Kuna hii article nimeitoa kwenye Tanzania Daima laleo 25/07/07
Ukishangaa ya Balaliiiii utaona ya Ka-damage!
Mpayukaji Msemahovyo
WANAKAYA bado wanaulizia marekebisho ya mikataba ya kijambazi ya madini yao.
Hata kabla ya kupewa jibu la haja, mara wanaletewa msiba mwingine! Laiti angekuwa Mtume Paulo angesema: Nyinyi Wadanganyika wapumbavu nani aliwaroga kuwa mikataba imebadilishwa?
Wakati uchafu wa Bunch of Thieves (BoT) haujapoa tunaletewa tusi jingine kuwa Omulangila Nshomile Nazimia Kadamage ameishabadilisha mbinu ya kusaini mikataba ya madini.
Kweli waliposema wanabadilisha mikataba hatukujua kuwa kumbe wanabadilisha mbinu ya ulaji zaidi. Kweli wamebadilisha.
Badala ya kufanyia ufuska wao Bongo sasa wanaufanyia Ulaya!
Balaliiii naye katushangaza kuwa licha ya sisi kuwa tegemezi havunji genge lake la wezi! Mkuu naye utadhani hana madaraka na kaya yake!
Bwana Kipaza Sauti (Speaker) naye eti naye kavunja maadili ya kijiwe kumwokoa mhalifu wa kawaida! Yaani kaya hii tangu baba aondoke imeingiliwa!
Hayo ni mahojiano ya ndani kwa ndani wakati mzee mzima nikiangalia muuza kahawa anavyochanganya makemiko yake.
Maana leo nimejilawa baada ya mshirika wa bedroom kuunusa upepo wa shumbwengu langu la Migomigo. Si kitimoto hicho, yaani usiku kucha!
Mara nastuliwa na sauti ya mgosi Machungi. Mgosi mbona unafikiia sana utadhani unataka kusaini mikataba ya madini kue Andani kwa maikia!
Kufumba na kufumbua naona timu nzima imetia guu. Inaonekana hawa washirika wanatoka kuweka sigara kubwa.
Mara Mbwa Mwitu anadakia. Mgosi usinichafulie siku yangu kwa kunikumbusha hawa tumbiri. Yaani kaya imekuwa kama mfuko wa chizi kila kibaka kujichotea anavyotaka!
Makengeza naye alivyochangamka baada ya kulipuliza! Analamba mic. Wazee leo mada ni ujambazi wa wakubwa kwenye ofisi za umma. Wanaziuma huku ukapa ukituuma sisi umma!
Kumbe ndiyo maana wanatuita umma maana wanatuuma kweli kweli! Kweli sisi ni umma na wao ni waumma umma tena kwa uma na mrija!
Du, kijiwe hiki! Sina hamu. Utadhani wale Magiriki ambao Msomi huwa anatolea mifano! Mkuru anamtazama Msomi na kuendelea. Hebu Msomi nikumbushe majina ya wasomi hawa.
Msomi huku akitabasamu anaibusu mic. Yupo rafiki yangu kipenzi na msomi mwenzangu Socrates, Plato, Sophocles, Herakritos, Demakritos, Cicero, Cassenius Lucinius Luculus na mimi msomi mwenyewe, Mkata vimeo vya kaya hii, pia yu...
Kabla ya kuendelea kupayuka majina ya magwiji hawa, Makengeza anaingilia. Msomi imetosha. Maana Mukurusi, Demokrasihasi du! Kweli wenzetu mlivibukua vitabu!
Msomi anabwia kahawa yake maana tangu bajeti ianze kuuma hana jeuri ya kubwia tangawizi na vitumbua kama awali.
Anasema: Mimi, akina Slaa, Mbowe na wengine ndiyo wasomi ambao hatuko tayari kubakwa kisiasa ili tuibakishe nchi yetu. Kisa eti kuhongwa pesa chafu kama kwenye uchafu alioongelea Mgosi.
Mzee Kidevu naye analamba mic. Nyie hamjui. Mkuu aliposema mikataba ya akina Tuni tuni, Vigoda, Vyenge na Miramba na wenzao wengine hamkumuelewa.
Alimaanisha kwa kuiboresha na kusainiwa Ulaya tena kwa mama mwenyewe. Kweli Kamaragi kajua kututenda.
Du! Hii kubwa mzee Kidevu, alichomekea Mpiga picha Kapende.
Ni kweli kwa watu hawa hata kubomoa kwao ni kujenga. Hukusikia wakisema maisha bora kwa kaya yanawezekana tusijue wanamaanisha wao na washikaji zao!
Hujasikia wakitutia madole machoni wakisema eti kaya ni kama dege linalopaa wakati lilishabutuka na kuungua?
Msomi kashikwa pabaya. Anakatua mic tena. Mie naona huyu Nshomile angebadilisha jina na kujiita Ka-damage. Maana kama ni kusababisha damage (uharibifu) ameishaongeza mafuta kwenye moto. Je, hapa wa kulaumiwa ni nani?
Anajijibu mwenyewe. Hapa mkuu hatuna. Mie nshawambia siku nyingi kuwa kaya imegeuzwa gheto la wezi kujizolea.
Angekuwa ni mtu mwenye kuambilika ningemshauri amteue Katelefoni Mpenda kuchukia vyombo vya habari ili awakoromee wawekezaji. Au anakoromea vyombo vya habari kwa vile havimpi ten percent?
Sijui na wanaopinga ukeketaji wako wapi! Maana ukeketaji si wa mwili tu. Kuna ukeketaji wa kiakili ambao ni mbaya sana. Hakuna udhalilishaji kama kutaka maelezo yasiyokuwapo kisa uzushi na upuuzi wa kawaida!
Msomi umeongea kama Mukurusi, hatujakuelewa, analalamika mzee Maneno.
Msomi anavaa jezi tena. Hamkuona mzee Ruxa alivyochoka na huu usanii na hadi uvumilivu ukamshinda akaamua kuwapa live?
Kumbe kaya hii ni shamba la ngedere kujifunzia kuharibu mazao! Angalia Balalii. Angalia Mheshimiwa Richmond, mkuu hawagusi au ndiyo huo uswahiba?
Mzee Kidevu kanitoa tongo tongo. Kumbe wanaharamu hawa na matapeli ni sawa! Umma unauuma! Unaahidi Kanani kutaswaga kwenda Misri! Kurekebisha mikataba unabadili staili ya ulaji! Badala ya kupeana cha mbele hapa wanatumana kwenda kupeana walipotulangulia rada!
Hapa kaya itajipindua pamoja na kuwa na genge la mapinduzi ya umma. Anakatua kashata huku akijifuta jasho. Anabwia kidogo kahawa na kuendelea. Tangu kufa mzee, kaya hii imekumbwa na balaa la kusimamiwa na vibaka huku wakialikana na kuzidi kutusukumizia ulofa.
Halafu wapo wapuuzi sijui wamekatiwa! Eti wanasema Tuni tuni apewe nishani! Kama ni nishani ya umachinga sawa lakini si ya uadilifu.
Kama kuna nishani ya ulaji basi apewe Balaliiii.
Kabla ya kuendelea kutambaa naye Mbwa Mwitu anaanza upuuzi wake. Msomi samahani sikukuelewa. Umesema inaonekana akina Nshomile wamekatiwa nini? Maana nimesikia ukisema wanakwenda kwa mama ili waibake kaya. Hii ni salsafa ngumu.
Mbwa nawe acha ushamba. Ni falsafa siyo salsafa, Mzee Kidevu anaamua kumkosoa Mbwa Mwitu. Vicheko si kawaida hadi tunawasahau majambazi wetu kwa kitambo!
Mpemba naye kapata upenyo. Yakhe mie nshasema siku za nyuma. Hapa watu wasipoanka kama Pemba wataendelea lia lia weee huku hawa watu waendelea kujizolea mdebwedo.
Sie tuligoma tukafanya muafaka ingawa baadaye watu fulani tuwajua, wakauvuruga na Alhamdulillah wemebaki historia tena chaafu! Anapiga chafya na kuendelea.
Mie wallahi nawaapia masafu ya Mtume kama Wabara mtaendelea lala na lelemama hii bila kufahamu wallahi mtajajuta siku moja. Hapa lazima watu wajitokeze na kutukua haki yao. Vinginevo twafanyiwa usanii nasi twabweteka.
Mpayukaji nami napata mwanya isitoshe mahasira niliyo nayo kutokana na kulazwa kitimoto na mshirika wangu we acha tu. Naanza kutambaa. Je, wapinzani huwa wanaelewa somo? Wanangoja nini kuandaa maandamano na migomo ili tujue hii kaya ni mali ya nani.
Maana inavyoonekana kundi hili litakuja kutuuza halafu litimkie huko wanakoendea kutuchuuzia kwenye madangulo yao.
Tuuzwe mara ngapi mzee mzima? Anadakia mzee Maneno.
Mzee mwenzangu umenena. Kama kweli hii kaya ingekuwa yetu na wezi wetu wangeelewa na kukubali hivyo mtu kama Balaliii au Ka- Damage wangekuwa wameishatimuliwa na saa nyingine wangekuwa Ukonga wakitubia makosa yao.
Yaani tumezidiwa na Mu-7 ambaye tulimkomboa juzi tu ameweza kuwatia korokoroni majambazi waliojifanya marafiki zake.
Alijua asipofanya hivyo umma usiotaka kuumwa utaelewa kuwa ni washirika wake kama ambavyo kaya yetu imeanza kuamini kutokana na vibaka kupewa kila aina ya ulinzi huku wakitafutwa majambazi wa vijibenki kwani Benki Kuu siyo benki sawa na ile ya Mwanga au ni kwa vile uvunjaji umeanzia ndani kwa kutumia kalamu badala ya bunduki?
kijiwe kikiwa ndiyo kinanoga si lilipita Limousine la Balalaliiiii na ka-damage, tukaamka kulitupia mawe, likatimua mbio!
Mpayukaji@yahoo.com