Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Mag3,
Ahsante kwa ufafanuzi wako wa kina kuhusu suala hili. Sina sababu ya kutotaka kulielewa hili kwa kuwa wanaohangaika ni ndugu zetu, Watanzania wenzetu. Wengi wa Wazee wetu hawa waliendelelea na AJIRA zao kwenye mashirika mapya ya UMMA yaliyoanzishwa kuchukua nafasi ya haya ya EAC iliyovunjwa na wanasiasa wetu. Kwa nini madeni na mafao yao haya hayakurithiwa na mashirika haya mapya?
WildCard,
Kumbuka kuwa EAC ilikuwa ni jumuiya ya kimataifa na ilikuwa na bunge lake, service commission yake, pensions fund yake na saving scheme yake. Makato ya pension yalitunzwa Uingereza kwa agents wa EAC waliojulikakna kama "crown agents". Mkataba wa EAC ulisema kuwa ikitokea jumuiya ikavunjika waajiriwa wake walipwe fedha zao kwanza ndio mengine yafuate, period. Pia walioainisha namna ya kulipa hizo kulingana na thamani halisi ya dola na riba ya asilimia 7%. Pia kumbuka kuwa baada ya muda mrefu serikali iliwahi kutamka kuwa madai ni makubwa kuzidi uwezo wa serikali - swali ni kwa nini hawakulipa mapema ?
Walioendelea na ajira kwenye serikali ilikuwa kwa matakwa yao na siyo wote walifanya hivyo. Kwa waliofanya hivyo ilitakiwa waingie mkataba mpya na serikali bila kuhusisha madai ya pesa zao toka EAC. Katika kutafuta upenyo wa kuwaibia wananchi wake ndio serikali ikataka kulazimisha hayo unayoongelea lakini nje ya utaratibu. Haingewezekana madai yao yakarithiwa na mashirika mapya, hii haiingii akilini hata kidogo kwa sababu hawakuwa na mkataba wowote na serikali. Wezi hawa wanatakiwa waache usanii na wazee wapewe haki yao ambayo haitapotea hata kama itadaiwa na vitukuu wao.