The Citizen: JK alilishinikiza Bunge kumpa Zitto ulaji

Tumuombe zitto alitolee ufafanuzi hapa Jf kama ni kweli alimchokoza Rais kwa kumuomba msaada huo na pia atueleze ni kwa nini hivi sasa anaandamwa na kashfa kuliko wakati mwingine wowote. Hana budi kujitizama upya na mwendendo wake wa kisiasa. Mke wa mfalme hatuhumiwi na akitumiwa ni lazima aachike........ zitto ana sehemu ya lawama katika hili tukio kama kweli lilipangwa.
 
Tumuombe zitto alitolee ufafanuzi hapa Jf kama ni kweli alimchokoza Rais kwa kumuomba msaada huo na pia atueleze ni kwa nini hivi sasa anaandamwa na kashfa kuliko wakati mwingine wowote. Hana budi kujitizama upya na mwendendo wake wa kisiasa. Mke wa mfalme hatuhumiwi na akitumiwa ni lazima aachike........ zitto ana sehemu ya lawama katika hili tukio kama kweli lilipangwa.

kuna majibu ya juu juu ametoa...pitia post za nyuma utaona.......
 
Chadema wamuangalie sana Zitto. Huyu bwana ana urafiki na Familia ya JK na CCM kwa ujumla. Asije akaharibu chama. Mimi nafikiri hatakiwi kuwa na uongozi wowote ndani ya Chama.
 
jambo moja najiuliza, obvious jambo hili uongozi wa juu wa chadema unalijua. kwann hawachukui hatua dhidi ya Zitto? naliona halijakaa sawa kiasi flani lakini kwa kuwa viongozi wenyewe wako quite/wameona iko sawa tumwache Zubery apige kazi tukishirikiana nae bennet kwa kumkosoa atakapokuwa anaenda tofauti basii! otherwise kashakuwa mwenyekiti tayari, cdm wenyewe wametulia,pengine nao wanaujua mpango mzima.
 
Siwahi kuamini chochote aemacho Zitto, huyo ni mnafiki na ukitaka kujua ni bonge la ndumila kuwili, angalia alivyokuwa tofauti na misimamo ya chama chake.
 
I contested and won. I fought to win. I fought in 2008 and won and did the same in 2011.
Chuki, husuda na wivu ndio unakusumbua siku zote. Stay outside the box kaka! Don't please yourself by lying yourself.
I have mastered parliamentary politics and that made me win! Eti favour

Zitto, naamini kuwa ilikuwa vizuri na busara ulipata hiyo nafasi adimu ya uenyekiti. Umejibu vizuri jinsi unavyoelewa kuwa uliambiwa na wabubge wa ccm kuwa waliambiwa na Pinda kwamba kaagizwa na Rais wakuchgue wewe. Nadhani huna uhakika luwa kweli Rais aliagiza hivyo na kama alifanya hivyo ilipaswa ujue kuwa katumia madaraka yake vibaya na hivo kumvunjia heshima yake kwamba tuna raisi anayeweza kupindisha sheria kwa mapenzi yake tu. Huoni kuwa kama kiongozi umesaidia kumdhalilisha raisi I'll hali huna uhakika na ulisemalo? Mimi ningetegemea useme tu kuwa ulishinda, basi, na vipi ulishinda huelewi! Pia kuendelea kujibizana na members wote humu ndani inakupunguzia focus yako na kukufanya ujibu hata mambo ambayo hukutakiwa kujibu aidha kwa sababu ni non issue au ni hoja mbovu kupindukia ambazo hazitakiwi kujibiwa na MP kana wewe. Jifunze kutosheka na majibu yako ba kuacha kuandika kuwa oh hii ni chuki na husda nk ambavyo havikujengi badala yake unaonekana kama just another commoner.
 
Salaam,
Naomba nitumie nafasi hii kufafanua kuhusu habari ya gazeti la The Citizen.
Nyote mnafahamu kwamba mkutano wa pili wa Bunge la kumi ulikutana kwa ajili ya kuchagua wenyeviti wa Kamati za Bunge ili kupata Kamati ya Uongozi ya Bunge. Mimi niligombea uenyekiti wa kamati ya POAC kamati niliyokuwa nikiongoza toka Bunge la kumi.
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kamati za oversight ni kamati za Kambi rasmi ya upinzani Bungeni ambapo CHADEMA ilitimiza masharti yote ya kuwa kambi rasmi ya upinzani Bungeni.
Wabunge wa CCM kwa kushirikiana na CUF, NCCR na UDP waliamua kuikomoa chadema kwa kuinyima kamati hizi na hivyo kufanya tafsiri ya kanuni. Habari ambazo tulizipata ni kwamba kamati ya PAC ingekwenda kwa Cheyo, LAAC kwa Mrema na POAC kwa Hamad Rashid na hivyo chadema kutopata nafasi yeyote na kupunguza nguvu yake kwenye kamati ya uongozi ya Bunge ambayo hupanga ajenda za Bunge.
Mara baada ya kupata majina ya wajumbe 15 wa kamati ya POAC nilianza kampeni na msaidizi wangu kwenye kampeni alikuwa ni Mhe. Regia Mtema. Tuligawana wabunge ili kupata kura 8 ambazo zingehakikisha ushindi. Kati ya kura hizo nane, tatu ni zetu sisi wabunge wa CHADEMA-mimi, mhe Matiko na mhe Mtinda. Kwa hiyo nilikuwa natafuta kura 5 kutoka CCM.
Spika alipotangaza majina ya wajumbe jina la Hamad Rashid halikuwemo. CCM wakaitisha kikao cha caucus yao ili kufanya maamuzi juu wenyeviti wa kamati (walifanya hivyo hivyo wakati mimi na dokta Slaa tulipochaguliwa kuwa wenyeviti mwaka 2008).
Kikao chao kikaamua kwamba mwenyekiti awe Hamad Rashid, na kwa kuwa yeye sio mjumbe basi Spika amteue kuwa mjumbe. Kama Spika hatamteua basi mhe Amina Mwidau wa CUF achaguliwe. Wajumbe wa kamati ya POAC kutoka CCM wakapinga ndani ya kikao chao kwamba mimi ninafaa zaidi kuliko huyu mama wa CUF (ambaye mie wakati huu nilikuwa simfahamu kabisa). Wajumbe wote waliopinga uamuzi wa chama ninaambiwa walizomewa na hatimaye kuitwa jina mmoja kutamka kuwa watafuata uamuzi wa chama. Pinda ndiye aliongoza kikao hicho.Spika alipoambiwa abadili orodha yake na kumweka mhe Hamad Rashid, alikataa kwa hoja kwamba orodha imeshakuwa public na hawezi kuibadili. Akabakia mhe Mwidau kama mgombea ambaye CCM wanamtaka.
Wajumbe watano ambao walikuwa wamenihakikishia kura walimfuata Waziri Mkuu kumwambia kuwa wao wataenda kinyume na maamuzi ya chama na watanipigia kura. Usiku kucha wa siku ya kuamkia kupiga kura mimi na Regia tulizunguka kuhakikisha kura zetu zinabakia intact na hata kumshawishi Mbunge wa CUF Mwidau ajitoe.
Tukiwa tunajiandaa kwenda kwenye kupiga kura CCM wakaitwa kwa dharura na kuambiwa na Pinda kuwa uamuzi wa jana usiku umefutwa na Rais ameagiza achaguliwe Zitto.
Tukaenda kwenye uchaguzi, nikagombea na mhe Mwidau na nikapata kura 13 dhidi ya 2 za Mwidau.
Hiyo ndio background kwa ufupi.
Kwa hiyo, sikumpigia simu Rais kutaka anisaidie. Nimekaa bungeni miaka mitano na nazijua siasa za Bunge. Nilikuwa nimejipanga kiasi ambacho kushindwa kungetokea iwapo tu Chief Whip wa CCM angekuja kusimamia mwenyewe uchaguzi. Ikumbukwe pia mie nimekuwa student leader, najua siasa za kipiganaji. Inawezekana hata huyo mgombea angekuja kwenye mkutano baada ya kura kupigwa!
CCM walibadili msimamo baada ya kutishiwa strong rebellion from their own ranks that they will vote for me. Wabunge 5 wa CCM kati ya 11 kumwambia Pinda kuwa watanipa mimi kura ilikuwa ni ishara tosha kwamba wanaweza kuaoibika.
Pia inawezekana kabisa CCM walibadili msimamo asubuhi ili kutaka kudhoofisha hoja ya chadema kwamba mabadiliko ya kanuni yaliwalenga kwa kusema 'mbona Zitto kashinda'
Hayo ndio maelezo ninayoweza kuwapa ndugu zangu kuhusiana na suala hili. Kama kuna maswali zaidi nitawajibu kwa kadiri ya uwezo wangu.

Mwenendo wako kwa sasa unatutia mashaka. Unataka tuamini haya uliyoyaandika? Kivipi? Kama ni kweli kakanushe habari iliyoandikwa kwenye gazeti la "Citizen" toleo la jana. Kama wamekusingizia una haki ya kuwashtaki endapo hawatakanusha habari waliyoitoa jana kuhusu wewe. Vinginevyo, hapa pia umetufunga kamba za mgomba.
 
Wakati mwingine muwe mnapita kwenye blogu yangu Zitto na Demokrasia kwa maelezo ya mambo mengi kabla ya kukimbilia kwenye judgements.

Mwenendo wako na tabia yako ya kutoa lugha chafu hadharani unajitosheleza kutoa tafsiri ya u-mtu wa namna gani kwa sasa. Unataka kutuaminisha majisifu yako kwenye blogu yako? Unaweza ukajiandika kwa mabaya wewe mwenyewe? Kamwe haiwezekani. Umepoteza dira na mwelekeo kwa uchu wa madaraka na utajiri wa haraka haraka.
 
20 March 2011

Dar Es Salaam — President Jakaya Kikwete personally intervened to help Chadema secure the chairmanship of at least one of the 17 parliamentary committees and avoid a whitewash, as newfound allies CCM and CUF had teamed up in the National Assembly to lock out the vocal opposition party.


President Kikwete, sources told The Citizen on Sunday, influenced the re-election of Kigoma North MP Zitto Kabwe, as chairman of the Public Corporations Accounts Committee (POAC), despite the raging hostility between his own Chama Cha Mapinduzi (CCM) and Chadema.
Sources in Chadema and within the National Assembly confirmed that Mr Kabwe, a rabid critic of the government in the last Parliament, telephoned President Kikwete to seek his help in his last-ditch efforts to hold onto the position. He was then facing stiff opposition from hostile CCM lawmakers supported by the opposition Civic United Front (CUF), Tanzania Labour Party (TLP) and NCCR-Mageuzi MPs.
After speaking to Mr Kabwe, the President, who is also the CCM national chairman, reportedly directed Prime Minister Mizengo Pinda to rally support for the Chadema MP to head the POAC.
"Mr Pinda told the CCM lawmakers that the President wanted them to vote for Mr Kabwe," a Chadema MP, who asked not to be named, as he is not the party's spokesman, told The Citizen on Sunday this week.


However, the State House in Dar es Salaam, denied that President Kikwete had exerted pressure on the MPs or directed them on how to vote for the heads of the parliamentary committees that monitor and audit the Executive's performance.
Assistant Press Secretary to the President Premi Kibanga said he was not involved in choosing or endorsing the heads of the parliamentary committees. She said that was the MPs' role, in accordance with the parliamentary Standing Orders.
"The President is not involved in such business. Everything is done by the MPs themselves," said Ms Kibanga in a telephone interview this week, when asked about Mr Kabwe's alleged SoS phone call to the Head of State.
The Kigoma MP would himself not give anything away on his supposed lobbying of President Kikwete to personally intervene to secure him a second term as chairman of the POAC. Formed by the last Parliament, it has oversight over more than 100 public organisations and agencies that spend billions of taxpayers' funds every year.


"What I know is that the CCM had agreed to endorse the Wawi MP, Mr Hamad Rashid Mohammed, in their midnight meeting instead of me, but later in the morning, things changed and I was endorsed with 13 out of 15 votes," he said.
But reached for comment, Mr Mohammed dismissed the claim, saying he had no intention of challenging Mr Kabwe.
"I know nothing about that matter. I had wanted to vie for the Public Accounts Committee (PAC) chairmanship, but dropped the idea after Bariadi East MP John Cheyo said he would defend it," he said.
Speaking on the sidelines of the recent MPs' seminar at Ubungo Plaza in Dar es Salaam, Mr Kabwe could not confirm whether he spoke to President Kikwete on the issue. "I was sure of winning the post because I had already secured eight votes, which is the threshold, but I ended up getting 13, which was good," said Mr Kabwe.
He defeated CUF Nominated MP Amina Mwidau Mohammed. According to the parliamentary Standing Orders, MPs, who are members of a given parliamentary committee, elect one of them to chair the committee. With 10 seats, CCM has a majority of members of the POAC. Chadema and CUF have three and two, respectively.


It was not immediately clear if Mr Kabwe called the President in his personal capacity or as his party's deputy secretary general. Chadema national chairman Freeman Mbowe, and the secretary-general, Dr Willibrod Slaa, could not be reached for comment.
The Kigoma North MP has in the past rubbed his party the wrong way, with critics alleging covert links with some top CCM bigwigs, an accusation he has vehemently denied.
Before the February Bunge committee elections, Mr Kabwe had been taken to task by his party for staying away, when they resolved to stage a walkout during President Kikwete's State address to open the 10th Parliament.
The MP would later be quoted by a section of the media, as saying that he held the President in high esteem and could not show disrespect by boycotting his address to Parliament.
Emerging details show that CCM had, in reaction to the walkout, planned to use its numerical strength in the House to block Chadema, which succeeded CUF as the official opposition in Parliament after the 2010 General Election, from heading the committees. The ruling party was also ready to support MPs from other opposition parties other than Chadema, to win those positions.
An MP said the Speaker of the National Assembly, Ms Anne Makinda, had rooted for Ms Mohammed for the post, after her own efforts to persuade the MPs to back Mr Kabwe had failed.
"Ms Makinda had also warned that removing the Chadema MP would be unwise because he had shown credible performance in the 9th Parliament," said the MP, who requested for anonymity.
The MP, who comes from the Lake Zone, said a meeting in the night preceding the election had settled on the former leader of the Official Opposition, but the situation changed dramatically in the morning after the PM's word went around. We could not reach Mr Pinda or his aides for comment
 
Simjui Waberoya.
Ila kwa maandishi yake humu JF ni mtu mwenye kutenda haki. Pale ninapofanya vizuri ananipa credits. Pale ninapokosea ananikosoa.
Pale anapokuwa na hoja na hana majibu anauliza. Nadhani ndio mijadala ya wastaarabu inapaswa kuwa hivyo. Mijadala kutukanana, kuwa judged, kupeana majina mabaya, kujaza chuki haijengi spirit ya kujadiliana na kupata ufumbuzi wa matatizo yetu. Isipokuwa inafanya JF kuwa kijiwe kama vijiwe vingine vilivyojaa majungu, chuki, wivu na husuda.
Waberoya, toka tumeanza JF amejaribu kuweka mbele heshima ya jamvi na wanajamvi hili.

Siamini kama wewe ndiye unayeyasema haya! Hata siku tatu hazijapita! Kumbe unachukia kutukanana eehh! Nilikuwa sijui!
 
Kwa hiyo lolote linaloandikwa humu unaliamini? Nilimtaka Waberoya athibitishe madai yake ya kokote hakuweza. I also challenge you the same.
Jua kuna uwongo na uzusho mwingi sana humu JF. Jua kuna kuna kupakana matope sana humu. Ndio maana watu wanatumia majina bandia. Mimi natumia jina langu halisi tofauti na wewe, unaweza kusema lolote and go away with it.

Naona umeanza kuonesha vile ulivyo.
 
Mwenendo wako kwa sasa unatutia mashaka. Unataka tuamini haya uliyoyaandika? Kivipi? Kama ni kweli kakanushe habari iliyoandikwa kwenye gazeti la "Citizen" toleo la jana. Kama wamekusingizia una haki ya kuwashtaki endapo hawatakanusha habari waliyoitoa jana kuhusu wewe. Vinginevyo, hapa pia umetufunga kamba za mgomba.

Umeishiwa wivu wa kike!

Mwenendo wako na tabia yako ya kutoa lugha chafu hadharani unajitosheleza kutoa tafsiri ya u-mtu wa namna gani kwa sasa. Unataka kutuaminisha majisifu yako kwenye blogu yako? Unaweza ukajiandika kwa mabaya wewe mwenyewe? Kamwe haiwezekani. Umepoteza dira na mwelekeo kwa uchu wa madaraka na utajiri wa haraka haraka.

Kapoteza dira ipi? kapoteza umaarufu upi? hiyo ni wewe kwangu mimi Zito ni kiongozi mzuri sana, tena kwa vijana hakuna kama yeye.



... Na hii imekaaje wakuu:

Si kasema ukweli, unataka nini, semeni msemalo zito ni mkweli

Hivi kwa akili yako mtamfanya nini Zito, labda kama nyie ndiye wapiga kura wake!
 
I contested and won. I fought to win. I fought in 2008 and won and did the same in 2011.
Chuki, husuda na wivu ndio unakusumbua siku zote. Stay outside the box kaka! Don't please yourself by lying yourself.
I have mastered parliamentary politics and that made me win! Eti favour

Naona umeanza!

Sasa kama rais alipiga simu kuwa uchaguliwe wewe hali wana ccm wote akiwemo waziri mkuu chaguo lao lilikuwa mgombea wa cuf, huoni kuwa hiyo ni favor? Una agenda gani katika hilo?

Na tunaona sasa unapambana hata ikiwezekana kutukana watu matusi makubwa makubwa na kuwakashfu/kuwakejeli wengine ili uwaridhishe waliokupa ulaji. You are lost my friend.
 
mtu wa kumkataa kabisa asionekane chadema ni zito, hana maana.....msaliti hakuna mfano.
 
Back
Top Bottom