Topic za mahusiano na mapenzi zapamba moto hapa JF

Ulitaka tujadili nini sasa??? Hujui mapenzi ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku bila hiyo kitu mmmhhh hapana
 
wana JF,
nimejaribu kupitia kwa juu juu nikaona kuwa topic zinazohusu ma 'love dove' ndio zenye chart na huchangiwa sana hapa jf kwa sasa (mods nisaidieni takwimu).najiuliza kunani GREAT THINKERS?wamelishwa nini ?mbona mawazo yote ''downstairs''
Nawasilisha.............[this is just the hypothesis]

jackbauer kwanza umenikumbusha movie ya 24 baada ya hapo ndo maana ma mods waliweka majukwaa kibao.
wengine siasa hatuziwezi ndo maana tuko huku ..tukija kule tutasema uongo bure
 
tatizo na shida zote zinazotukabili bado tunakomalia chini tuuuu!!
 
Kila kitu na zama zake. Wakati wa Uchaguzi hazikuwepo.

Binadamu ana priority za:

Power & Authority; Mapenzi na Pesa. Hivyo ndo vikuu. Power na Authority limepita (Uchaguzi), sasa na Pesa na Mapenzi kwa wengi.
 
wana JF,
nimejaribu kupitia kwa juu juu nikaona kuwa topic zinazohusu ma 'love dove' ndio zenye chart na huchangiwa sana hapa jf kwa sasa (mods nisaidieni takwimu).najiuliza kunani GREAT THINKERS?wamelishwa nini ?mbona mawazo yote ''downstairs''
Nawasilisha.............[this is just the hypothesis]

Si Ukifukuzwa juu unakimbilia chini? Juu tumefukuzwa baada ya CCM kuiba kura za Dr. Slaa na CHADEMA. Wengine tumeamua kuachana na siasa baada ya huo mchakachuo. Halafu mimi najuta kupoteza muda wangu mwingi katika masuala ya siasa na uchaguzi wa 2010. Chini ndo kuna mambo; yaani warembo wote nimewakuta huku chini....

Mind you, all great thinkers come from 'downstairs'. We are still great thinkers.
 
tatizo na shida zote zinazotukabili bado tunakomalia chini tuuuu!!

shida zako zipeleke kwa watakaokusaidia ila kama ni za kimapenzi zilete hapa ndio mahala pake, hutaki chapa mwendo usilete siasa huku
 
Watu wajadili nini tena bana wakati tumeshaibiwa kura zetu, ndio msimu wake haswaaa!!!
 
tatizo na shida zote zinazotukabili bado tunakomalia chini tuuuu!!
Mods walitenganisha majukwa we unawaona wajinga? we ni sawa sawa na yule aliomba acess mwenyewe kwenda jukwaa la wakubwa then akaanza kulalamika.....kazi kwelikweli
 
Mods walitenganisha majukwa we unawaona wajinga? we ni sawa sawa na yule aliomba acess mwenyewe kwenda jukwaa la wakubwa then akaanza kulalamika.....kazi kwelikweli

Hapana Kimey...huyu ameathirika huko juu...tumpokee tu na atayaona maisha kwenye mwanga mpya

Hebu tumuulize kwanza kama ni he/she ili tujue pakuanzia
 
mtoa mada bila mapenzi ungezaliwa? kwani wewe hauna demu au bwana?
 
wana JF,
nimejaribu kupitia kwa juu juu nikaona kuwa topic zinazohusu ma 'love dove' ndio zenye chart na huchangiwa sana hapa jf kwa sasa (mods nisaidieni takwimu).najiuliza kunani GREAT THINKERS?wamelishwa nini ?mbona mawazo yote ''downstairs''
Nawasilisha.............[this is just the hypothesis]

Kumbuka hata wewe ulipatikana kwa njia hii hii sahihi
 
Ni dhahiri Kuwa wabongo wanapenda starehe kuliko kazi na mara nyingi utaona kinachozunguziwa siyo mapenzi kama baadhi ya wachangiaji walivyodai ni masuala ya ukahaba uliopindukia na mada za maana za kuweza kuleta maendeleo hakuna wa kuchangia maana zinahitaji utulivu na uchambuzi wa kina na sio kujiropokea hovyo
 
Ulitaka tujadili nini sasa??? Hujui mapenzi ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku bila hiyo kitu mmmhhh hapana

hivi siasa,michezo nadini sio sehemu ya maisha.natamani kuelewa kwa nini mapenzi sana ?i think yote yanayojadiliwa hapa ni sehemu ya maisha.
 
wana JF,
nimejaribu kupitia kwa juu juu nikaona kuwa topic zinazohusu ma 'love dove' ndio zenye chart na huchangiwa sana hapa jf kwa sasa (mods nisaidieni takwimu).najiuliza kunani GREAT THINKERS?wamelishwa nini ?mbona mawazo yote ''downstairs''
Nawasilisha.............[this is just the hypothesis]

I think you have the wrong perception of this section and it seems you are not a regular here,watu wengi wamepata msaada wa mawazo kutatua matatizo yao ya mahusiano,kuna kundi kubwa tu hapa huwa tunaanzia kwenye picha,mahusiano,utani na kumalizia jukwaa la wakubwa na tunaonekana majukwaa mengine kwa nadra sana.
 
Wana/tunaondoa au kupunguza stress za uchaguzi!!! na hata hivyo zile za msingi zina wachangiaji wachache sana, maana hata uelewa ni mdogo kwa walio...wachache!!! sio ndio maana hata ile petition imejazwa na wana JF wachache sana!!! HUKO hawana ujuzi nako sana, ila sasa hapa ambapo hapahitaji darasa, mmmmh hata kilaza atachangia tu, tuna dare ku-speak openly
 
Mi nafikiri kinachotokea hadi Wana JF kujikita kwenye Mapenzi zaidi kwa kuwa mambo mengine kama Sijui Pinda amekataa shangingi ukichangia watu wanakuuliza umeipata wapi hbr hiyo lakini haya ya mapenzi mada zake ni kila mtu mataalamu hivyo ndio maana watu hujitanua wawezavyo kwa maana akiambiwa source ni ipi anajibu ni yeye mwenyewe! Hivyo kwenye mapenzi hakuna haja ya kutumia nguvu sana.
 
Wabongo si wanapenda Starehe ila tunaenda na matukio subiri kipindi cha Bunge hapa tutaamia katika Bunge ikija katiba mpya tutajikita kwenye katiba lakini kwa sasa tunajikita kwenye mapenzi mwishoni tunaamia X mass! hayo ndio maisha ya mwanadamu hutawaliwa na matukio na wakati pia!
Ni dhahiri Kuwa wabongo wanapenda starehe kuliko kazi na mara nyingi utaona kinachozunguziwa siyo mapenzi kama baadhi ya wachangiaji walivyodai ni masuala ya ukahaba uliopindukia na mada za maana za kuweza kuleta maendeleo hakuna wa kuchangia maana zinahitaji utulivu na uchambuzi wa kina na sio kujiropokea hovyo
 
Wabongo si wanapenda Starehe ila tunaenda na matukio subiri kipindi cha Bunge hapa tutaamia katika Bunge ikija katiba mpya tutajikita kwenye katiba lakini kwa sasa tunajikita kwenye mapenzi mwishoni tunaamia X mass! hayo ndio maisha ya mwanadamu hutawaliwa na matukio na wakati pia!

hivi starehe ni mapenzi tu?starehe ni kula Tigo?kama tunaendeshwa na matukio,unataka kuniambia topic za challenge cup zilitesa sana siku za karibuni.
Tukubali ukweli kuwa jamvi limeanza kuwa Ze URODA.Great thinkers are thinking like Uwazi,Kasheshe and Kibonde.
 
Hivi mbona hili jukwaa linatupiwa mawe sana? sio siku hzi tu tangu najiunga mm naona kila siku malalamiko tuuu watu wan discuss mapenzi mapenzi....Teamo, Aspirin, Fidel, Rev Masa Mwanajamii etc wote watakuwa mashahidi kwenye hili......:embarrassed:
 
Back
Top Bottom