Franky Samuel
JF-Expert Member
- Oct 10, 2018
- 4,910
- 12,988
Mimi situmii sana tiktok, lakini naomba niseme ni moja kati ya mtandao unaokuja kwa kasi hivyo kuwa mshindani namba 1 wa youtube.
Kwa sasa hawajaifikia youtube, lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba ni threat namba 1 wa youtube, ndiyo maana Marekani wanaipiga vita ili kumuokoa youtube ambayo ni ya Mmarekani.
Marekani ndivyo alivyo, kumbuka hata Huawei alifanyiwa figisu baada ya kuonekana ni threat kwa Iphone/Apple. Ni mbinu za kijasusi za Mmarekani ili kuokoa makampuni yao yanayopata ushindani mkali kutoka kwa Wachina.
Hivyo wote mnaoibeza tiktok kaeni mkijua ni kweli inaleta threat kwa usitawi wa youtube.