The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Zitto aliwasilisha vizuri hoja yake nzito yenye vipengele muhimu kumi na moja. Karamagi akajibu kipengele kimoja baada ya kingine (kwa vijembe huku akinukuu vifungu mbalimbali vya sheria za madini na mapato alivyovitumia Zitto, akieleza jinsi Zitto alivyovitumia kulipotosha bunge). Na hapo ndipo alipowapiga bao wengi waliokuwa wanafuata mkumbo.

Kilichotokea ni kwamba majibu ya Karamagi yakawachanganya waliokuwa wamejiandaa kuunga mkono hoja kiasi kwamba wakabaki kuchanganyikiwa wakati wa kuchangia. Kungekuwa na uwezekano wa kujitoa, leo hii wabunge wengi wangemwomba spika aondoe majina yao. Hakuna mbunge hata mmoja aliyeweza kuoanisha hoja za Zitto na majibu ya Karamagi. Inaonyesha walikuwa wamekariri majibu, sasa baada ya Karamagi kumchambua Zitto wakabaki kujiumauma kiasi cha kufikia hatua ya kumwombea msamaha Zitto kwamba alikuwa anahitaji kueleweshwa (Maulida Komu). Wengine wakaanza kusoma vifungu vya Katiba vinavyompa mbunge kinga ya kutoshtakiwa kutokana na atakayochangia bungeni kana kwamba walishaamua kwamba Zitto kadanganya. .. walichanganyikiwa kweli kweli.

Hoja ikabadilishwa ikawa kwamba Kamati Teule iundwe ili kusafisha jina la Karamagi lililochafuliwa na tuhuma hizo. Hapo ndipo nikachoka kabisa. Aliyefurahisha zaidi ni Chacha Wangwe maana hakujua hata anachangia hoja ipi. Leo kwa kweli ilikuwa ni vichekesho tu bungeni.

Leo Karamagi nami kanishangaza manake huwa hajui Kiswahili fasaha lakini leo kakomaa...na kum-reduce Zitto to almost nothing. Kachambua kipengele kimoja baada ya kingine, kwa data na kwa kujiamini. Kila mtu kaona kwamba Zitto alisema uongo ili kutaka umaarufu. Bado nadhani kumfungia sio jawabu, mimi nadhani ile aibu ya kwamba kadanganya, katoa data za uongo ingetosha (ingawa huyu bwana hana uso wa haya hata anapogundulika kasema uongo).

Kama alivyosema Maulida Komu, Mbunge mwenzake wa CHADEMA, anachohitaji Zitto ni kueleweshwa (ingawa shida yake ni kujifanya mjuaji).
 
"mimi nadhani ile aibu ya kwamba kadanganya, katoa data za uongo ingetosha (ingawa huyu bwana hana uso wa haya hata anapogundulika kasema uongo)."

this one sounds familiar.. labda na wewe tukuonee huruma tu kuwa huwezi kukiri kukosea isipokuwa ile "aibu" inatosha.
 
Ndani ya Habari za TVT leo hii dakika kama 30 zilizopita nimepata mshtuko baada ya kuona wakitangaza kusimamishwa kuhudhuria na kushiriki vikao vya Bunge Mhe. Kabwe Zitto mpaka Januari kwa Madai ya kuudanganya Umma nafikiri kuhusiana na Masuala ya Madini na hivyo Mhe. Mudhihir Mudhihir kulingana na kipengele namba..... kinamruhusu MB kuomba kutolewa adhabu kali kwa Mbunge mwingine kama ikibainika amedanganya Umma.

Habari zaidi Kesho!

Uwe unasoma kwanza kabla ya kupost. Hiyo habari imeshajadiliwa sana kwenye thread nyingine.
 
1. Zito na Mugongo nani muongo?
2. Zito na Mugongo nani anajifanya mjuaji?
3. Zito na Mugongo nani mtetezi wa wabadhirifu?

Afande Sele yuko wapi atuimbie tungo hii?

Kumbe niko ligi moja na Zitto? Mie nilijua Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mugongo Mugongo is some anonymous lunatic in the net.
 
Wanamfungia Zitto kwa kosa gani? Tatizo letu ni sisi wananchi
ambao hatuwawajibishi wabunge wajinga na wanaotetea ujinga huko bungeni.

Hivi suala la madini, kweli Zitto ndio anatakiwa kufungiwa?
 
Hivi nani alisema yana mwisho haya.....hivi vicheko vilivyojaa bashasha na mikogo....

Mungu atupe uhai tuuone huo mwisho.....kwa salama

Tanzanianjema
 
Kumbe niko ligi moja na Zitto? Mie nilijua Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mugongo Mugongo is some anonymous lunatic in the net.

Kuna mtu anamwamini Mugongo? Basi ataamini kile anachaondika. Je, yule asiyemwamini? Hataamini anachoandika. Mimi nawamini Mugongo.

Anajitambulisha kwetu kama Mugongo the lunatic. So, this is Mugongo. What a name! Au kuna mtu kamwandikia posting hii?
 
Muongomuongo,

Why hizo scripts while tunaona edited/live hapa?

Kwa kuwa unajua kuwa Karamagi ana timu ya watu kama ninyi kwa mamia na pamoja na umiliki wa huo mkataba unaongelewa hapa ambao anadai hauna hitilafu na wakati huohuo hayupo tayari kumpa Zitto ili kujenga kesi yake.

Tuhuma zinapanguliwa kwa majibu na sio vithibitisho ambavyo Mbunge amenyimwa lakini Waziri aliyenavyo hayupo tayar kuvitoa.

Kaka kama wewe upo hapa for Irresponsible endeavors tupo ambao tunatumia muda wetu hapa for responsible causes...

Hebu msikilize Field Marshall Chacha Wangwe hapo..

Tanzanianinjema
 
Kuna mtu anamwamini Mugongo? Basi ataamini kile anachaondika. Je, yule asiyemwamini? Hataamini anachoandika. Mimi nawamini Mugongo.

Anajitambulisha kwetu kama Mugongo the lunatic. So, this is Mugongo. What a name! Au kuna mtu kamwandikia posting hii?

That is deep, philosophical, stuff right there.
 
Nadhani haya madai ya kusema "kamwe serikali isingeweza kuacha nafasi hiyo ipotee bure na ndiyo maana ikasaini mkataba huo mapema Februari kabla ya tarehe ya mwisho ya Machi mwaka huu" yanahitaji ufafanuzi.

  • Je serikali ndiyo iliyowaomba wawekezaji hawa, ambao waliweka masharti kuwa watawekeza tu ikiwa mkataba utasainiwa kabla ya mwisho wa Machi?
  • Lakini si wawekezaji wenyewe ni Barrick Gold Mines ambao wapo nchini tayari na walikuwa wanajua kuwa serikali inapitia upya taratibu za mikataba, nao walitaka waingie mkataba huo katika katika utaratibu wa zamani? Je hamuoni kuwa hata hii effort ya serikali "kuwashawishi" wawekezaji hawa kubadilisha vipengere kadhaa vya mikataba hiyo itapiga mwamba?
  • Kwa nini ripoti ya mazingira haikutiliwa maanani? Je wakati wa uchimbaji ikigundulika kuwa mradi huo ni hatari kwa mazingira serikali itasemaje wakati imeshainingia mkataba?

Je kama ripoti za mazingira zitaionyesha kuwa uchimaji huo utaharibu mazingira, serikali itafanya nini huku ikiwa imeshaingia mkataba?

..haya maswali yako hayana majibu sahihi!

..sababu hii issue ishakuwa siasa tayari!

..mwana si rizki tena huyu!
 
Wanamfungia Zitto kwa kosa gani? Tatizo letu ni sisi wananchi
ambao hatuwawajibishi wabunge wajinga na wanaotetea ujinga huko bungeni.

Hivi suala la madini, kweli Zitto ndio anatakiwa kufungiwa?

hii ndio ccm wanafanya as if wao pekee ndio wenye hati miliki ya nchi hii..hatutafika na hii nidhamu ya kichama wapinzani hata wakipeleka hoja muhimu kama hii wanafukuzwa na kupingwa tu kwa kuwa ni wapinzani...hatutafika!!! hatutafika!! hatutafika!!!.......wabunge wa ccm wako pale kutetea uzandiki tu.....tuongeze idadi ya wapinzani bungeni ..hata kama wewe ni mwana ccm makini itabidi ukubali haja ya upinzani wenye nguvu.....ameadhibiwa ili kukatisha juhudi za wapinzani kuleta hoja.....nafikiri ni bora wapinzani wote nao wakaungana na zitto ku walk out kwa hizo siku mbili ili na dunia ijue...........bunge limetekwa ..sio muhimili tena!!!!!!!!!!!!

nina hasira sana!!!!!!
 
Wewe, acha kutumia exclamation marks nyingi kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom