Tiketi ya treni hadi uwe na kitambulisho

HASSAN SHEN

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
428
69
Mh.Mwakembe aeleze hivi ni kwa nini ukitaka tiketi ya treni kutoka kigoma kuja dar na vice versa,unaombwa uoneshe kadi ya kupigia kura,kwani kigoma sio Tanzania?
 
Kuzuia wahamiaji haramu kutoka nchi za jirani hasa Kigoma wahamiaji haramu wapo wengi mno. Kwangu mimi sioni kuwa ni tatizo hilo. Hata Serikali akiamua kuwaambia polisi watuulize vitambulisho mitaani naona poa tu kwa usalama wetu na nchi yetu dhidi ya Wahamiaji haramu.
 
Hata Marekani kupanda ndegee siku hizi lazima uonyeshe kitambulisho.
 
Kwa hilo naunga mkono 100%, tena ikiwezekana tutembee navyo kabisa na mtu asiruhusiwe kupanda treni bila kitambulisho maana kuna wengine wanadandia tu bila tiketi.
 
Mkuu nchi nyingi za ughaibuni na baadhia ya Africa kama Africa Kusini huwezi pata kazi kama huna kitambulisho au kusoma shule au chuo. Kitambulisho ni muhimu sana
 
Mbona kutokea Unguja, Pemba, au Kenya vitambulisho havihitajiki? Ni upande gani ni hatari zaidi kwa usalama wa nchi? Kigoma au Pemba/Kenya? Tumesahau maharamia ya kisomali yamezagaa huko baharini na kupitia mpaka wa Kenya na upande bahari?

In short, kama usalama wa nchi uko mashakani kutokana na uhamiaji haramu basi wahamiaji hao ni kutoka Somalia, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, na Sudan ya Kusini. Kigoma ni cha mtoto, after-all upande wa west ni wabantu wenzetu. Ukisikia kuchuja mbu ukameza ngamia ndio kitu kama hiki.
 
Kwa hilo naunga mkono 100%, tena ikiwezekana tutembee navyo kabisa na mtu asiruhusiwe kupanda treni bila kitambulisho maana kuna wengine wanadandia tu bila tiketi.

Mkuu ni sahihi lakini isiwe upande au sehemu moja tu bali iwe utaratibu wa nchi nzima.
 
Kuzuia wahamiaji haramu kutoka nchi za jirani hasa Kigoma wahamiaji haramu wapo wengi mno. Kwangu mimi sioni kuwa ni tatizo hilo. Hata Serikali akiamua kuwaambia polisi watuulize vitambulisho mitaani naona poa tu kwa usalama wetu na nchi yetu dhidi ya Wahamiaji haramu.

Wahamiaji kigoma tu? Vipi kuhusu mikoa mingine ya mipakani kama mtwara,mbeya,arusha,tanga nk?
 
Mbona kutokea Unguja, Pemba, au Kenya vitambulisho havihitajiki? Ni upande gani ni hatari zaidi kwa usalama wa nchi? Kigoma au Pemba/Kenya? Tumesahau maharamia ya kisomali yamezagaa huko baharini na kupitia mpaka wa Kenya na upande bahari?

In short, kama usalama wa nchi uko mashakani kutokana na uhamiaji haramu basi wahamiaji hao ni kutoka Somalia, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, na Sudan ya Kusini. Kigoma ni cha mtoto, after-all upande wa west ni wabantu wenzetu. Ukisikia kuchuja mbu ukameza ngamia ndio kitu kama hiki.

Kweli dudus mi naona kama ni sort flani ya ubaguzi.
 
ninaunga mkono hoja ni kwa usalama wetu na taifa kwa ujumla na sio tanzania tu china kupanda tren lazima passiport au kitambulisho kwa wachina, italy popote unapoenda lazima uwe na passiport au permit kwa sababu muda wowote na mahali popote askari anaweza kukusimasha na akahitaji kuviona hivyo vitu
 
Mh.Mwakembe aeleze hivi ni kwa nini ukitaka tiketi ya treni kutoka kigoma kuja dar na vice versa,unaombwa uoneshe kadi ya kupigia kura,kwani kigoma sio Tanzania?

Acha Mawazo kama ya ndugu zetu wa Zanzibar wao wanasema sio WABANTU
 
Wa mjini vp? Hivi hawa wahamiaji haram tunaosikia kila siku kwenye vyombo vya habari mara wamekamatwa mara wamekufa wanapitia kigoma?

Kigoma ndipo wanapoadandia treni kuja Dar, Umeshawahi kusikia Treni imetokea Arusha mpaka Dar? njia ya Tanga wahamiaji haramu hawaitumia sana kuliko ya Kigoma kwa sababu ya Treni. Njia ya Arusha inawahamiaji haramu wengi ila kuwadhibiti huko ni rahisi
 
Mh.Mwakembe aeleze hivi ni kwa nini ukitaka tiketi ya treni kutoka kigoma kuja dar na vice versa,unaombwa uoneshe kadi ya kupigia kura,kwani kigoma sio Tanzania?

kigoma ni saturation point ya majambazi ya kirundi, kikongo na mengineo lazima tuwe extra vigilent
 
Mh.Mwakembe aeleze hivi ni kwa nini ukitaka tiketi ya treni kutoka kigoma kuja dar na vice versa,unaombwa uoneshe kadi ya kupigia kura,kwani kigoma sio Tanzania?

Mmegombea Hayo Maendeleo...Mmeondoa NGUZO za VIONGOZI halafu Mmefunga VITUO VYA WAKIMBIZI na KUGAWA

ARDHI YAO KWA VIONGOZI wa SERIKALI na MARAFIKI; WAKATI wa Mwl. Nyerere Hao Wakimbizi Wasingelazimishwa

Kurudi kwao na Wangesikilizwa na kupewa URAIA na hiyo ARDHI wangegawiwa; Lakini sasa la hasha haraka haraka

Sasa wanajua watakimbilia MIKOA mingine... Wanaweka SHERIA TICKETI ya TRENI lazima kitambulisho...

NI ULAFI WA HIYO ARDHI...
 
Back
Top Bottom