Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,850
- 12,086
Fuatilia yanayojiri Bungeni kwenye Bunge cha 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 8 leo Aprili 17, 2023.
SERIKALI YACHUKUA HATUA KUFUNGIA TOVUTI NA MITANDAO YA KIJAMII
Akizungumzia hatua zilizochukuliwa kupambana na wanaotangaza mapenzi ya jinsia moja, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema tovuti 334, akaunti za Facebook 361, Instagram 198, Twitter 12 vikoa zaidi ya 2,456 vimefungiwa
Awali, Anatropia Lwehikila Theonest aliuliza swali Bungeni kuwa Sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu mapenzi ya jinsia moja? Ambapo Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Pauline Philipo Gekul amesema “Kifungu cha 9 cha Sheria ya Ndoa kinatafsiri Ndoa ni mahusiano ya hiyari kati ya Mwanaume na Mwanamke
Ameongeza “Pia Kifungu cha 154 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 kinabainisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile ni kosa la jinai na adhabu yake ni kufungo cha maisha jela au kisichopungua miaka 30 jela.”
MIUNDOMBINU YA DAR HALI NI MBAYA, MVUA ZIKINYESHA KAZI HAZIFANYIKI
Mbunge wa Segerea, Bonnah Ladislaus Kamoli amesema “Mvua ikinyesha Kisarawe maji yanakuja Ilala, hasa katika majimbo ya Segerea, Ukonga na Ilala kutokana na miundombinu mibovu.”
“Mfano juzi Wananchi wa Kata ya Vingunguti na Mnyamani wameshindwa kutoka ndani hadi tulipoomba msaada wa kampuni inayotengeneza barababa kusaidia kuondoa maji.”