rkgx
Senior Member
- Nov 30, 2013
- 100
- 80
Kuna kitu huwa sikielewi kabisa kwanini kuna tofauti kubwa ya mishahara ya wafanyakazi wa serikali kuu na wa kwenye mashirika ya umma wakati kazi ni zile zile na maisha ni yale yale? najua wanapoandaa range za mishahara huwa kuna factor nyingi wanazingatia ikiwemo cost of living etc, sasa sijaelewa kwanini wafanyakazi wanaoishi kwenye mazingira sawa, na kwa muajiri mmoja serikali wawe na tofauti kubwa hivyo ya mishahara?? Ninachomaanisha hapa ni kwamba kwanini graduate anayeanza kazi halmashauri alipwe 567,000 while anayeanza kazi kwenye academic institution au mifuko ya jamii aanze na 867,000( not very much sure with that scale)??. Sipati majibu kwanini serikali haioni muda umefika sasa wa hawa watu kuwa na mishahara inayofanana.