Thamani ya gwanda la chadema hii hapa

Mi ninachotaka watengeneze mengi lakini siyo kwa bei ya 75,000/= ni kubwa sana na ndiyo maana wanachama wengi hawana hili gwanda pia wengine ukiwakuta wamevaa basi ni shati lake tu chini jeans.Naanza kupata wasiwasi inawezekana wanafanya mtindo wa kugawana wanachanga pesa halafu mmoja anadaka suruali mwingine shati sasa hii ndiyo nini.Punguzeni bei bana watu wayanunue.Ni aibu wale vijana wamezunguka mkutano mzima lakini Gwanda hazikununuliwa.

we kama bei imekushinda nenda kangoje za magamba
 
Mkuu, mi hata sikioni kilichokufanya uje kulia hapa.
Kwanza, kuwa mwanachama wa chadema, nadhani, siyo lazima uvae gwanda.
Pili, hata kuvaa gwanda peke yake hakukufanyi automatically kuwa mwanachama mzuri wa chadema. Unaweza kuwa mwananchama mzuri bila kuvaa gwanda. Ingawa kuvaa gwanda ni vizuri zaidi maana unachangia pia pesa kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za chama chenu.
Tatu, kama unaona magwanda yao ni ghali mno, unaweza kwenda 'kule kwingine' ambako unapata kofia na tshirt bure, na ubwabwa juu!
 
Hapa hapa ndiyo eneo sahihi ya kusema jambo kama hili huwezi kusema wananchi wamepigika lakini bado we unauza sare kwa bei kubwa ya 75,000/=Nafikiri hata wewe uliooona thread hii umestuka na ndiyo maana umeamua kucomment kwa sababu bila kutetea hii hoja utaonekana ushabikii chama chako vizuri shida yako akili yako umeikalia kwa kutumia tofali.
Asante mkuu, nilidhani utakuwa kwenye sura ya kwanza kwa nilichokiandika lakini mpaka sasa najua upo upande wa pili wa nilichokiandika, nashukuru mkuu na umeeleweka kwa hiki ulichonijibu
 
Mkuu, mi hata sikioni kilichokufanya uje kulia hapa.
Kwanza, kuwa mwanachama wa chadema, nadhani, siyo lazima uvae gwanda.
Pili, hata kuvaa gwanda peke yake hakukufanyi automatically kuwa mwanachama mzuri wa chadema. Unaweza kuwa mwananchama mzuri bila kuvaa gwanda. Ingawa kuvaa gwanda ni vizuri zaidi maana unachangia pia pesa kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za chama chenu.
Tatu, kama unaona magwanda yao ni ghali mno, unaweza kwenda 'kule kwingine' ambako unapata kofia na tshirt bure, na ubwabwa juu!
Hapa kwenye red pamenivunja mbavu kweli, haya ndo matatizo ya watanzania wengi, hawapendi kupanda, wao kila kitu wanata iwe mtelemko tu
 
Si lazima kuvaa gwanda, na Bei itakua imekua hivo kwa ajili ya gharama za ushonaji na material!!
 
Picha ile haitawaondoka wana Singida, mauaji yale ni kinyama haijapata kutokea. Tunashukuru wauaji wanaendelea kukabiliana na mkono wa sheria japo walioagiza mauaji haya wanaendelea kutembelea magari yenye AC
Mauaji ya singida yamefikaje tena hapa kwenye hii thread mkuu
 
Shati moja la kijani la magamba ni sh.50000 na zaidi,full gwanda toka juu mpaka chini ni sh.75000,chagua hapo,wapi nafuu.
 
Shati moja la kijani la magamba ni sh.50000 na zaidi,full gwanda toka juu mpaka chini ni sh.75000,chagua hapo,wapi nafuu.

Mleta mada hajanishawishi bado. Angekuja na bei ya kitambaa kinachotosha full gwanda (shati na suruali), gharama ya mashono, halafu tukafanya hesabu za kujumlisha. Jibu tutakalopata ndio lingetusaidia kujadili vizuri maana hapa hatuna base. Labda kama mantiki yake ni gwanda liuzwe bei chee bila kuzingatia input cost.
 
Katika hali ambayo sikuwa najua lakini leo hii baada ya viongozi wa BAVICHA kuwasili hapa kwetu Mpanda Mjini nilivutiwa sana na Gwanda.Sikuishia kulitazama bali ilinibidi niulizie namna ya kulipata ndipo niliwauliza vijana waliokuwa wanayatembeza pale mkutanoni lakini nilistushwa na thamani ya lile Gwanda kumbe huwezi kulipata bila kuwa na TSHS 75,000/= sabini na tano elfu sasa nikajiuliza inakuwaje wanasema WaTZ tumepigika halafu Gwanda liuzwe kwa bei kubwa kiasi hiki.Kweli hapo kuna dhamira ya kututoa kwenye umasikini?Muungwana vitendo!!!!!

kwanza, hawashoni kama chama, ni wewe mwenyewe na fundi wako, au anayeuza anaangalia ametumia sh. ngapi. hapo chama hakihusiki, na wala siyo mradi wa chama. kwa kuwa limependwa, watu wanatumia fursa hiyo kujitengenezea shekeli kidogo.

hata wewe ukipenda unaweza kuanza kulitengeneza, na kuwauzia watu. lakini kwa jinsi lilvyo complicated, inaweza kukugharimu 50,000 mpaka 70,000/- itategemea na viwango vya fundi wako, kitambaa na mengine.

kama suti ya kawaida ni 50,000/= unafikiria gwanda linaloshonwa kama unifom za maofisa wa polisi itakuwa sh. ngapi?
 
bado hujitambui ndugu mleta vioja badala ya hoja.Hebu nenda kanunue kitambaa hicho mwenyewe kisha peleka kwa fundi na baada ya hapo rudi hapa utuambie ghalama ni kiasi gani?Ukitaka pia ni PM itakuelekeza wapi utapata kwa bei ya 50,000/= ila usiulize wao wanapata wapi vitambaa na kushonea wapi.
 
Katika hali ambayo sikuwa najua lakini leo hii baada ya viongozi wa BAVICHA kuwasili hapa kwetu Mpanda Mjini nilivutiwa sana na Gwanda.Sikuishia kulitazama bali ilinibidi niulizie namna ya kulipata ndipo niliwauliza vijana waliokuwa wanayatembeza pale mkutanoni lakini nilistushwa na thamani ya lile Gwanda kumbe huwezi kulipata bila kuwa na TSHS 75,000/= sabini na tano elfu sasa nikajiuliza inakuwaje wanasema WaTZ tumepigika halafu Gwanda liuzwe kwa bei kubwa kiasi hiki.Kweli hapo kuna dhamira ya kututoa kwenye umasikini?Muungwana vitendo!!!!!

kuwa CDM lazma uvae gwanda?

................... inferiority complex..................
 
Umezoea fulana na kofia za bre kutoka kwa magamba wanao kukaanga kwa mafuta yko mwenyewe unajiona mjanja
 
Katika hali ambayo sikuwa najua lakini leo hii baada ya viongozi wa BAVICHA kuwasili hapa kwetu Mpanda Mjini nilivutiwa sana na Gwanda.Sikuishia kulitazama bali ilinibidi niulizie namna ya kulipata ndipo niliwauliza vijana waliokuwa wanayatembeza pale mkutanoni lakini nilistushwa na thamani ya lile Gwanda kumbe huwezi kulipata bila kuwa na TSHS 75,000/= sabini na tano elfu sasa nikajiuliza inakuwaje wanasema WaTZ tumepigika halafu Gwanda liuzwe kwa bei kubwa kiasi hiki.Kweli hapo kuna dhamira ya kututoa kwenye umasikini?Muungwana vitendo!!!!!
kwani suti sh ngapi? Au HUJAWAHI VAA SUTI?
 
Back
Top Bottom