tiGO mtavunja ndoa za watu!

poleni sana wahanga wenzangu mliokuwa mmelizwa na tigo pesa kwa mfumo wa kununua muda wa hewani. Nilipatwa na mkasa huo takribani wiki moja iliyopita kwa kiasi cha zaidi ya tsh. 20,000/. Nililipoti tatizo hilo kwa ofisi za tigo pale mlimani city wale warembo wakanishauri niorodheshe jina langu, namba yangu na kiasi kilichokwamishwa na mtandao, sikusita nami nilikuta orodha ndefu sana nami pia nikatia jina langu. Nimekaa kwa muda sasa lakn leo tigo wamenitumia ujumbe wa kuniomba radhi na salio langu limeongezeka kwa kile kiwango ambacho kilikwamishwa na mtandao.

Poleni sana tigo kama kweli mtandao wenu umeingiliwa na hackers, lkn kama ni uzembe wenu no thanks on this foolish!

Naomba sana wadau ambao wamelizwa kwenda manualy ofisi za tigo kila kitu kipo poa.

hilo tatizo pia lilinitokea kama wiki moja iliyopita nikaripoti tigo makao makuu Moshi. Leo asubuhi wamenirudishia salio langu.
 
wanalipizia yale mameseji yao wanayotumaga
mpaka uko choo cha bar unaskia sms
unadhani ya maana ooh sijui ukitaka
midundo na blablablaa kibao
sasa ndo wanakata kufidia



i hate them
 
Back
Top Bottom