Tigo 'Marketing Team' mnatukosea wateja...

Igwachnya

Member
Jan 5, 2011
80
20
Hivi hawa jamaa wazima kweli? Huu ulikuwa wakati muafaka kupandisha gharama za simu na sms? Wapo busy ku-promote wimbo wa mbayuwayu hadi wanakera... hivi kumsikilizisha mtu kitu asichotaka sio kosa?

Inawezekana hawa jamaa wapo kwenye payroll ya kampuni nyingine kwa ahadi ya kuiua tigo....

RIP TIGO
 
labda wanafanya demarketing. Ukizidiwa na wateja si lazima uwabebe wote. Unatafuta namna ya kuwapunguza.
 
Choice guys! Kama unaona huwezi gharama zao basi waweza hamia vodacom, zantel na wengineo.
 
Choice guys! Kama unaona huwezi gharama zao basi waweza hamia vodacom, zantel na wengineo.

Wakati mwingine ukiwa mtu mzima kuhama hama mitandao au kubadili namba kila wakati hailipi.... Inawezekana tigo walikuwa na plan ya kukua na kushika soko wakasahau plan ya kubakia juu...... Wakati huu ni kama vita imepamba moto kila kampuni inashusha gharama za kupiga simu isipokuwa tigo..... kila kampuni inajitahidi ku customize servicess ili kuendana na makundi tofauti tofauti ya wateja wake isipokuwa tigo..... hili linaweza kuwa sikio lakufa
 
Back
Top Bottom