Time For Change: Sema "hapana" ngwe ya pili ya JK

Nyani, umenena.
Do we real have an alternative ama they are just like JK????????
To many promises before they get to power and once they are on top wanasahau wajibu wao!
Sijui kama Tanzania tuna viongozi waadilifu hata wakati huu tunaolilia ufisadi na mengine mengi!


Kama ni kweli TZ haina viongozi bora kuliko JK then tusahau kuhusu maendeleo. Lakini kwa mtizamo wangu, pamoja na ufisadi ulioendelea awamu ya tatu bado BWM ni bora kuliko huyu jamaa yetu. Yaani ni kama kulinganisha maji na mafuta. In fact kuna jamaa kibao wanauwezo zaidi yake tatizo sisi tunaangalia sifa badala ya uwezo.

Hata mama Asha Rose nafikiri ni Prez material and could do much better that what we have now!!!
 
Niseme nini kisichojulikana? Alishinda kwa asilimia nyingi ya kura akijaza mioyo ya watanzania matumaini ya mwanzo mpya wa ujenzi wa taifa lao. Watu walitaraji mabadiliko. Walichopata badala yake ni mwendelezo wa sera ya uzembe, itikadi ya ufisadi na siasa za kubebana na ahadi za kuzugana. nchi yetu inastahili uongozi bora. Hatuitaji miaka mingine 5 ya viongozi walioshindwa. No 2nd term 4 kikwete. Yes i said it.
Wacha kuota mchana, huna job nini?
 
Hata kama sina idea kwa sasa nani anaweza kuongoza nchi hii vema baada ya 2010, nakubaliana na Mwanakijiji kwamba huyu wa sasa (JK) hastahili miaka mingine mitano. Amini amini nawaambia iwapo tutathubutu kumchagua tena 2010 nchi itarudi nyuma kwa miaka mingine mitano. Hivi ni sifa gani kubwa ya uongozi mnaiona kwa mtu huyu? Mie namfahamu vizuri na nilionya watu kuhusu kumchagua tangu 2005 - kwamba hafai. Ni mswahili tu aliyetaka urais kwa sifa. Rais gani anashindwa kukemea ufisadi wa waziwazi unaoliangamiza taifa huku yeye akicheka cheka tu... Naamini tuna watu wengi wenye sifa na ambao wana dhamira ya kweli ya kukemea ufisadi, wenye uchungu na nchi yao na wenye mtazamo wa maendeleo ya kweli. Tuna resources zote muhimu za kuifanya nchi iwe tajiri lakini tuna viongozi dhaifu kupindukia na ndio maana kwa wananchi wengi "KILA KUKICHA AFADHALI YA JANA".
 
MzeePunch,
Mkuu ni haki yako kusema unayoyasema lakini unasahau kwamba viongozi wote waliotangulia wamechukua ngwe ya pili tena kwa sababu mbaya, na chafu zaidi JK. tunaposema tusimchague Jk kwa kutokemea Ufisadi, tukumbuke tu kwamba Mwnyi na Mkapa wao walikuwa MAFISADI na tukawapa ngwe ya pili..Na ajabu tulidai maendeleo makubwa yaliyotolewa na takwimu za kitaifa wakati Tanzania kwa mara ya kwanza kabisa watu walikufa njaa kwa maelfu, tukaendelea kushuka daraja (rank) ya nchi maskini duniani. Nchi kama Rwanda na Ethiopia zikapanda juu yetu, lakini bado tukajigamba kuwa nchi inapendeza.

Leo mnaponambia tusimchague JK kwa mtazamo usiokuwa na ushindani ndani ya mfumo ambao umepangwa nashindwa kuelewa tutaweza vipi kutomchagua JK..
Simamisheni mtu wenu, mtu ambaye kwa maelezo haya haya sisi wananchi tunaweza kuona sababu ya kutomchagua JK laa sivyo JK anasimama na kivuli!.. Bora huyo JK kuliko kuchagua kivuli....
 
Tatizo kubwa sana ni mfumo na pia hata mtu akiwa ana nia safi kiasi gani mfumo umefidasadiwa tayari
 
Mitanzania mingine mivivu sana kufikiri. Kitu gani kinawafanya mfikirie urefu wa kamba kama mbuzi? Tanzania ina watu milioni 40. Kati ya hao wenye umri zaidi ya miaka 40 (kama ni 40%) na miongoni mwao 0.01% tu wakawa na sifa za kutawala, basi hatukosi Watanzania 1600.

Watanzania wengi wamo, mfano Rashidi Mohamedi, Slaa, Salimu A SAlim, [Mkandara, Pundit na Kuhani (wa JF), hawa 2 sijui wametokomea wapi]. Jamani msitutie aibu kuona kuwa hakuna zaidi ya JK kwa sasa Tanzania!
 
Tatizo kubwa sana ni mfumo na pia hata mtu akiwa ana nia safi kiasi gani mfumo umefidasadiwa tayari

Kweli kabisa tatizo ni mfumo na baadhi ya individuals. Lakini swala lingine ni kwa nini JK tuliyetegemea, na aliahidi mfano kubadilisha mikataba ya madini, mbona ameshindwa???
 
Mitanzania mingine mivivu sana kufikiri. Kitu gani kinawafanya mfikirie urefu wa kamba kama mbuzi? Tanzania ina watu milioni 40. Kati ya hao wenye umri zaidi ya miaka 40 (kama ni 40%) na miongoni mwao 0.01% tu wakawa na sifa za kutawala, basi hatukosi Watanzania 1600.

Watanzania wengi wamo, mfano Rashidi Mohamedi, Slaa, Salimu A SAlim, [Mkandara, Pundit na Kuhani (wa JF), hawa 2 sijui wametokomea wapi]. Jamani msitutie aibu kuona kuwa hakuna zaidi ya JK kwa sasa Tanzania!

Ndugu yangu wadanganyika tulisha rogwa hatuoni tena.
 
  • Mwinyi hakuwa na sifa nyingine zaidi ya upole, tukampa awamu ya pili akauza hadi tausi wa Ikulu.
  • Mkapa hakuwa na sifa yoyote zaidi ya ukimya, tukampa awamu ya pili akajiuzia hadi mradi wa Kiwira.
  • Kikwete ameingia bila sifa yoyote zaidi ya urembo, tunataka kumpa awamu ya pili - lini tutajifunza.
Angalau Mwinyi na Mkapa walikuwa na cha kuonyesha kwenye awamu zao za kwanza, je huyu ambaye ametoka kapa ? Huyu ametumia awamu ya kwanza kuranda randa kuuza sura, awamu ya pili si ndiyo hatutamwona kabisa ?
 
Nani kama JK atakuwa pembeni? Mfumo uliopo ni kama utaleta mtu mwenye mitazamo ya aina ileile ya watu waliopo. Ingawaje baada ya sesion ya leo na Tido Mhando, nategemea atakuwa ameng'amua mambo si vile wanavyomsimulia wapambe wake
 
Who's the alternative? Or it's just Anybody But Kikwete (ABT)....

Kwa sababu mpaka sasa sijaona kiongozi yeyote aliyeonesha uongozi madhubuti na uliotukuka hususan ikija kwenye masuala ya ufisadi na muunganiko wake kwenye utawala mbovu vis-a-vis utawala bora.

Oh well....[/QUOTE]

- Mkulu Nyani, ahsante sana kwa kuniwahi maana huu wako ndio ukweli wenyewe, ni kwamba nani wa kushika hiyo nafasi ambaye ni bora kuliko JK, mbona hatujamsikia au kuwa kimya ni moja ya skills better than JK?

- Binafsi baada ya yote yaliyojiri politically in the last five weeks, sina nguvu sana na wala imani katika uwezo wetu wa-Tanzania kufanya tofauti na walioko kwenye power sasa hivi, labda atajwe japo mmoja tumchambue!

- Nilikuwa nina imani sana na Zitto na Chadema kwa ujumla kwa mbele ya safari, lakini wamenikatisha tamaa kabisaa, labda watoto wetu lakini kwenye hii generation, labda itokee miracle!

Respect.

FMEs!
 
Wakuu,
Hakuna mtu alosema kwamba hatuna watu wenye uwezo wa kuongozi zaidi ya JK,,, Hakuna!
Ila tunachosema hakuna mtu alosimama against JK hivyo JK anapimwa na kivuli.. sidhani kama mtu yeyote mwenye akili timamu atachagua kivuli.
Ndio wapo kina Salim, Mwandosya, Dr.Slaa, Magufuli na wengine wengi tu ambao tunaweza kuwaweka mbele ya JK lakini maadam hawapo ktk kugombea urais tunabakia na JK..
Nipeni jina la mgombea kisha nambie nisimpe kura yangu JK hapo nitaweza kupima maelezo yote haya lakini haya maswala ya kufikiria kutompa kura JK hata kama akisimama na Rostam au kivuli sii akili hata kidogo. Chadema na vyama vya Upinzani wakati ndio huu jitokezeni na mgombea/Wagombea wenu tupate kuwapima mapema kabla ya uchaguzi wa ndani ya vyama vyenu.. Au mnaogopa Kukolumbiwa! Mnaogopa yaliyowakuta Kahama na Mwaikambo!
 
Wakuu,

Ndio wapo kina Salim, Mwandosya, Dr.Slaa, Magufuli na wengine wengi tu ambao tunaweza kuwaweka mbele ya JK lakini maadam hawapo ktk kugombea urais tunabakia na JK..
QUOTE]

- Kuacha Dr. Slaa hao wengine wamefanya nini hasa cha maana?

- Halafu na yeye Dr. Slaa baada ya yote yaliyojiri huko Chadema hivi majuzi, anapata wapi tena ile moral authority aliyokuwa nayo siku zote huko nyuma? Iwapo anashiriki kwenye demokrasia makini inayotumia busara za wazee wa chama ambao hawamo kwenye katiba ya chama kumuengua kiongozi mwenziwe, tena msaidizi wake katika kugombea uongozi wa juu wa chama hicho, sasa akipewa Jamhuri itakuwaje?

- Ina maana hata hawa mafisadi anaowalalia macho kuwafichua atawapeleka huko huko kwenye baraza la wazee wa chama, badala ya kufuata katiba ya jamhuri, ndiyooo! si ukweli tumeuona kwa macho yetu na tumeusikia kwa masikio yetu tena na wahusika wote wa hiyo cinema hapa JF, au?

Inasikitisha sana, hili taifa tumelaaniwa tu tutaendelea kudanganyana na kuzunguka hapa hapa tulipo!

Respect.

FMEs!
 
Field Marshall Es,
Hapana mkuu wangu, huwezi kumlaumu Dr.Slaa kwa yaliyotokea Chadema hata kama alikuwa upande wa wazee au kuwaunga wazee kwa sababu Zitto kama msaidizi wake ingebidi amjulishe au hata awe na wajuimbe wa kutosha kugombea nafasi hiyo na sii kufanya mchezo wa sinema kumwona co starring anayekufa ktk tambara tu...

Zitto hakuwa na umri unaoruhusiwa kugombea Urais, hakuwa na caucus nyuma yake isipokuwa washabiki, sasa nini lengo lake kugombea nafasi ambayo anajua wazi haimtahili?..Kisha mkuu wangu ni jambo la kawaida kabisa kwa wazee wa chama kuongea na mgombea alochukua form kutoleta ushindani ambao hauwezi kukisaidia chama. Iwe ubunge au Urais. Na demokrasia ya kweli haiwezi kumtenga Dr. Slaa mapendekezo yake ktk nafasi hiyo. Kama alikuwa akimpendekeza Mbowe basi lilikuwa jukumu lake kusimama nyuma ya Mbowe hata iwe ni uchaguzi wa ndani. Wewe mwenyewe uliona jinsi maseneta walivyojipanga nyuma ya Obama wakamwacha Mama Clinton na wakasema mengi kuhusiana na mama Clinton.

Mwenye makosa hapa ni Zitto mwenyewe alotaka kugombea kisha akaliondoa jina lake yeye mwenyewe wakati tunawaona vigogo wa siasa kama mzee Malecela alilia haki yake hadi dakika ya mwisho pamoja na kwamba wazee wa CCM walimmfuata na kumwomba achomoe jina lake toka ktk wagombea...Hakufanya hivyo hadi wazee wenyewe walipolazimika kuchukua hatua kinyume cha katiba..

Hata hivyo issue hapa sii upinzani kati ya Zitto na Dr.Slaa..isipokuwa ni mila na desturi za chama katika kuugombea nafasi za juu za chama badala ya kutumia njia za kina Don Coleone..hiyo ni party assassin ambayo mheshimiwa Dr. Slaa asingeweza kushiriki! Pili siudhani kama unafahamu kwamba kulikuwepo na makundi tayari ndani ya Chadema!.. toka Zitto achukue ile nafasi ya kamati ya madini kinyume cha mapendekezo ya kamati ya chama chake.. Zitto aligeuka kuwa mshindani ndani ya chama na naweza kusema alionekana kuwa na ambition!..Hiyo ambtion ndiyo ilikuwa tishio kwa chama kizima..
 
Field Marshall Es,
Hapana mkuu wangu, huwezi kumlaumu Dr.Slaa kwa yaliyotokea Chadema hata kama alikuwa upande wa wazee au kuwaunga wazee kwa sababu Zitto kama msaidizi wake ingebidi amjulishe au hata awe na wajuimbe wa kutosha kugombea nafasi hiyo na sii kufanya mchezo wa sinema kumwona co starring anayekufa ktk tambara tu...

..

- Bob ninasema hivi, ya Zitto sio ishu hapa the ishu ni politics of it, ni kwamba DR. Slaa ameshiriki kwenye vitendo vya kutoheshimu katiba ya chama chake mwenyewe, sasa eti unasema akipewa Jamhuri ataheshimu katiba ya Jamhuri? Are you serious?

- Bob ni mara ngapi hapa nimesema hivi haya maviongozi yote mafisadi, ukiyapekua pekua utakuta yalianza ufisadi toka siku nyingi sana, haiwezekani kwamba yalianza ufisadi baada ya Mwalimu kutoka uongozi au kutangulia mbele ya haki,

- Sasa eti unasema kwamba Dr. Slaaa akiwakamata mafisadi atawapeleka kwenye sheria na sio kwa hao wazee wa chama chake cha siasa wasioheshimu katiba ya chama chao wenyewe?

Pleaseee!

Respect.

Field Marshall Es!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom