Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,152
Siku ya jana, tarehe 26/2/2024, shirika la reli hapa Tanzania (TRC) lilifanya jaribio la kwanza la treni ya kisasa, umeme na mwendokasi (SGR), na miongoni ya malengo (matarajio ya watu?) ya msingi yalikuwa ni haya;
1. Mwendokasi (muda wa kusafiri uwe mchache huku umbali uwe mrefu).
2. Nishati ya Umeme (uhakika wa umeme wakati wote)
Bila kumumunya maneno, malengo yote mawili hayakufikiwa. Treni haikuwa na kasi ya kutosha, safari ikatumia muda mrefu zaidi kutoka Dar mpaka Moro. Lakini mara mbili umeme ulikatika katikati ya safari, treni ikapunguza mwendo na huduma ya umeme ndani ya mabehewa ikapotea.
Kwa wale wasiofahamu kuhusu Sayansi ya majaribu (practical trial/ testing ama Pilot survey) ni kuwa, ili malengo yanayotegemewa kuwepo katika uhalisia yaweze kuonekana kwelikweli inabidi majaribu yafikie malengo na kupitiliza walau robo zaidi ya lengo (yaani yafikie 125%). Kwa mfano kama Treni ya SGR inategemewa kutoka Dar-Moro kwa dakika 75 tu basi wakati wa majaribio walau itumie dakika zisizozidi dakika 57.
USHAURI.
TRC inabidi ifanye mambo haya matatu kwa sasa;
1. Itoe taarifa kamili ya kitaalamu kuonyesha taswira nzima ya hilo jaribio, wapi walifikia lengo na wapi walishindwa kufikia lengo.
2. Wakae chini kujipanga upya namna ya kuweza kukabiliana na mapungufu hayo.
3. Waje kufanya jaribio lingine baada ya kupata utatuzi wa mapungufu yote.