TIGO PESA na LAKEBROKERS wameshirikiana kuniibia

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Naamini JF inasomeka sehemu nyingi, naamini pia kuwa kuna wasomaji watanifikishia hii kwa Tigo. Toka tarehe 18 Julai nimetoa pesa kwa wakala akasema eti nimekosea namba. Kila nikipiga simu naambiwa niwe mvumilivu eti wakala hapatikani kwa simu? ref no sio siri ni C0120718.1202.F04425. Baada ya kupiga simu nyingi sasa nimeanza kuwarekori mimi mwenyewe wahudumu wa tigo, jana alikuwa David na akanihakikishia kuwa ameripoti kama kronik issue nisubiri saa 24. Kumbe wahudumu wamewekwa kama masanamu tu na kujibu kama roboti.Hadi sasa sijapata pesa yangu. Leo nimemkuta Clement naye kasema nimpe ref no, nimekataa kwa sababu huu ni uhuni. Nimemwambia anipe David aliyeniahidi jana kuwa hela yangu itarudi, akaniambia leo david yuko off. Pengine hata majina wanabadilisha hawa watu. Nisaidieni wakuu, nitapataje hela yangu. Kuna mtu au namba nyingine zaidi ya hawa ma-robot?
 
Nimekomaa sasa kapokea Edith, huyu mpole kidogo na aliponiahidi kuwa suala linashughulikiwa kamekuja na kameseji kutoka +800. Ninachokataa ni kusubiri majaaliwa ya mwenyezi kujua kama nitarudishiwa pesa au la? wash.enzi kweli na vitigo vyao.....
 
km uko karibu na customer care office ni heri uende mwenyewe kuliko kupiga simu
 
Hawa tigo wanamatatizo sana chakufanya kama nipesa nyingi nenda tigo makao makuu kawaeleze
 
Back
Top Bottom