The difference between Toyota VVTI and D4 Engines

wakuu, one of the best of the best thread, nimejifunza mengi sana maana napenda sana haya masuala ya tech. na umeme in general..kuna nshkaji mmoja amepost apo juu issue ya mafuta yakiisha in D4 engine kuna wakati gari inaweza kumiss au kukataa kuwaka, jana exactly that hapened to me! i have brevis Ai250 na ilikua iko empty, nikaweka wese la 40, nimeenda kupaki, nawasha ngoma inagoma, fundi kuja akachomoa mawaya flani pale kwenye engine na kuchomeka, gari ikawaka! now what coulod be the problem? halafu wazee hii kitu inakula wese acha, any maujuzi on what to do ili niweze ku preserve kidogo ni save fuel? appreciated guys..
 
also mtaalam wa umeme,funguo original ya brevis ilivunjika, nikabadilisha na ku transfer ile mashine ya key to my new key, programed it and ikawa inawasha gari, but remote haifungi mpaka nifunge na kufungua kitasa manually, others wananiambia ni imobilizer problem, wengine wanasema mashine ile iliyowekwa sio yenyewe kwenye ufunguo, na inaboa kweli kila wakat kufungua kwa kuchomeka ufunguo kwenye kitasa, kuna utaalam wwote naweza kufanya au ndio ishakula kwangu, maana nlipeleka jamaa wa ku diagnose kwa mashine akachemka, alifanikiwa ku unprogram tu, akifika a certain point inagoma kufika asilimia 100...any help or advice will be ,much appreciated.
 
naomba nijue ulaji wa mafuta kati ya d4 na vvti, mafundi wengi wanasema d4 inakula sana mafuta naomba ufafanuzi
 
Kiongozi kila aina ya engine ina code yake.

Mfano,
Engine za vvti ndio zinakuwa na code ya 1G na cc zake zinakuwa mara nyingi hazizidi 2000
Angalia verrosa.

Engine za d4 zinakuwa na code ya JZ1 au 2,
Zenye 1Jz huwa na cc 2400
Zenye 2jz huwa na cc 2900
Angalia brevis na verrosa.

Engine nyengine zina code ya ya 3s,1az.

Ishu inakuja kwa mafundi wetu wa Kibongo ukimwambia akupe hizo tofauti inakuwa shida na ukitaka ushauri kutoka kwake atakwambia nunua 1G iwe kavu. Utaijuaje kavu, angalia bamba la nyuma utaona taa zake hazijaungana na buti. Basi inakuwa tafrani tu.

ha ha ha mkuu nimecheka sana apo iyo 1G kavu!!!! au kuna ile gari inaitwa carina tako la nyani!!!
 
also mtaalam wa umeme,funguo original ya brevis ilivunjika, nikabadilisha na ku transfer ile mashine ya key to my new key, programed it and ikawa inawasha gari, but remote haifungi mpaka nifunge na kufungua kitasa manually, others wananiambia ni imobilizer problem, wengine wanasema mashine ile iliyowekwa sio yenyewe kwenye ufunguo, na inaboa kweli kila wakat kufungua kwa kuchomeka ufunguo kwenye kitasa, kuna utaalam wwote naweza kufanya au ndio ishakula kwangu, maana nlipeleka jamaa wa ku diagnose kwa mashine akachemka, alifanikiwa ku unprogram tu, akifika a certain point inagoma kufika asilimia 100...any help or advice will be ,much appreciated.

Kama ulitumia those same electric internals za old key they zitakua zimeharibika tuu. Ila kama ni nzima kuna jinsi ya kuprogram remote keys za toyota, na unaweza fanya mwenyewe bila hata fundi.
 
Binafsi ninavyofahamu, engine nyingi kama sio zote za Toyota za kuanzia 1997 kuendelea ni VVTi, weather ni D4 au sio D4. Za kabla ya hapo zilikua only VVT. So the letter 'i' added stands for vvt with intelligence, or simply intelligent. Kwamba engine inaweza kutengeneza variation ya air and fuel intake kwa mahitaji tofauti tofauti ya engine, tofauti na vvt ambapo variation zilikua fixed muda wote.

D4 ni kwenye fuel injection kama wengi walivyosema. Ila D4 engine bado ni vvti pia, sema yenyewe ina direct fuel enjection. Kiukweli D4 ziko poa tu, actually zina advantages nyingi kuliko zisizo na direct fuel injection (port injection delivery) ila utafiti unaonesha D4 engine nyingi zina matatizo ya reliability hasa kwa nchi zenye baridi kali huwa inasumbua kuwaka at times, ina kelele za engine saana ikiwa silent na wakati mwingine inapoteza nguvu hasa ukiwa kwenye mwendo mdogo, ndio utasikia yale maneno kuwa engine bado haijachanganya vizuri. N chanzo kikubwa ni kwamba huwa inajaza carbon kwenye intake valves.

Lengo la hiyo teknologia ilikua kuboresha utumiaji wa mafuta, na kupunguza emission, but ukilinganisha na engine nyingine za Toyota, D4 zimeprove less reliable especially kama hauko makini saana hasa kwa kuweka mafuta yaliyochakachuliwa. Na problems za D4 engines huwa zinahitaji higher maintenance and repair costs kuliko engines zingine. Toyota wamelikubali hilo tatizo, na sasa hivi wame fix problems za d4 kwa kutengeneza engine nyingine wanaita D-4S.

Hi D-4S in advantages za both engines, so ukipata hii ni bora zaidi kuliko ile D4 ya kawaida.
 
naomba nijue ulaji wa mafuta kati ya d4 na vvti, mafundi wengi wanasema d4 inakula sana mafuta naomba ufafanuzi

mkuu sio kweli inaonekana wewe na hao mafundi bado hamjaelewa nini maana ya d4 na vvti.

ukishajua maana yake basi huwezi uliza swali hilo kamwe.
 
also mtaalam wa umeme,funguo original ya brevis ilivunjika, nikabadilisha na ku transfer ile mashine ya key to my new key, programed it and ikawa inawasha gari, but remote haifungi mpaka nifunge na kufungua kitasa manually, others wananiambia ni imobilizer problem, wengine wanasema mashine ile iliyowekwa sio yenyewe kwenye ufunguo, na inaboa kweli kila wakat kufungua kwa kuchomeka ufunguo kwenye kitasa, kuna utaalam wwote naweza kufanya au ndio ishakula kwangu, maana nlipeleka jamaa wa ku diagnose kwa mashine akachemka, alifanikiwa ku unprogram tu, akifika a certain point inagoma kufika asilimia 100...any help or advice will be ,much appreciated.

upo wapi mkuu kama hakuna kitu ambacho ulibadilisha inatakiwa ifanye kazi bila tatizo lolote lile kama upo dar upo pande zipi tufanye kazi hiyo??
 
mkuu sio kweli inaonekana wewe na hao mafundi bado hamjaelewa nini maana ya d4 na vvti.

ukishajua maana yake basi huwezi uliza swali hilo kamwe.

Naomba elimu mkuu
 
Kwa nchi yetu hii ya ujanja ujanja huwezi tegemea kituo kimoja tu cha mafuta katika uhai wa gari yako yeneye D4 engine. Uchakachuaji ni mwingi mno. ili kupunguza pressure kwa kukabiliana na hali hiyo ukijumlisha hatuna mafundi professional, nunua gari yenye kuweza kumudu hali mafuta yaliyochakachuliwa na mafundi wa miembeni. Achana na D4 utajilaumu. Nunua VVTi au 3S 4A 5A nk.
 
Ni kweli kabisa unayosema mkuu, mafundi wengi wa kibongo hawapo updated na teknolojia mpya. Mimi natumia Toyota Opa yenye engine ya D4 mwaka wa tatu sasa haijaniletea matatizo yeyote. Tatizo kubwa tu nililowahi kulipata ni kuwa gari ilikuwa inakataa kukaa sailensi kama kwenye foleni hivi ilikuwa ikizima, muda wote ilikuwa inataka lazima niwe ninakanyaga accelerator hivyo nikiwa kwenye foleni ilikuwa ikinilazimu niweke neutral ili niwe ninakanyaga accelerator.

Nikahangaika sana kwa mafundi wa mtaa wa lindi, mikocheni, maomeni na kwingineko, walikuwa wakibahatisha mara waninunulishe plug, nosel, fuel pump na vitu vingine bila mafanikio. Lakini baada ya kusearch kwenye mitandao yenye forums mbalimbali za magari nikaja kukuta kumbe watu wengi walipata tatizo kama hilo kwa engine ya aina hiyo na solution kumbe ni kubadilisha air cleaner. Fasta nikaenda pale msimbazi kituo cha bahresa nikanunua air cleaner... baada ya kuifunga mpaka leo tatizo lile likawa limetokomea.

Sasahivi gari yangu inakaribia km 100,000 za milage, nilishakuwa na corolla yenye engine ya 5A ambayo imeandikwa wazi kabisa kuwa ibadilishwe timing belt kila baada ya km 100,000. Sasa kwenye Opa yangu yenye D4 sijaona hayo maandishi wala sehemu yenye hiyo timing belt, sasa nauliza je hilo ya kubadilisha timing belt pia linaaply kwenye engine ya D4? pia naomba hapo kwa mafundi wako wanaofanya mainternance hizi kisomi hasa isiwe wale wa DT DOBIE na Toyota Tanzania ambao bei zao wanaoweza kuzimudu ni ma STK, SU na DFP

Sio kila Gari ina timing belt.
Kuna baadhi ya Magari yana timing chain na mengine yana timing gear.

Hayo ya timing belt ndio huwa yanaandikwa 100,000 km kabla ya kubadilisha.

Yale ya timing chain na gear huwa hayaandikwi chochote zaidi ya normal check wakati wa service au ikiisha check ingine light itakuonesha.
 
Kwa nchi yetu hii ya ujanja ujanja huwezi tegemea kituo kimoja tu cha mafuta katika uhai wa gari yako yeneye D4 engine. Uchakachuaji ni mwingi mno. ili kupunguza pressure kwa kukabiliana na hali hiyo ukijumlisha hatuna mafundi professional, nunua gari yenye kuweza kumudu hali mafuta yaliyochakachuliwa na mafundi wa miembeni. Achana na D4 utajilaumu. Nunua VVTi au 3S 4A 5A nk.

hahaha mkuu umeaua lakini huwezi ukimbia ukweli technologia ndio yaja huko hizo engine unazozitaja zinapotea kbs.

nanaona hata ww bado hujaelewa juu ya utofauti au maana ya vvti na d4.

kuna dawa flani zinauzwa kwajili ya kusafisha systerm ya mafuta ni nzuri sana watu wenye gari zinazotumia mfumo wa d4 Hata kama sio mfumo wa d4 ni nzuri sana ukawa baada ya mda fulani unanunua na kuitia kwenye tank la mafuta huwa inasafisha vizuri sana.

harafu nchi yetu naombea sana waanzishe ushuru wa kupima gas analyse.

sasa mkuu unaikimbia gari yenye mfumo wa d4 unategemea nn tena?? gari inatumia mafuta kidogo ,nguvu kubwa na ni rafiki wa mazingira.

kwa sababu hizo tatu tu hapo juu sijui kama utaeleweka ukisema gari ya d4 mbovu.

mbona kwenye maeneo mengine mmekubali kukubaliana na technologia inakokwenda??
acha kutumia hiyo simu now nunua nokia jeneza au ile philips ya mkonga .
 
Nini Tofauti ya mafuta haya Uleaded, super na petrol

jinsi ulivyo yataja ndivyo quality yake ilivyo kuna magari ya marekani na europe huko kwenye mfuniko wa tank utakuta umeandikiwa kabisa use gasoline only.

ukijaza mafuta mengine kama hiyo petrol hapo ni shidaa gari inaweza isiwake kabisa au ikiwaka ujue ni majanga kwa kwenda mbele miss haziishi na gari linaweza likashindwa kutembea kabisa.
au ikatembea ikawa haina performance nzuri.
 
Back
Top Bottom