Tido Mhando atemwa TBC

hapo aliletwa na lowasa ndo swahiba wake,kazi haikutangazwa hiyo popote..nafikiri pia imemcost ile siku alipomuhoji lowasa kwa kumsafisha nakumponda pinda..lakini lowasa anaanzisha radio arusha soon abda atampa kazi huko
i will never do this if i love my country... politicizing professions!!!

Kazi itangazwe na yeye aombe... kwani alikujaje kutoka huko UK, was the process competitive??

What happened to him was not unexpected kabisa, kumbukeni wanasema ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga... how was he recruited in teh first place? what about his allies who came along with him?? Guys...

hebu acheni kuleta siasa hapa....

Kila kazi lazima ishindanishwe....
 
Biafsi sijafurahiswa na Matangazo ua TBC. Kwa wale wenye king'amuzi cha Star-Times jaribuni kuangalia Luninga Za Kenya Kama K.B.C, NTV na kadhalika. Anagalieani jinsi habari zao zilivyo za kisasa, wanahabari walivyo wachangamfu na jinsi wanavyoripoti habari. vibonzo vyao n.k.

kisha geukia T.B.C yetu. Mhhh!!!!!! Kichefuchefu. Wakati mwingine Mtangazaji anakaa dakika kadhaa akisubiri habari ije.
Haya si ya kujivunia hata kidogo.

Ni Sawa tu TIDO aende ili tupate Damu Mpya inayoweza kutufikisha Pazuri zaidi.

Natoa mchango.
 
Biafsi sijafurahiswa na Matangazo ya TBC. Kwa wale wenye king'amuzi cha Star-Times jaribuni kuangalia Luninga Za Kenya Kama K.B.C, NTV na kadhalika. Angalieani jinsi habari zao zilivyo za kisasa, wanahabari walivyo wachangamfu na jinsi wanavyoripoti habari. vibonzo vyao n.k.

kisha geukia T.B.C yetu. Mhhh!!!!!! Kichefuchefu. Wakati mwingine Mtangazaji anakaa dakika kadhaa akisubiri habari ije.
Haya si ya kujivunia hata kidogo.

Ni Sawa tu TIDO aende ili tupate Damu Mpya inayoweza kutufikisha Pazuri zaidi.

Natoa mchango.
 
Mkuu I beg to differ.... Kama TV ya taifa inabidi isiendeshwe kwa manufaa ya kibiashara na kuleta faida... hii ni service kwa taifa.... kwahiyo hata vipindi ambavyo havina profit lakini they are informative na educational inabidi iviweke pia.... Hebu niambie faida ya zile kamali kwa jamii...

Sawa mkuu mimi na wewe tunapishana kidogo sana!kwanza mimi nakiri kuwa huyu jamaa ana mapungufu yake,lakini kuna mambo mazuri aliyoyafanya.Sisemi kuwa TBC ijiendeshe kibiashara zaidi,lakini ina wajibu kwa kiasi furani kupunguza utegemezi wa ruzuku ya serikali ,hii ni kwa sababu ruzuku inayotolewa na serikali haitoshi kuendesha TBC,hivyo ubunifu ulikuwa muhimu sana.Kuna vipindi ambavyo kwa mtazamo wako unaweza ukaviona havina maana ,lakini kwa wengine vina maana!kwa mfano chelekocheleko,kuna baadhi ya watu wanakipenda sana kipindi hiki kwa sababu uburudisha pia ufundisha.Naomba suala la kamali nisiliongelee kwa kuwa kipindi hicho sijawahi kukiangalia na kujua namna kinavyofanyika!inawezekana katika hili na yeye alichemka!!
 
Mimi naona watakaoumia kwa dhati kabisa katika wapinzani ni CUF, maana CHADEMA tayari wanachombo chao cha ITV ambacho kiliapa kutotangaza kampeni za CUF na kujikita kidhati kabisa kui promote CHADEMA! sasa hii itakuwa imekula kwa CUF!!! ndio siasa hizi waache walale tu na siasa zao za Unguja na Pemba....

Source yako ni ipi? Ni lini ITV wameapa kutotangaza kampeni za CUF! Mbona wakuropoka sana wewe! Sidhani kama nyumbani hapa ni pako!
 
run tbc ofcourse.... Na uwezo wake angeweza kuifanya tbc iwe maradufu kuliko ilivyo sasa.... when you buy messi you dont expect him to perform like peter crouch or eric djemba djemba.... I think you get my point

but you should give due credit to tido alipoifikisha tbc
 
NImefurahi sana Tido kuondolewa hasa nikikumbuka jinsi alivyomdhalilisha waziri mkuu pinda kwa kumuweka kama pambano la utangulizi ili lowassa aongeee later

safi sana serikali

Naomba ajaye awe professional, neutral and asitoke dailynews wala habari leo na wala siwe na any association.... pia asiwe salva rweyemamu, muhingo rweyemamu au kibaraka mwingine kwani hao wamenifanya nidhani kwamba huna haja ya kusomea uandishi kabisa...
 
PDidy,
Kwa akili yako unafikri kwa nini wote wako makao makuu TBC :A S-confused1:na siyo mikoani???
 
Sawa na kushangaa kwa nini idadi kubwa ya wachoma nyama Dar ni wachagga wa Rombo ingawaje si wafugaji!!!
 
Aliingia kwa uhusiano na wanasiasa japo alifanya mengi kuibadili TBC na kuifikisha hapo ilipo na ameondoka kwa uhusiano huo huo. Kitu cha kuzingatia hapa ni kuwa wanasiasa wachache sana wameshika nchi hii na wanafanya maamuzi kwa niaba ya watanzania wote milioni 40. Tatizo kubwa hapa ni kuwa wanasiasa hao wachache vi vilaza na mbaya zaidi mafisadi. Ukiangalia mtiririko wa mambo toka kabla ya uchaguzi mpaka leo hii na ukahusisha mtiririko wa mambo kabla na baada ya uchaguzi wa 2005 utaona mambo haya ya ajabu.
 
NImefurahi sana Tido kuondolewa hasa nikikumbuka jinsi alivyomdhalilisha waziri mkuu pinda kwa kumuweka kama pambano la utangulizi ili lowassa aongeee later

safi sana serikali

Naomba ajaye awe professional, neutral and asitoke dailynews wala habari leo na wala siwe na any association.... pia asiwe salva rweyemamu, muhingo rweyemamu au kibaraka mwingine kwani hao wamenifanya nidhani kwamba huna haja ya kusomea uandishi kabisa...
mkuu tunashukuru kwa mtizamo ''binafsi''

lakin ninaomba kutofautiana na wewe ''ki-mtizamo''

Tido was The Man
 
Na nani alisema yeye kufanya kazi BBC ndo kinga ya kutositisha mkataba wake....c'mon people.
If he perfomed well and good, if he did not haya tena...
Uzuri ni sisi wenyewe tunapima hiyo perfomance yake!

Nightangale, the unfortunate thing is SIO SISI TENA tunapima Perfomance ya wanaotekeleza majukumu ya taifa. Kama ukifuatilia mjadala huu vizuri, unaona bila shaka yeyote kwamba ufisadi ndiyo nguvu kubwa inayoleta mabadiliko katika mifumo yetu. Na hata kama sisi(wananchi) tungekuwa tunamwona TIDO kama mchapakazi ambaye angetusaidia kuendeleza kile kitengo chetu tena kwa muda, bado tusingeweza kushawishi hao wenye maslahi binafsi wafanye tofauti na walichofanya. Na ninaweza kuhakikishia (labda wajitokeze wapinzani ), swala la Tido halitajadiliwa katika kikao cha bunge kinachofuata. Maana yake nchi inatawaliwa bila kanuni bila sheria, inakwenda kwa utashi wa kiufisadi tulioulea sisi wenyewe! Inasikitisha.

Lakini binafsi, Tido alikuwa ananiuzi sana alipokuwa anaelekeza matangazo ya TBC kwenye kiingereza, kama vile kubeza kiswahili. Nililaumu sana kubadili jina la TVT kuwa TBC! Niliona kama ukoloni mambo leo! Nilimwona kama bado alikuwa na tongotongo ya Uingereza. Kwa hivyo sikuwahi kumpenda kwa sababu hii. Ila kile chombo kimefanya maendeleo makubwa na kwa ajili hiyo napenda kumpongeza Tido na Timu yake kwa pamoja.
 
Watanzania tujifunze kumove on. Jamani Tido has been there for our years. Sasa I think this is a right time to move on with other things. Tatizo kubwa la wengi wetu ni kuona kwamba watu fulani wana hati miliki za kazi fulani. Na wala mimi sioni kosa la serikali. Imemuondoa baada ya mkataba wake kuisha. Sasa hizi conspiracy theories ni za nini? Jamani the guy has been with BBC miaka kibao..kafanya kazi RTD na kwingineko. Nadhani kwa sasa ni wakati muafaka wa yeye kukaa chini na kuwa mbunifu na kufanya mambo yake binafsi katika tasnia ya habari kama akina Jeff Koinange. Kwa nini umri ule uwe bado unang`ang`ania kuajiriwa? Mi nadhani uzoefu wake wa BBC..unamtosha kabisa kuwa hata media consultant mkubwa sana bongo..tatizo watu wanapeana hivi vyeo kwa kujuana..hata leo ukiondolewa bila kufuata utaratibu...huwezi lalamika..

Cha muhimu kazi itangazwe watu washindanishe vyeti na uzoefu..and best candidate apewe nafasi. Hii kasumba ya kutegemea kwamba ni mtu fulani tuu ndo anaweza kuwa mkurugenzi au waziri tuu...nadhani watanzania tunajinyima opportunity ya mambo mengi.

Tido go home..na nitakuheshimu usipoomba ajira tena..Jiajiri..hata vijana wetu waje kuomba internship ya kufanya kazi na mtu mzoefu kama wewe....

Mwisho kabisa nawashauri watanzania wenzangu. Kazi nzuri ya kuajiriwa ni ile kazi uliyosomea! Omba kama wengine..bila KUBEBWA..hata kazi ikiisha unaondoka vizuri...na unaenda kwingine wanakupa kazi kutokana na elimu yako na uzoefu wako... Hii ya kushikwa mkono na mjomba sijui shemeji..my friend..akiingia mwingine ambaye hakujui....taabu inaanzia hapo.
 
nimefurahi sana tido kuondolewa hasa nikikumbuka jinsi alivyomdhalilisha waziri mkuu pinda kwa kumuweka kama pambano la utangulizi ili lowassa aongeee later

safi sana serikali

naomba ajaye awe professional, neutral and asitoke dailynews wala habari leo na wala siwe na any association.... Pia asiwe salva rweyemamu, muhingo rweyemamu au kibaraka mwingine kwani hao wamenifanya nidhani kwamba huna haja ya kusomea uandishi kabisa...

unaweza shangaa analetwa mmoja kati ya hao uliowataja
 
wako wapi wale waliokua wanailaani TBC nao waseme yakwao?? maana hapa naona zimejaa sifa wakati very short while ago nilizoea kusoma mabaya kuhusu TBC na huyu baba??

Au ndio wale mbayuwayu sisi??

Human nature..... ni balaa!! Kweli binadamu tuna maajabu sana tu duh!
 
Back
Top Bottom