chadema! chadema! chadema! wanatisha kila pembe ya nchi kweli freedom is coming tommorow

kessy kyomo

Member
Feb 1, 2011
72
11
kila kila kona ya nchi watu wanajivua gamba kweli hii balaa mpaka tufike 2015 tutaona mengi


CHADEMA Newala yazoa 276 CCM



VUGUVUGU la Mabadiliko (M4C) linaloendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) limeendelea kukichanganya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilayani Newala, na kufanikiwa kuzoa wanachama 276.

Katibu wa CHADEMA, Wilaya ya Newala, Mhunzi Rashid, katika taarifa yake iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, alisema kuwa wananchi mbalimbali wengi wao wakitokea CCM, walifanikiwa kujiunga na chama hicho baada ya kufanya mikutano ya ukombozi kwenye kata tano na vijiji vyake vipatavyo 32.
“Tumetumia uwezo na elimu bora tuliyoipata kutoka kwa viongozi wa kitaifa wa CHADEMA waliopata kutembelea mikoa ya kusini na pia walipofanya mikutano yao hapa imetutia ujasiri mkubwa, nasi kufanikiwa kupata wanachama hawa,” alisema Mhunzi.
Katika mikutano hiyo, Kata ya Kitangari waliweka kambi kwa siku saba na kufanya mikutano ya hadhara na kuvunja ngome ya CCM.
Mhunzi alitaja kata nyingine walizotembea katika jimbo hilo la Newala lenye kata 28 kuwa ni Mtopwa, Maputi, Nandwahi na Chiwonga.
Aliwataja baadhi ya vigogo ndani ya vijiji waliojivua gamba kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Azimio, na Mwenyekiti wa Kijiji cha Samora, aliyefahamika kwa jina la Mzee Mpotto.


Operesheni Vua Gamba Vaa Gwanda yazoa Tarime



na Sitta Tumma, Tarime



OPERESHENI maalumu ya 'Vua gamba vaa Gwanda' inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imeitikisa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, baada ya zaidi ya wanachama 3,500 wakiwemo viongozi wa CCM kujiunga na CHADEMA.
Wanachama hao wakiwemo viongozi wa CCM, wamejiunga rasmi na CHADEMA mwishoni mwa wiki, wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho, uliofanyika mjini Sirari kisha kuhutubiwa na mwenyekiti wa Baraza la Vijana taifa wa chama hicho (BAVICHA), John Heche.
Miongoni mwa viongozi wa CCM waliorudisha kadi kisha kukabidhiwa za CHADEMA mkutanoni hapo, ni pamoja na mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Sirari, Masha Vincent na mkewe Veronika Masha.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama wengine wapya waliojiunga na chama hicho kikuu cha upinzani nchini mara baada ya kukabidhiwa kadi, Masha alisema wamechukua uamuzi huo baada ya kuchoshwa na kile alichodai majungu, fitina na uhasama unaofanywa na baadhi ya viongozi wa CCM wilayani hapa.
Alisema, enzi za CCM zinaonekana kuelekea kuisha, hivyo kujiunga kwao na CHADEMA ni kuongeza vuguvugu la mabadiliko, na kuwaomba vijana kufanya maamuzi ya dhati katika kuleta mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi nchini.
Awali, mwenyekiti wa BAVICHA taifa, Heche aliwaomba Watanzania kutumia kura zao vizuri uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2014 pamoja na uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika nchini mwaka 2015 kwa kuipigia kura CHADEMA ili ishike dola na kuleta mabadiliko ya kweli katika maendeleo ya wananchi.
Alisema, CHADEMA imedhamiria kuleta ukombozi mpya kwa wananchi wa taifa hili, na kwamba iwapo itawezeshwa kuingia madarakani mwaka 2015, itahakikisha serikali yake inatumia vizuri rasilimali za nchi kwa faida ya Watanzania wenyewe na si wawekezaji.
Aidha, akiwa katika mkutano wa hadhara Muriba Tarime, Heche alilaani vikali mauaji ya vijana yanayodaiwa kufanywa na baadhi ya askari polisi katika mgodi wa dhahabu wa Nyamongo uliopo wilayani hapa, na kusema upo uwezekano wa kuishtaki serikali ya Tanzania katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu (ICC).


[h=2]Dk. Slaa afanyiwa umafya[/h]



comment_bubble.png

Maoni




headline_bullet.jpg
*Meneja wa hoteli amnyang�anya chumba
headline_bullet.jpg
Umeme wakatika, Tanesco wakana hujuma





Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa, amefukuzwa katika nyumba ya kulala wageni ndani ya Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) Mikumi, Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni sababu za kisiasa ikiambatana na kuzimwa kwa umeme kwa mji mzima kwa saa zaidi ya 12 ili kudhibiti mikutano yake ya hadhara anayoifanya.

Dk. Slaa ambaye aliwasili majira ya saa 8.00 mchana mjini Mikumi akitokea tarafa ya Malinyi, wilayani Ulanga, Morogoro, katika Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) ikiwa ni mwendelezo wa Operesheni Sangara, alifikwa na udhalilishaji huo baada kuonyeshwa chumba chake lakini baadaye akanyang’anywa.

Baada ya kuwasili hotelini hapo, Dk. Slaa alikabidhiwa funguo ya sehemu ya kufikia kutoka kwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare, na kuingia chumbani, muda mfupi baada ya kuingia katika chumba hicho alitokea meneja wa hoteli hiyo, Jacob Sumary, na kumueleza kuwa sehemu hiyo imeshawekewa ‘oda’ na wateja wengine na hivyo kutakiwa kuondoka katika eneo hilo mara moja.

Hata hivyo, Dk. Slaa alihoji sababu za mmoja wa walimu wa Veta kuacha majukumu yake na kujipa jukumu la kuhudumia hoteli kwa kumhudumia eneo lenye vyumba vitatu lenye thamani ya Sh. 75,000 kwa kila chumba kimoja Sh. 25,000.

Meneja huyo alishikilia kumtaka Dk. Slaa aondeke hotelini hapo kwa kuwa yeye hakuwa na taarifa za ujio wake. Dk. Slaa alitii na kuondoka.

Naye Sumary alipofuatwa na NIPASHE jana kwenye hoteli hiyo kuzungumzia kitendo cha kumnyang’anya Dk. Slaa malazi, alikataa kuzngumzia suala hilo.

Awali alisikiliza NIPASHE ikimuuliza juu ya hatua alizochukua na kutaka kujua ni kwa nini, lakini alisema hawezi kuzungumzia suala hilo na kukata simu yake.

Akizungumzia hali hiyo katika mkutano wa hadhara, Dk. Slaa alisema kuna mipango imefanywa kwa nia ya kumdhoofisha katika kampeni za kuwakomboa Watanzania.

“Kama mimi nafanyiwa mambo hayo kwa suala dogo la malazi tu na serikali ya CCM, je nyinyi wengine mtafanyiwaje? Mnapaswa kujifikiria mara mbili,” alisema Dk. Slaa.

Ghafla umeme ulizimwa katika mji wa Mikumi hali iliyotafsiriwa kuwa ni muendelezo wa hujuma zinazofanywa dhidi ya Chadema, kwani wananchi walidai mji huo haukuwa na tatizo la umeme.

“Watanzania wa leo siyo wa jana. Zimeni umeme. Hata mfanye nini tutaendelea na mkutano na wananchi watatusikiliza tu. Lakini nitakula nao sahani moja waliofanya hivi,” alisema Dk. Slaa.

Hata hivyo, kukatika kwa umeme huo kuliongeza mori kwa wakazi wa Mikumi kutokana na kuongezeka kwa wingi katika mkutano huo na kukemea vitendo vilivyofanywa na serikali dhidi ya Dk. Slaa.

Akizungumza kwa njia ya simu na NIPASHE, Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Morogoro, Deogratius Ndamugaba, alisema kukatika kwa umeme kulitokana na hitilafu za kawaida na siyo hujuma au msukumo wa kisiasa.

“Kukatika kwa umeme Mikumi siyo kwa sababu ya Chadema ila ni feeder ya Mikumi iko nje tangu saa 12.45 jioni. Nguzo imeanguka na inapaswa kubadilishwa na sehemu yenyewe ni porini. Kuna giza na Chui,” alisema Ndamugaba.

Alisema amekuwa akijaribu kuwasiliana na vyombo vya habari ili kuwapa taarifa wananchi wa Mikumi.

Alisema utendaji kazi wa eneo hilo kwa muda huo ulionekana kuwa mgumu na kwamba, tayari mafundi wa Tanesco walikuwa katika eneo la tukio kufanya marekebisho.



nilikuwa napita ndugu wadau


 
Inakuwaje Chadema kila wanapokwenda wanapokelewa na kukubalika vizuri na wananchi wa eneo husika?

Kwa mwendo huo, huenda CCM atabaki Nape mwenyewe kama alivyojitabiria mwenyewe.
 
Hujuma zooote,matokeo yake ni ushindi wa kishindo,Mungu yupo pamoja nasi.....M4C forever!!
 
Na bahati mbaya halipiti tu, linabaki hapohapo Newala na kuendelea kuharibu kuelekea 2015!

umenikumbusha kauli za kikwete kwamba ni upepo tu, utapita lakini sasa anapita yeye upepo umegeuka wa kisulisuli, unazunguruka tu at the same position! Alisema ni fotokopi lakini vimegeuka orijino na wao ndio wamekuwa fotokopi mashine! Wanakopi na kupesti!
Kaazi kweli kweli!
 
Huwezi kuzua mabadiliko kamwe. Mkolon ccm awaulize wenzake Wareno Wajeruman na Waingereza walitumia mbinu hzo wakashindwa itakua ccm hii ya ufisad makundi na dhuluma itaweza nini
 
Yule meneja wa mikumi ni ndugu yake na sioi sumary wa arumeru,bado ana hasira na moto wa cdm,wakae wakijua mafuriko hayazuiliki kwa mikono
 
wanaiga kunya kwa tembo[cdm] watapasuka ...............................
 
____.gif NIMECHUKIZWA NA KUSIKITISHWA SANA NA KITENDO KILICHOFANYWA NA MENEJA WA HOTELI KWA KUMFUKUZA DK SLAA. ILA TUKAZE MOYO MAKAMANDA WENZANGU KTK MAPAMBANO HAYA YA KUMNG'OA HUYU MKOLONI MWEUSI (CHAMA CHA MABWEPANDE). SIJAPATA KUONA WATU WENYE ROHO MBAYA KAMA HAWA CCM, ILA MUNGU YU PAMOJA NASI TUTAMUANGUSHA VIBAYA 2015.

KUNA HAJA KUTEMBEA NA JENERETA NA LOUD SPEAKERS KTK MIKUTANO YETU, NA KTK MALAZI POA TU, TUTALALA HATA KWENYE MAGARI YETU.

yaani ukiona mtu wa ccm anashambuliwa na simba msaidie simba ili ammeze vizuri.

Msiyashangae haya mambo yanayoratibiwa na kufanywa na CCM dhidi ya CHADEMA au dhidi WANANCHI WANYONGE NA MASIKINI.
Ni kwamba hali waliyonayo kwa sasa hawa ccm hawafai hata kufuga bali ni kuwasaka kokote walipo na kuwaangamiza kabisa.
cheki evolution yao;
View attachment 61926

TUSHIRIKIANE KWAPAMOJA WAPENDA MABADILIKO NA WANACHADEMA KWA UJUMLA KUMUANGAMIZA HUYU MNYAMA MBAYA KABISA CCM IFIKAPAO 2015.

Pipooooooooooooooooooooooooooo ooooooooz?????????????????????
 
Back
Top Bottom