stardust JK
JF-Expert Member
- Jan 7, 2018
- 2,975
- 4,207
Mkuu hii namba 6 kama sijakupata hiviKwa mujibu wa relativity, kwa huyo Kulwa, kila kitu kitakuwa cha kawaida, yani ataona muda unaenda kama kawaida.
Ukichukua mfano extreme wa ku freeze muda ni vigumu kueleweka na hauwezekani kufikiwa kwa vitu vyenye mass (akizidi kukaribia speed of light, ndivyo uzito wake unavyozidi kukaribia infinity). Mfano mzuri zaidi ni wa Kulwa ku age kwa maiaka kama 10 wakati Doto ana age kwa miaka 60.
Mfano huu unapigia mstari ukweli kwamba:-
1.Muda ni relative (Relativity Theory ya Albert Einstein)
2. Speed inapunguza kupita kwa muda kwa aliye katika chombo kinachokimbia kwa mujibu wa macho ya mtu aliyesimama ambaye hakimbii.
3.Kwa mtu aliye katika chombo kinachokimbia, muda utakuwa unaonekana kupita kama kawaida
4. Kinadharia, ukiweza kufikia speed of light unausimamisha muda
5. Kiukweli huwezi kufikia speed of light, unavyozidi kuikaribia uzito wako unazidi kukaribia infinity
6. Speed inaongeza uzito
Speed inaongeza uzito au inapunguza uzito? jinsi unavyoikaribia speed of light uzito nao si unapungua?