This is too much.. Wazee nao warusha mawe Hazina!

na mie nasubiria tu za mzee wangu, kulipa washalipa ndiyo lakini hawakulipa inavyotakiwa ndio maana malalamiko yapo, wanadhania wanaweza dhulumu jasho la watu hivi hivi, mie mzee hadi anakaribia kufa aliniambia mahesabu ya haki zake zote yanakaribia m.100 kwa rate za wakati huo, na hiyo ilikuwa miaka 6 iliyopita.

Mahesabu kama haya ya milioni 60, milioni 100,.... za mwaka 1977 ndio yanayofanya zoezi la ulipaji kuwa utata mtupu!
 
Heko wazee!!!!!!!!!!!

Kikwete lazima atambue nchi inaenda pabaya. Mawe yaliyorushwa na waalimu,
wakazi wa Chunya na tena Wastaafu wa EAC ni viashiria vya kutosha kwamba
wananchi wameuchoka ufisadi na danganyatoto ya nchi hii.
 
Its a pity TAIFA LETU LINASHINDWA KUHURUMIA WAZEE - wengine wametoka mbali mikoani - wana -incur expenses kuja mjini, kuishi ili wapate haki yao - MZAZI SIO YULE ALIYEKUZAA TU - ILA ALIYESAWA NA BABA/BABU YAKO - OUR PRESIDENT SHOULD INTERVENE - OTHERWISE ITS A CURSE FOR OUR NATION TO MISTREAT THE ELDERLY
- GOD WATCHING AND HIS JUSTICE PREVAILS ALWAYS
 
Kikwete 'saddened' by stoning of motorcade
By The Citizen Reporter
THE CITIZEN

President Kikwete was "deeply saddened" by the stoning of his motorcade in Chunya District, Mbeya Region, on Wednesday evening, a State House official said yesterday.

Communications director Salva Rweyemamu told the BBC that the President, whose limousine and escort vehicles were not affected, was informed of the incident at Kanga Village after arriving in Mbeya.

"The President expressed his deep sorrow when told of the stoning," Mr Rweyemamu said in an interview last evening from Mbeya where he was accompanying President Kikwete on a tour of the region.

He said the villagers stoned several cars in the motorcade out of anger at around 7.30pm after the convoy did not stop to allow the President to greet local residents who had been waiting for him for several hours.

"The President usually stops to greet the people during his visits. However, there was no time for this on Wednesday evening. What happened at Kanga was a spontaneous reaction by some people who were angry at not getting the opportunity to see the President," Mr Rweyemamu said.

Asked why President Kikwete could not stop and greet the villagers even for a few minutes, Mr Rweyemamu said it was getting late, and this had ruled out the possibility of the Head of State stopping again before arriving in Mbeya.

He added that there was a big crowd of people who were singing and chanting in anticipation of being addressed by President Kikwete. Mr Rweyemamu noted that President Kikwete had earlier addressed public rallies in Makongolosi and Mkwajuni areas in the same district.

Two people were injured and six cars, including one carrying a Cabinet minister, were slightly damaged in the incident. Meanwhile, there were unconfirmed reports that police had arrested several suspects in connection with the stoning.

However, Mbeya regional authorities could not be reached for comment on the incident and reports circulating on the Internet that several people were injured and admitted to hospital during an operation to trace the suspects.

Following the incident, Civic United Front secretary-general Seif Shariff Hamad urged the President to initiate a national debate to discuss the "worrying political situation in the country".

Mr Hamad told The Citizen in his office in Dar es Salaam that political developments in the country called for quick action to prevent the situation from deteriorating. He added that the Mbeya incident is a sign that people were getting tired and needed to be reassured.

"We need to have a national dialogue involving all stakeholders, including community-based organisations, religious leaders, politicians, academicians and human rights activists to rescue the country," he noted. He said the Government should look at its own performance and tackle problems that were bothering the people.

Meanwhile, President Kikwete yesterday advised Tanzanians living in Zambia who had been issued a repatriation notice to return home.

He made the remarks after receiving information from Mbozi District Commissioner Halima Kihemba that about 250 Tanzanians living in Zambia had been ordered to leave the country.
" I advice them to strictly adhere to the order issued by the government of Zambia without any delay," he said.

Additional reporting by Brandy Nelson
 
Date::10/17/2008
Rais Kikwete asikitishwa na waliompopoa mawe
Salim Said na John Stephen
Mwananchi

Rais Jakaya Kikwete amesikitishwa na kitendo cha wananchi wa Kijiji cha Kanga wilayani Chunya kuurushia mawe msafara wake na kuwajeruhi baadhi ya watu waliokuwa kwenye msafara huo.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu wakati akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) baada ya msafara wa Rais Kikwete kushambuliwa kwa mawe na wananchi wa kijiji hicho.

Rweyemamu alisema kuwa Rais Kikwete amesikitishwa na tukio hilo na kwamba, alishindwa kusimama na kuwasalimia wananchi wa kijiji hicho kwa kuwa muda haukuruhusu kufanya hivyo.

"Rais amesikitishwa kwa kuwa alishindwa kusimama na kuwasalimia wananchi, lakini pamoja na hayo mazingira ya jana asingeweza kusimama," alisema Rwehemamu.

Alisema tukio hilo, lilitokea baada ya saa 1:00 jioni na kwamba, baadhi ya vijana waliurushia mawe msafara huo baada ya kuona Rais anawapita bila kusimama na kuwasalimia.

Kufuatia kupigwa huko kwa mawe kwa msafara wa Kikwete juzi Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amemtaka Rais huyo kuitisha kongamano la kitaifa la wadau wote kujadili na kutafuta suluhu ya hali mbaya ya nchi.

Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalum ofisini kwake Buguruni jijini Dar es Salaam jana Hamad alisema nchi inayumba kwa kukosa mwelekeo wa kiongozi imara na kwamba inavimba huku wakionya kuwa wakati wowote inaweza kupasuka.

Hamad alisema, kitendo cha kuhujumiwa kwa msafara wa kiongozi wa taifa ni ushahidi kuwa nchi imevimba na kwamba wakati wowote inaweza kupasuka.

"Bila ya kuona aibu Rais aitishe kongamano la kitaifa la wadau wote yaani vyama vya kijamii, viongozi wa dini, wasomi, wanasiasa, mashirika ya haki za binadamu na taasisi zisizo za kiserikali kuinusuru nchi yetu kwa sababu inayoyoma," alishauri Hamad.

Alisema serikali lazima ikae chini na kufikiria mahali gani ilipojikwaa na kujirekebisha kwa kuwa matukio kama hayo hayaashirii mambo mazuri bali ni mabaya tu.

Alimwomba Rais kukaa kitako na kutafakari kwa kina nchi inakoelekea kwa sababu inahitaji uongozi imara na kudai kwamba nchi inayumba kama jahazi lililokosa mwelekeo kwa kukosa uongozi imara.

"Serikali lazima ikae chini na kufikiria mahali gani ilipojikwaa na kujirekebisha haraka kwani matukio kama haya hayaashirii mambo mazuri bali ni mabaya tu" alisema Hamad.

Alisema, Rais Kikwete bado anayo nafasi ya kujirekebisha na kurudisha imani ya Watanzania kwake na kwamba asitafute sababu rahisi za matokeo hayo kushambuliwa kwa misafara yake.

"Kila siku misafara inapozomewa au kupigwa mawe tunaambiwa ni wahuni au walevi ndio waliofanya hivyo, lakini ulevi na uhuni haukuanza leo wala jana. Hivyo wasitafute sababu rahisi rahisi" alisema Hamad.


Aidha alisema, Tanzania inasifika kwa utulivu, uvumilivu, usalama na amani kwa watu wake, na kwamba matukio ya kuhujumiwa kwa misafara ya viongozi yanaonesha kupotea kwa rasilimali hizo.

Hamad alilaumu kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya John Mwakipesile cha kupeleka vikosi vya askari wa kutuliza fujo (FFU) kutuliza ghasia na kukamata wahusika akidai kuwa siku zote matumizi ya nguvu na mabavu hayatatui migogoro ya kisiasa.

"Kitendo chenyewe kimefanyika usiku, kwa hiyo Polisi watakamata na kupiga watu hata wasiohusika, wangepeleka makachero ningekubaliana nao lakini si Polisi kwa kweli," alilaumu Hamad.
 
Du, tutayaona mengi ya mfano huu siku zijazo. Yetu macho. Its a bad sign, selikali inatakiwa kujipanga upya kwa kuwa wananchi wamechoka na kupanda kwa gharama za maisha kulikofumbiwa macho na viongozi wakuu.
 
Du, tutayaona mengi ya mfano huu siku zijazo. Yetu macho. Its a bad sign, selikali inatakiwa kujipanga upya kwa kuwa wananchi wamechoka na kupanda kwa gharama za maisha kulikofumbiwa macho na viongozi wakuu.


Ni jambo la kusikitisha and for the first time in the political history of Tanzania involving a presidentail motorcade!!! Something crucial need to be addressed soon!!! It is a bad warning signal!!!! Correct me if I am wrong!!!!
 
Hiyo ni tanzania inayobadilika taratibu, kurusha mawe, migomo kila mahali, huwezi kuamini hata wale wazee wanaodai mafao yao ya Afrika Mashariki wanakaa na kuziba njia ya hata kupita viongozi au wageni pale Wizara ya Fedha au wanakwenda kulia ikulu. Ni wazee haohao zamani walikuwa wakiwalaani watoto wao wanaogoma katika Vyuo Vikuu, leo wanazomea FFU wenye mitutu. Ni walimu wenye maadili sasa wanapigana viti Diamond Jubilee, wanawarushia mawe polisi. Naona zama zilizobadilika, zinazotupeleka mahali fulani. Siamini, hii ni hali mbaya! Raisi haheshimiwi, haogopwi, polisi wanawakebehi. Suala siyo kukamata watu, ni kujiuliza kwa nini? Unapoona moshi unafuka tafuta moto uko wapi
 
Mahesabu kama haya ya milioni 60, milioni 100,.... za mwaka 1977 ndio yanayofanya zoezi la ulipaji kuwa utata mtupu!
utata wanaweka wenyewe, kwani wamekosa watu wa kukokotoa hizo pesa kwa thamani halisi ya hela yetu against the dollar, its as simple as that, sema hizo pesa washazitumia kwa mambo yao hilo ndio linaleta utata!
 
Kisa msafara wa Raisi kikwete Kupigwa mawe kinanikumbusha kisa kimoja kwenye Biblia amabapo wapagani kama mimi waliokuwa wakimpeleka Yesu kusulubiwa walimvalisha vazi la kifalme na kumwambia yeye ni mfalme wa wayahudi halafu wakaanza kumtemea mate na kumpiga vibao na mijeledi barabara mfululizo non stop.

Na Raisi Kikwete naye alipofika Mbeya wapagani wanyakyusa wa Mbeya wakamvalisha vazi la Kichifu na kumtangaza rasmi kuwa yeye ni Chifu Mwangupili halafu wapagani wanyakyusa hao hao wakamtandika Chifu huyo na mawe barabara mfululizo nonstop na msafara wake na kumfanya kuwa chifu wa kwanza wa kinyakyusa msafara wake kupigwa mawe na waliomvisha vazi la kichifu.

Hii lazima iwekwe kwenye rekodi kuwa kuna Chifu wa Kinyakyusa alishawahi kushambuliwa kwa mawe kwenye maktaba za wanyakyusa.

Walahi wapagani hawatabiriki.Siku ingine watu wakitaka kumvisha vazi la kichifu akumbuke yaliyopata Yesu akatae.
 
utata wanaweka wenyewe, kwani wamekosa watu wa kukokotoa hizo pesa kwa thamani halisi ya hela yetu against the dollar, its as simple as that, sema hizo pesa washazitumia kwa mambo yao hilo ndio linaleta utata!

Unajua nini MamaParoko, hata tunaostafu sasa hivi, hakuna anayelipwa kiasi hicho!
 
Kikwete 'saddened' by stoning of motorcade
By The Citizen Reporter
THE CITIZEN

President Kikwete was "deeply saddened" by the stoning of his motorcade in Chunya District, Mbeya Region, on Wednesday evening, a State House official said yesterday.

Communications director Salva Rweyemamu ...

He said the villagers stoned several cars in the motorcade out of anger at around 7.30pm after the convoy did not stop to allow the President to greet local residents who had been waiting for him for several hours.

...

nadhani ni majibu mepesi kwa maswali magumu. naamini majibu ya kina zaidi yangeweza kutolewa.
 
I doubt if anxiety to see someone can turn into stonning the same person you were eager to see.

Kikwete and your buddies, stop pretending that you don't see what is going on. The people are angry. Your obedient servants are tired of your incompetence and corrupt leadership. If you dont change, you shouldn't be supprised to continue losing elections, even to idiots.
 
usifananishe hali ya wastaafu wa EAC na wastaafu wengine, rejea maelezo ya mag3 kuhusu utata wa pesa hizo, ina maana wewe utakubali kweli kulipwa madai yako ya mwk lets say 70 kwa thamani ya hela ya wakati huo, is that fair? hela yetu imebadilika kiasi gani, afadhali hiyo pesa ingekuwa inatoka mfukoni mwa serikali, lakini hiyo pesa siyo ya serikali, period na wanavyoendelea kulimbikiza ndo interest inavyozidi kupanda.
 
Utabiri na busara zangu zinanionyesha kuwa rais lazima afanye kitu kikubwa tarehe 2 Novemba...sikuwa nimefahamu kuhusu siri ya tarehe 3...

Aite wahariri azungumze kuhusu kadhia mbalimbali za taifa hili...EPA, Mikataba ya madini, Richmond, TICTS, EAC, Walimu...arejeshe matumaini
 
Well, walilala barabarani Mwanjelwa kumzuia ili awasikilize, ikaonekana kama tukio la kawaida. sasa wamefikia hatua hiyo kama njia ambayo wananchi wameona wafikishe ujumbe wao, iwapo hawataeleweka kama awali, sijui watachukua hatua gazi zaidi. Silaha waliyokuwa nayo karibu ni mawe, je wangekuwa na AK 47?
 
usifananishe hali ya wastaafu wa EAC na wastaafu wengine, rejea maelezo ya mag3 kuhusu utata wa pesa hizo, ina maana wewe utakubali kweli kulipwa madai yako ya mwk lets say 70 kwa thamani ya hela ya wakati huo, is that fair? hela yetu imebadilika kiasi gani, afadhali hiyo pesa ingekuwa inatoka mfukoni mwa serikali, lakini hiyo pesa siyo ya serikali, period na wanavyoendelea kulimbikiza ndo interest inavyozidi kupanda.

Nakubaliana na wewe. Sheria ya kustaafu inasemaje kuhusu mafao haya? yanakuwa na INTEREST yanapocheleweshwa kulipwa?
 
mie sijui sheria inasemaje kuhusu hilo ila natumia common sense tu, mbona walituambia kuwa wametenga bilion 400 kulipa hayo madai, zilitoka wapi na ziko wapi?
 
Ujumbe wamefikisha, hii ya Salva ni majibu ya kisiasa, lakini Jk na serikali kwa ujumla wamejua nini kinakuja. Na sasa amejua silaha si askari wengi, si ameyaona Tarime?
 
Kuna mawe mengine yanakuja kumbonda.

Nayo yanatokana na hoja ya kadhi kutaka iingizwe katika katiba.

Asipoingiza hoja ya kadhi kwenye katiba Waislamu watambonda mawe yeye na msafara wake maana wamepania aaingize.

Akiingiza hoja ya kadhi kwenye katiba Wakristo watambonda mawe na msafara wake maana tayari wameshaapa na kutoa matamko ya kutishia nyau.

Na wapagani wasiokuwa na dini wasiopenda udini uwemo kwenye katiba vile vile hawatakuwa nyuma kumvurumishia mawe yeye na msafara wake kwa kugeuza katiba iwe na dini ndani.

Kazi kwake na hao walio kwenye msafara wake.

Wale walio katika msafara wa Kikwete walioko kwenye bunge,serikali na mahakama kama wanafikiri mawe yakivurumishwa hoja ya kadhi ikikubaliwa au kukataliwa kuwa mawe yatampata Kikwete peke yake wanaota ndoto za mchana.Kila aliye kwenye msafara ajiandae kubondwa jiwe.

Nyerere alipokataa nchi isiwe ya kidini sasa ndio mtajua kuwa mzee wa watu alichokuwa akiogopa ni kubondwa mawe na si kitu kingine akaona dawa ni kuachana na mambo ya dini kwenye bunge,serikali na mahakama ili mawe yampite pembeni.
 
Back
Top Bottom