The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

KadaMpinzani

Source umeiona mwenyewe.... kumbe Mkandara alikuwepo
 
Ama kweli, Mrema ni mzee wa michapo. Ametuvunja mbavu katika mkutano wa hadhara Mwanza, kwamba Zitto ni mbwa wake. Eti yeye amechoka na kuzeeka, lakini walau anaweza kuwaamuru mbwa wake akina Zitto na Dk. Slaa, "kamata yule, kamata yule." Mbavu hatuna!

Labda kaiga msemo ambao una umaarufu mkubwa Marekani "That is my dog."
 
NADHANI ITAKUWA NI VIZURI SANA KAMA AKITAJA WALIOHUSIKA KWENYE ISSUE YA DHAHABU, tuombe Mungu tu asife au asiwe chizi kabla ya kufika hiyo tarehe 15. INAWEZEKANA KUWA WOTE WALIOHUSIKA WALIENDELEA KUTESA na HUENDA MPAKA SASA WAKO FREE?
 
Mrema kustaafu siasa

na Joseph Senga, Makambako

MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, amesema anaweza kupumzika wakati wowote kujihusisha na masuala ya siasa ndani ya vyama vya upinzani na badala yake kuwa mshauri tu ndani ya vyama hivyo.

Akihutubia katika mkutano wa hadhara wa vyama vinne vya upinzani mjini hapa juzi, Mrema alijigamba kwamba, atafanya hivyo kwa kuwa amepata vijana watakaochukua nafasi yake kisiasa.

Alisema awali baadhi ya wananchi walimshauri kupumzika katika masuala hayo, lakini alishindwa kufanya hivyo kwa kuwa hakukuwa na mtu wa kumwachia kuendeleza mapambano aliyoyaanzisha ndani ya vyama vya upinzani.


“Na mimi sasa nitakuwa Kingunge wa vyama vya upinzani, kwa kuwa sasa ninao watu watakaovaa viatu vyangu. Wakati ule wapo walionifuata na kunishauri niachane na siasa eti nimezeeka, ningemwachia nani nchi hii? Ningemwachia nani mikoba yangu? Sasa yupo Zitto na Dk. Slaa, nitawakabidhi mikoba yangu yote waendeleze mapambano,” alijigamba Mrema.


Alisema, kwa kuwa CCM wanao viongozi ambao wamezeeka na sasa ni maarufu kama washauri wakuu wa chama hicho, akimtaja Kingunge Ngombare - Mwiru, hivyo na yeye angetamani siku moja kuwa mshauri wa vyama vya upinzani, akijifananisha na kigogo huyo wa CCM.


Mwenyekiti huyo wa TLP ambaye yuko katika ziara ya vyama vinne vya upinzani katika baadhi ya mikoa, alisema wabunge wa upinzani wameonyesha njia ya kufuata nyayo zake na wameonyesha umahili wa kuthubutu kuikemea serikali ya CCM kwa kile alichokiita udhalimu na ufisadi wa viongozi wa chama hicho.


Alisema, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kushirikiana na wabunge wengine wa vyama vya upinzani, ndio wanamfanya aone haja ya kukabidhi mikoba yake kwao, ili waendeleze mapambano ya kisiasa nchini.


Ziara za viongozi hao wa vyama vinne vya upinzani ambavyo ni CUF, CHADEMA, TLP na NCCR- Mageuzi, imekuwa ikiacha gumzo na mijadala mbalimbali katika kila mikutano inayofanywa, kutokana na sera zinazoelezwa kuwagusa wananchi wa kila rika.


Moja ya hoja iliyoibuliwa na viongozi hao ni pamoja na kuanzishwa kwa Azimio la Songea, kwa lengo la kuanzishwa uhamasishaji wa wananchi kuunga mkono vuguvugu la ukombozi na kulinda rasilimali.


Hadi sasa viongozi hao wamefanya mikutano katika mikoa saba, wakizunguka kwa kutumia helikopta, ambayo ni Mwanza, Shinyanga, Tabora, Rukwa, Mbeya, Ruvuma na leo wanatarajiwa kukamilisha ziara katika Mkoa wa Iringa kabla ya Mkoa wa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.



Source: Tanzania Daima.

Hii itakua mfano mzuri kwa upinzani, hatutaki kuona sura za aina moja miaka nenda rudi.Vijana tupo tayari kuvaa viatu vya akina Mrema,au bado tumekolea kuishi mamtoni?
 
mhh,kidogo ningekurupuka nimpe hongera.Hapa nahitaji subira nisijeumbuka bure.Ila Mrema tueche utani sasa tuwe serious,ng'atuka mzee hilo ni ombi tu maanake tukikupigia kelele utaanza kutuita majina ya ajabu ajabu kabisa.
 
Huyu Mrema ni mbumbumbu anayetumiwa na CCM bila kujijua. Mtu aliyefikiri atakuwa rais kwa utapeli. Aeleze kama ni haki kununua nyumba binafsi kwa pesa ya chama. Baada ya uchaguzi 2000 na maandamano yaliyofuatia uchaguzi huo huko visiwani, huyu bwana kwenye mikutano yake alikuwa akisema CUF ni ngangari lakini yeye ni ngangari kinoma. Sasa hivi baada ya hoja ya Zitto bungeni, ameishupalia lakini ukimuangalia kwa makini huyu ni tapeli kuliko hawa kina Karamagi. Opportunist anayeelekea kwenya kaburi la kisiasa.
 
mmhh!!!
hapo yetu macho...anyway perhaps he means what he says...siju kina njomba malecela,kingunge,mangula (aliyeangushwa juzi),etc wao wanasubiri nini,maana wako kimyaaaaaaaaaaaaaa despite madongo direct toka kwa Muungwana na PM wake....
 
rais mwinyi aliwahi kusema upepo ukivuma huna uwezo wa kuuzuia, kura za maoni zilionyesha 20% ya watanzania wanataka vyama vingi akasema maadam duniani sasa wimbo ni huo tusishindane tuingieni.

na sasa upepo uliopo wazee wapumzike kwa nguvu au hiyari, sasa kila mtu apige mahesabu.

Lipumba nasikia yeye anampango wa kun'gatuka, sijui Maalim Seif au hadi na yeye ya mkute ya Shamhuna na wenziwe,

na Mrema wahi mkuu yasije kukuta usiyoyapenda jiondoe bila ya watu kupika pilau ya kukun'goa kwa nguvu
 
Kila la kheri mzee wa Kiraracha, baada udikteta, undumilakuwili, ugeugeu, unafiki, uroho wa madaraka etc hatimae ameanza kusoma alama za nyakati.

Hata hivyo mchango wako si haba ktk kulijenga taifa na upinzani.. nenda, nenda kampuzike Lyatonga..
 
Naomba kuliza umri hasa wa kung`atuka kwenye siasa ni kuanzia miaka mingapi? Kwani watu wanastaafu ktk kazi zao na nawaona wanaelekea kwenye siasa na pia nimesikia viongozi wakisema wazee waachie ngazi lakini naona hata yule anayetaka wenzake wang`atuke na yeye kama tayari ni mzee.
 
Sasa hivi baada ya hoja ya Zitto bungeni, ameishupalia lakini ukimuangalia kwa makini huyu ni tapeli kuliko hawa kina Karamagi. Opportunist anayeelekea kwenya kaburi la kisiasa.

You gat be kidding me....

Mrema ni tapeli kuliko Karamagi?
That's........................
 
...Mrema angekuwa mbunge kelele zake zingesaidia sana bungeni lakini kwa ofisi ya pale Manzese bora akapumzike tuu na tunashukuru amejua hilo.
 
Duh hii kali...Mrema kapumzike au ukaanzishe kampuni ya Ulinzi. Maana zile sungusungu na Polisi ni CV tosha ya kuwa na kampuni yako ya Ulinzi kujilia vya uzeeni...
 
Mhh,mimi nitakua nikimuomba taratibu tu apumzike asije niita sijui jina gani lile............
 
Mahakama yaamuru Mrema akamatwe..

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imeamuru Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) Augustine Mrema na mwenzake, wakamatwe kwa kuwa wameidharau mahakama.

Hayo yalisemwa jana na Hakimu Mkazi Said Msuya anayesikiliza kesi ya kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya serikali, inayomkabili Mrema na Tundu Lissu.


Hakimu Msuya aliamuru Mrema na Lissu wakamatwe kwa kushindwa kufika mahakamani wakati kesi yao ilipotajwa na kwamba hawakutoa taarifa na wadhamini wao hawakuwepo.


Akiomba hati ya kuwakamata, Mwendesha Mashitaka Pamphily Mhollely, alidai mara kwa mara washitakiwa hao wamekuwa na tabia ya kutofika mahakamani siku ya kesi yao bila kutoa sababu za msingi na kwamba hata wadhamini wao hawaonekani.


“Upande wa mashitaka tunaomba hati ya kuwakamata washitakiwa, kwani wanajua kuwa leo (jana) ni siku ya mahakamani, lakini hawajaonekana wala wadhamini wao hawapo, hii ni dharau kwa mahakama na lazima vitendo hivi vikomeshwe ili mahakama iheshimike,” alidai Mhollely.


Aliongeza: "Hatuna taarifa kwa nini hawajafika, tunaomba hati ya kuwakamata ili waje kujieleza kwanini dhamana zao zisifutwe kwa kukiuka mashariti ya dhamana kwa kuacha kuja mahakamani siku ya kesi.”Mrema na Lissu wanadaiwa kutoa maneno ya uchochezi katika jamii dhidi ya serikali ambayo waliyatoa katika mkutano wa hadhara huko Manzese, Argentina wakati Mrema akihutubia mwaka 2002.


Baadhi ya maneno yanayodaiwa kutolewa na Mrema na kwamba ni ya uchochezi na kusababisha uvunjifu wa amani katika jamii ni: “Serikali ya awamu ya tatu haiwajali wananchi wake, kwani wachimbaji wadogo wadogo wa Bulyanhulu wamezikwa hai kwa kufukiwa katika machimbo, lakini serikali haikuchukua hatua zozote.


”Hii ni zaidi ya mara tatu, Mrema kushindwa kufika mahakamani wakati kesi yake inatajwa , ambapo kwa Lissu ni mara ya pili.
 
Wana JF
Mpaka leo nashindwa kuelewa maana ya hili neno "uchochezi". Can anyone please try to help me understand the meaning of this word. Sina idea hata kidogo ya mambo ya sheria, kila siku napata taabu kuelewa hasa wanaposema kuwa ametoa maneno ya uchochezi. Anani anayeamua kuwa haya ni maneno ya uchochezi, na ni maneno gani hasa yanatakiwa kuitwa uchochezi?
Kama kuna kipengele kama hiki kwenye sheria zetu, basi naona kinatoa nafasi ya kutuzuia tusiseme kitu kinatufanya tuogope kusema kwa sababu kitatufanya tuwe na hofu ya kuitwa wachochezi.
 
Back
Top Bottom