The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Huyu Mswahili Mdhihiri Mdhihiri ni mnafiki tu!,anajua tosha kuwa kabebwa kufikia hapo alipo,alipandishwa kiajabu ajabu kutoka kwenye Street Red Line, Ulinzi wa Viongozi hadi kwenye Uwaziri,na hata huo Ubunge wa Mchinga anaupata kwa migongo ya wapambe wake!Hana haki kuomba kusimamishwa Ubunge kwa Zitto!,inabidi tuwe serious sasa!!!!,

Unategemea mchango gani kwa mwana mipasho wa vidole juu by proffesion....

Tutafika lakini safari ya peponi haiwezi kuwa rahisi kama tungelipenda iwe...

Tanzanianjema
 
Duh!! wamemfungia, Kwani huo mkataba ulisainiwa ama haukusainiwa? au ndio mambo ya nani ameshikilia mpini?
 
Leo sisemi kitu ila ni aibu tupu kwa TAIFA LETU.... WATANZANIA WATATUSHANGAA SANA

..kama wamezoea kuona wazungu wakipita kwenye 4*4 zao kuelekea kuchuma shambani kwao!

..wakiruka na ndege kwenye anga yao kuangalia shambani mwao mna nini ili wachukue!

..wameshazoe kuwahudumia wazungu kwa fedha walizozichuma kwa migongo yao wenyewe!

..wameshazoe kuishi kimungumungu!wasijue kesho kuna nini!

..washauzoe umasikini na kuukubali!

..watashangaa kitu gani!

..tushukuru hewa tunayovuta hamna anayewekeza na kufaidika nayo ama sivyo tungekufa wengi!
 
Ndg Icadon,
Mkataba umesainiwa na Ushahidi upo!,Mh.Zitto atakuja hapa nae atasema wazi nini kilichotokea huko Bungeni,Ikiwa ataingia hapa tujadili nini kimemleta, na sio kuuliza Vinginevyo! na kutaka kudhalilishana,tutoe nafasi ya kujadili masuala ya maana kwa jamii na sio kuwa kijiwe cha kujadili masuala binafsi!.Zitto pekee ndio mtu anayeweza kutupa ukweli kuhusu suala zima la Karamagi!!.Mh.Tuanaomba maelezo yako hapa.
 
Leo sisemi kitu ila ni aibu tupu kwa TAIFA LETU.... WATANZANIA WATATUSHANGAA SANA
 
Nashauri Zitto achukue muda wake kabla ya kujitosa katika bahari hii iliyojaa mamba na kenge kuzidi hata ule mtandao wetu...

Take your time kaka usije na ghadhabu zako hapa ukawapa watu faida...

Tanzanianjema
 
Mpaka hapo ZITO shujaa.Siku zote tunasema wabunge wa chama cha wenyewe sio wawakilishi wa waTz bali wa wao wenyewe.SHAME
 
Ndg Icadon,
Mkataba umesainiwa na Ushahidi upo!,Mh.Zitto atakuja hapa nae atasema wazi nini kilichotokea huko Bungeni,Ikiwa ataingia hapa tujadili nini kimemleta, na sio kuuliza Vinginevyo! na kutaka kudhalilishana,tutoe nafasi ya kujadili masuala ya maana kwa jamii na sio kuwa kijiwe cha kujadili masuala binafsi!.Zitto pekee ndio mtu anayeweza kutupa ukweli kuhusu suala zima la Karamagi!!.Mh.Tuanaomba maelezo yako hapa.

kwa hiyo mwendo ni mabavu na kuonyesha who is the boss sio? ebwanae maslahi ya Taifa naona hayawekwi mbele kabisa siku hizi, alafu viongozi watajiuliza kwa nini watu wanapoteza Uzalendo taratibu?
 
Ndani ya Habari za TVT leo hii dakika kama 30 zilizopita nimepata mshtuko baada ya kuona wakitangaza kusimamishwa kuhudhuria na kushiriki vikao vya Bunge Mhe. Kabwe Zitto mpaka Januari kwa Madai ya kuudanganya Umma nafikiri kuhusiana na Masuala ya Madini na hivyo Mhe. Mudhihir Mudhihir kulingana na kipengele namba..... kinamruhusu MB kuomba kutolewa adhabu kali kwa Mbunge mwingine kama ikibainika amedanganya Umma.

Habari zaidi Kesho!
 
Ndio tatizo la kukurupuka. Siku Zitto alipomtuhumu Karamagi na kuahidi kuleta hoja binafsi...ndio akawa amejifunga kitanzi. Baada ya kutoa hoja ndio akaanza research...iliyo-lead kwenye ukweli kwamba alikurupuka...kuna wakati alikwishaamua asiwasilishe hoja hiyo baada ya kukosa data. Lakini kwakuwa aliahidi kwa mbwembwe hakukuwa na njia zaidi ya kuwasilisha hoja dhaifu....baada ya Karamagi kujibu, ikaonekana kwamba huyu Mheshimiwa aliongopa na wenzake sasa ndio wanamtwanga kwa hoja ya kusimamishwa Ubunge kwa kusema uongo. Hata hivyo, mimi nadhani ni hoja ya kipuuzi ya kutaka asimamishwe Ubunge. Mimi nadhani wamuache aumbuke na uongo wake manake hii ni tabia yake ya kusema uongo kutafuta umaarufu.


huju Mheshimiwa hata kama kakurukupa bado hawajathibitisha kuwa kasema uongo kwani madai yake hayajafanyiwa kazi, hapa ni kasumba ya kufata mkondo wa maji, nani kasema nini na ni mambo ya kichama zaidi. mheshimiwa Zitto amekuwa shujaa kwani hata alipoombwa kusema kama ana with draw statement yake akasema yeye ni mwanademokrasia na anaomba Bunge limjadili na kumpa adhabu kama kweli amesema uongo. Lakini still ukweli bado upo pale pale maamuzi haya kwa uono wangu ni ya kuzima moto kwani hawajathibitisha kama kasema uongo.
 
Star TV wamerekodi wataanza kuonyesha kuanzia saa nne usiku
 
Hoja kuchunguza mkataba Buzwagi yatibua Bunge

*Waziri, Mbunge watunishiana misuli
*Hoja yageuzwa ya kisiasa
*Wabunge wengine wavutana
*Baadhi watishiana, wengine walalama


Na Ndyesumbilai Florian, Dodoma


HOJA binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) kuhusu utaratibu uliotumiwa na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kusaini haraka mkataba wa mradi wa madini wa Buzwagi, Wilayani Kahama, umeligeuza Bunge kuwa kikao cha mapambano ya kiitikadi na kupunguza uzito wa hoja na mjadala wenyewe.

Kinyume na ilivyotarajiwa na wengi, hatma ya hoja hiyo ilionyesha zaidi kufuatiwa na kurushiana vijembe na kejeli kutoka miongoni mwa wabunge wa chama tawala, CCM dhidi ya wale wa upinzani ambao kwa kiasi kikubwa walionekana dhaifu, kushindwa kuhimili vishindo, hususan katika kujibu mapigo ya Waziri Karamagi dhidi ya hoja ya msingi ya Kabwe.

Matokeo yake, karibu kila mchangiaji aliyesimama, alikuwa akionyesha kuegemea zaidi kwenye itikadi au fungamano la kambi yake kisiasa, kuliko uzito wa hoja hiyo iliyoibuliwa na kujengwa na mwanasiasa huyo kijana, hasa ile inayohusu matatizo kuhusu mikataba katika sekta ya madini na sheria zinazosimamia sekta hiyo.

Akiwasilisha hoja hiyo, Kabwe alilitaka Bunge likubali kuunda kamati hiyo teule ili kuchunguza mwenendo mzima wa kusainiwa kwa mradi huo kulikofanyika jijini London, Uingereza Februari mwaka huu. Alidai kuwapo kwa ukiukwaji katika baadhi ya taratibu zinazosimamia, kuongoza sekta ya madini nchini.

Miongoni mwake ilikuwa ni haraka iliyomfanya Waziri Karamagi ausaini mkataba huo akiwa nje ya nchi bila kusubiri kwanza ripoti ya tathmini ya athari kwa mazingira (EIA) kuhusiana na mradi huo ambazo kwa kawaida hutolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (Nemc).

Katika hoja yake yenye vipengele 11, Kabwe alitaka kamati hiyo iundwe kwa lengo la kujiridhisha na kuondoa utata huo ambao alidai umejitokeza zaidi na kugubika mchakato mzima wa kusainiwa kwa mkataba huo, akidai kuwa ilikuwa kinyume na Sheria ya Madini ya mwaka 1998.

Pia, alihoji sababu za kuendelea kuiita miradi wakati Kampuni ya Barrick imewekeza mtaji mkubwa katika mradi huo, kiasi cha dola za Kimarekani milioni 400, ikiwa ndio mradi mkubwa wa pili baada ya ule wa Bulyankhulu, pia ulioko Kahama, ambao umewekezwa dola milioni 600 na kampuni hiyo.

Hata hivyo, aliposimama, Waziri Karamagi alianza kuzipangua hoja hizo moja baada ya nyingine, huku akishangiliwa kwa makofi na wabunge wa CCM.

Kama vile hiyo haitoshi, Karamagi alionyesha dhahiri kukejeli hoja za Kabwe kuwa hazikuwa na msingi na zaidi zilitokana na ukosefu wa uelewa wa masuala yanayosimamia sekta ya madini na kuongeza kuwa hakukuwa na uvunjaji wowote wa sheria za nchi.

Badala yake, alisema alichokifanya akiwa katika ziara ya kikazi ya muda mrefu nje ya nchi, ni kupata habari kuhusu kuwapo kwa nafasi ya uwekezaji katika mradi huo wa madini na hivyo kuichangamkia.

Alisema alichoshindwa kuelewa Kabwe ni kushindwa kutofautisha na kisha kuchanganya sheria zinazohusu utafutaji na uwekezaji katika madini na uchimbaji halisi.

Aliongeza kuwa hilo ndilo limemfanya afikirie suala la EIA kwa mradi wa Buzwagi, ambalo kwa kawaida huwagusa zaidi wachimbaji ambao tayari wamepewa leseni za uchimbaji katika migodi ya madini na siyo wale wanaoendelea na uwekezaji kama ilivyo kwa kampuni ya Barrick kupitia mradi wa Buzwagi.

Kwa maana hiyo, Karamagi alieleza kuwa hakukuwa na sababu ya kuhitaji kwanza ripoti hiyo ambayo itafikiwa wakati wawekezaji hao watakapoanza shughuli rasmi za uchimbaji wa dhahabu katika mgodi huo.

Kuhusu manufaa ambayo Watanzania wataweza kupata kutokana na mradi huo, Karamagi alieleza kuwa ni kupatikana kwa ajira zaidi ya 600 kwa Watanzania, zikiwamo zile za maafisa wa vyeo vya juu.


Aliongeza kuwa mradi huo utaweza kuwekeza kiasi cha zaidi ya dola milioni 800 baada ya kukamilisha uwekezaji wake na kuongeza kuwa kamwe serikali isingeweza kuacha nafasi hiyo ipotee bure na ndiyo maana ikasaini mkataba huo mapema Februari kabla ya tarehe ya mwisho ya Machi mwaka huu.

Karamagi ambaye alizipangua hoja za Kabwe kwa umakini mkubwa, hatimaye alionyesha kuteleza na kutumbukia katika mtego wa kiitikadi alipodai kuwa hoja hiyo iliibuliwa na Kabwe na sasa imechukuliwa kama ajenda na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, anayeipigia debe majukwaani huku akivishambulia vyombo vya habari kuwa vimetumika kumchafua na kumpaka matope.


Wakichangia hoja hiyo, wabunge wa kambi ya upinzani, Khalifa Suleiman Khalifa (Gando-CUF), Mhonga Ruhwanya (Viti Maalum-Chadema), Chacha Wangwe (Tarime-Chadema), Maulida Anna Kome (Viti Maalum-Chadema) na Margareth Sakaya (Viti Maalum- CUF), wao waliunga mkono hoja ya kuundwa kwa kamati hiyo.


Hata hivyo, alikuwa Komu aliyewaacha hoi wabunge kwa kudai kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere pekee, ndiye anayeweza kukemea mambo yanayoendeshwa na serikali ya CCM ikiwamo wizi na ubadhirifu wa rasilmali za umma, yakiwamo madini.


Waliochangia kwa upande wa CCM, walikuwa Ruth Msafiri (Muleba Kaskazini-CCM), Suleiman Kumchaya (Lulindi), Adam Malima (Mkuranga), ambao walionyesha dhahiri kuungana na msimamo wa serikali na hata kuwabeza wapinzani.

Nadhani haya madai ya kusema "kamwe serikali isingeweza kuacha nafasi hiyo ipotee bure na ndiyo maana ikasaini mkataba huo mapema Februari kabla ya tarehe ya mwisho ya Machi mwaka huu" yanahitaji ufafanuzi.

  • Je serikali ndiyo iliyowaomba wawekezaji hawa, ambao waliweka masharti kuwa watawekeza tu ikiwa mkataba utasainiwa kabla ya mwisho wa Machi?
  • Lakini si wawekezaji wenyewe ni Barrick Gold Mines ambao wapo nchini tayari na walikuwa wanajua kuwa serikali inapitia upya taratibu za mikataba, nao walitaka waingie mkataba huo katika katika utaratibu wa zamani? Je hamuoni kuwa hata hii effort ya serikali "kuwashawishi" wawekezaji hawa kubadilisha vipengere kadhaa vya mikataba hiyo itapiga mwamba?
  • Kwa nini ripoti ya mazingira haikutiliwa maanani? Je wakati wa uchimbaji ikigundulika kuwa mradi huo ni hatari kwa mazingira serikali itasemaje wakati imeshainingia mkataba?

Je kama ripoti za mazingira zitaionyesha kuwa uchimaji huo utaharibu mazingira, serikali itafanya nini huku ikiwa imeshaingia mkataba?
 
Star TV wamerekodi wataanza kuonyesha kuanzia saa nne usiku
 
najitahidi kutafuta ile connection ya bure StarTv siipati...mwanakijiji naomba msaada wako..
 
Zitto aliwasilisha vizuri hoja yake nzito yenye vipengele muhimu kumi na moja. Karamagi akajibu kipengele kimoja baada ya kingine (kwa vijembe huku akinukuu vifungu mbalimbali vya sheria za madini na mapato alivyovitumia Zitto, akieleza jinsi Zitto alivyovitumia kulipotosha bunge). Na hapo ndipo alipowapiga bao wengi waliokuwa wanafuata mkumbo.

Kilichotokea ni kwamba majibu ya Karamagi yakawachanganya waliokuwa wamejiandaa kuunga mkono hoja kiasi kwamba wakabaki kuchanganyikiwa wakati wa kuchangia. Kungekuwa na uwezekano wa kujitoa, leo hii wabunge wengi wangemwomba spika aondoe majina yao. Hakuna mbunge hata mmoja aliyeweza kuoanisha hoja za Zitto na majibu ya Karamagi. Inaonyesha walikuwa wamekariri majibu, sasa baada ya Karamagi kumchambua Zitto wakabaki kujiumauma kiasi cha kufikia hatua ya kumwombea msamaha Zitto kwamba alikuwa anahitaji kueleweshwa (Maulida Komu). Wengine wakaanza kusoma vifungu vya Katiba vinavyompa mbunge kinga ya kutoshtakiwa kutokana na atakayochangia bungeni kana kwamba walishaamua kwamba Zitto kadanganya. .. walichanganyikiwa kweli kweli.

Hoja ikabadilishwa ikawa kwamba Kamati Teule iundwe ili kusafisha jina la Karamagi lililochafuliwa na tuhuma hizo. Hapo ndipo nikachoka kabisa. Aliyefurahisha zaidi ni Chacha Wangwe maana hakujua hata anachangia hoja ipi. Leo kwa kweli ilikuwa ni vichekesho tu bungeni.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom