Naibu Waziri Sagini amuwakilisha Waziri Mkuu katika Uzinduzi wa Idara ya JMAT

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
IMG_9001.jpeg
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amemuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika Halfa ya Uzinduzi wa Idara Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) iliyofanyika Novemba 8, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Karimjee Hall Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Naibu Waziri, Sagini ameihakikishia Jumuiya ya Maridhiano na Amani JMAT kuwa salamu zao walizomtuma kufikiasha kwa Waziri Mkuu zimefika bila wasiwasi na wategemee ushirikiano mkubwa.

"Mimi kama Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi nimepokea salamu zenu niwahakikishie kuwa yote mliyoeleza katika hotuba yenu pia kuhusu Wizara yangu yatafanyiwa kazi," amesema.

Aidha, Sagini amewapongeza JMAT kwa kuwa na Idara nyingi zenye wasomi na kutaka wasomi hao kutenda kazi kwa taaluma zao ili kuleta matokeo chanya katika Jumuiya na kwamba Idara mbalimbali zinazoenda kuanzishwa ndani ya Jumuiya hiyo zitaleta tija na watakamilisha majukumu yao kikamilifu.

IMG_9002.jpeg

Amewataka watu wa Idara ya uchumi kuhakikisha watatumia mbinu mbalimbali ili kujikwamua kwenye changamoto ya kibajeti pindi wanapokuwa wanatekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo uandaaji wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo.
 
Back
Top Bottom