRA wana access ya kuweza kublock huduma fulani kwenye nchi hii, iwe specific au General, unaweza kufungiwa.

Umejiuliza mbona Tovuti za Ngono, au ukiingia YOUTUBE akaunti za ngono huzioni?

Tovuti za ngono wazifungie wakati wao wenyewe wanashinda humo kuziangalia? Hivi kuna watu wanachukulia habari za hilo bunge serious?
 
Ushoga hauna madhara yoyote kwenye Kodi zetu na Tozo zetu ila hao Covid 19 na hao waliobainishwa kupora matrilioni na CAG wana madhara kwenye Wallet zetu.
 
TCRA wana access ya kuweza kublock huduma fulani kwenye nchi hii, iwe specific au General, unaweza kufungiwa.

Umejiuliza mbona Tovuti za Ngono, au ukiingia YOUTUBE akaunti za ngono huzioni?
Hivyo sio kufungia bali wanazuia usifikiwe na ip address ila ukurasa upo pale pale
 
Mbona yale mapunga james nani sijui , yule punga wa wasafi, na yule punga mwingine mweusi ana kitambi hivi bado yanakata mauno tu huko instagram
 
Fuatilia yanayojiri Bungeni kwenye Bunge cha 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 8 leo Aprili 17, 2023.


SERIKALI YACHUKUA HATUA KUFUNGIA TOVUTI NA MITANDAO YA KIJAMII
Akizungumzia hatua zilizochukuliwa kupambana na wanaotangaza mapenzi ya jinsia moja, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema tovuti 334, akaunti za Facebook 361, Instagram 198, Twitter 12 vikoa zaidi ya 2,456 vimefungiwa

Awali, Anatropia Lwehikila Theonest aliuliza swali Bungeni kuwa Sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu mapenzi ya jinsia moja? Ambapo Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Pauline Philipo Gekul amesema “Kifungu cha 9 cha Sheria ya Ndoa kinatafsiri Ndoa ni mahusiano ya hiyari kati ya Mwanaume na Mwanamke

Ameongeza “Pia Kifungu cha 154 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 kinabainisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile ni kosa la jinai na adhabu yake ni kufungo cha maisha jela au kisichopungua miaka 30 jela.”

MIUNDOMBINU YA DAR HALI NI MBAYA, MVUA ZIKINYESHA KAZI HAZIFANYIKI
Mbunge wa Segerea, Bonnah Ladislaus Kamoli amesema “Mvua ikinyesha Kisarawe maji yanakuja Ilala, hasa katika majimbo ya Segerea, Ukonga na Ilala kutokana na miundombinu mibovu.”

“Mfano juzi Wananchi wa Kata ya Vingunguti na Mnyamani wameshindwa kutoka ndani hadi tulipoomba msaada wa kampuni inayotengeneza barababa kusaidia kuondoa maji.”
UCHUMI wa TANZANIA imekuwa Kwa asilimia 100 na inakaribia kuwa juu kupita nchi zote za Afrika na dunia!
Bajeti ya kununua V8 Mpya 86 Kwa wizara Fulani.

Nyingine zimefichwa Kule Kisutu Nyuma ya soko na pleti namba zimengolewa!.
Tanza Giza.
 
Tanzania wanafikiri bado wapo kwenye ujima ,Kwa Sasa huwezi kufungia chochote duniani wanapoteza muda tu
 
Back
Top Bottom