TICTS wagoma!

The Fixer

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
1,365
583
Leo asubuhi Wafanyakazi wa Kitengo cha kupakuwa makontena katika hii Bandari ya Salama wameanza mmgomo wao kufuatie kile ambacho waliona kama kuwa na wasiwasi wa mafao yao pale ambapo kuna tetesi kuwa TICTS inaweza kusimamishwa kutoa huduma hiyo na serikali.
Wafanyakazi hao amboa walimwandikia CEO Bwana Nivel na kutaka kujua kama TICTS watasimamishwa wao kama wafanyakazi watalipwa vip ? kwakuwa katika mikataba yao hakuna mahala ambapo TICTS inaonyesha kama wao wakikwamisha mkataba malipo yanakuwaje ?

More updates baadae.........!!
 
They have all the resons kuwa makini tetesi zinaendelea kukuwa kila muda unavyosonga mbele!!
 
Mkuu,
Wakafanye kazi nani amewambia kuwa inasimamishwa.Tetesi hazifai, tafuta ukweli mwenyewe kabla ya kugoma.
Kweli itaongelewa bungeni, lakini hakuna mwenye uhakika kuwa itasimishwa.
Kafanye kazi malipo yatakuwepo angalia sheria kwa mtu ambaye ameshafanya kwenye kampuni zaidi ya miezi 3, lazima alipwe mfao yake
 
Ngoja tusubiri yetu masikio na macho.Lakini ninavyolifahamu bunge letu ni makelele tuuuu hakuna la maana litakalo amuliwa
 
Kumbukumbu zangu zinaonyesha kuwa katika hotuba za mheshimiwa jk kuna siku alisema kuwa haoni hatari kama wizara au idara ya serikali kuanza moja akiwa na maana ya kufuta kila kitu na kuanza moja

hili la ticts linawezekana kabisa maana hata mzee pinda alisema bungeni kuwa wameprove kuwa ticts haina faida kwa serikali

wazee nyie gomeni serikali isiogope kupata hasara ya mwaka kuliko kukumbatia ugonjwa ambao utatutesa na unaendelea kutesa watanzania na kutuchafulia jina

gomeni wakuu ili haki ipatikane
 
ah aaahh!! hii sio habari nzuri hata kidogo.... wengine tuna mizigo yetu pale bandarini ..hii itakua imekaa vibaya sasa
 
Sio kweli hakuna mgomo wowote Ticts tena sasa hivi hata msongamano umeisha watu wanapiga kazi na kawaida. Kwa kuwa tayari tuna negative attitude kwa Ticts kila kitu ni rahisi kuonekana kweli...Halafu pia tunahitaji kidogo elimu kuhusu mambo ya meli maana siku hizi kuna waandishi wa habari tena waandamizi kazi yao ni kwenda pale ferry magogoni wanahesabu meli wanazoziona baharini uko na kurudi kuandika habari, huu ni upuuzi sio kila meli inapakuliwa na ticts...tena takwimu zinaonyesha kuwa mamlaka ya bandari ndio wanapakua meli nyingi zaidi...watanzania mnaingizwa kwenye mambo msiyoyajua. kuna jamaa anaitwa Igogo yeye ana washirika wenzake ndio wanataka kuleta kampuni nyingine ichukue nafasi ya ticts na huyu ndie anayelipa waandishi wote wanaoandika habari mbaya kuhusu ticts.
 
jamani jamani kama hamna data ni vizuri mkakaa kimya
wewe unayesema kuwa kuna mtu ana kampuni yake anataka kuipiku ticts nani kakuambia
sidhani kama waziri mkuu alikurupuka na kusema kuwa ticts wameonyesha kuwa kazi wameshindwa
 
Mzee amini usiamini mambo haya ni ya kweli, yafanyie kazi utajua undani wake. Kuna jamaa mmoja anaitwa Chagama yeye ni kati ya waratibu wakuu wa zoezi hilo. Unataka mpaka upewe jina la kampuni waliyoiandaa nini?
 
Back
Top Bottom