Timu ya Taifa ya Pooltable yaifunga Kenya 13 – 9, mashindano Afrika Nchini Zambia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,842
12,046
TIMU ya Taifa ya Pooltable Waanaume imeanza vyema mashindano Afrika kwakuwafunga majirani Kenya 13-9 katika mchezo wake wa kwanza wa mashindano hayo yaliyoanza leo Nchini Zambia.

Mashindano hayo yameanza kwa makundi A na B ambapo kundi A ni Tanzania, Kenya Uganda na Zimbabwe wakati kundi B ni Afrika Kusini, Swaziland na wenyeji Zambia.

Jumla ya Nchi saba zikiwakiliswa na timu ya Wanaume na Wanawake zinashiriki mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka.

Meneja wa Timu ya Taifa , Omary Soup ametamba kufanya vizuri katika mashindano hayo kutokana vikosi vya timu ya Wanaume na Wanawake alivyosafiri navyo kuwa imara.

Omary alitaja wachezaji wanaowakilisha nchi kupitia mchezo wa Pool Wanaume ni Abdallah Hussein, Mussa Mkweja, Baraka Jackson, Baraka Joachim, Festo Yohana, Melkzedeck Amedeus, Jackson Steven, Isaya Paul, Amos Boniphace, Innocent Sammy na Kapteni Charles Venance wakati timu ya Wanawake ni Neema Hamis, GraceShitindi, Rebecca Magaigwa na Jackline Titto

Mashindano yameanza leo yanatarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki huko Lusaka Zambia.
IMG_20220304_174118_542.jpg

Timu ya Taifa ya Pooltable ya Wanaume na Wanawaake wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mashindano ya Afrika yaliyoanza leo Lusaka Zambia kwa kushirikisha Nchi saba ambazo ni Tanzania, Uganda, Kenya, Afrika Kusini, Zimbabwe, Swaziland na wenyeji Zambia.
 
Hivi huwa kuna ligi ya ndani ya nchi inayohusisha mikoa yote?, au wanachaguliwa wale wadarasalama tu kuwakilisha Taifa huku mafundi wengine tukisahaulika mafichoni huku Nanjilinji?. Anyway kila la heri wawakilishi wetu
 
Back
Top Bottom