TGIF: Ujiko Tujipe Wenyewe: JamiiForums Yapepea!!

Da thread inataja sleepness na sasa ni sa 9:58 alfajiri,tangu sa4 usiku niko humu. Kweli ni sleepness niite,basi ngoja nikaangalie kama kitanda changu kipo chumbani. Bye.
 
basi unadhani wanaweza kuja na kutoa compliment? noo.. hawakubali kukosea au hata in the same good "humor" kuonesha kuwa they were unnecessarily harsh. Bwana mdogo katoka kiukweli.

Teh teh teh....kweli hapo kajitahidi. Ila sijui stylist wake ni nani kwa sababu hilo coat suit kama limempwaya flani hivi. Ndo maana ile majuzi nilisema jamaa aanze kupiga tizi ajenge body ya kunyukia pamba za ukweli. Hivyo vimbavu viwili na pamba za ukweli wapi na wapi bana?

Hebu nenda GNC ukamnunulie protein shakes aanze kunywa na kupiga tizi. Aongeze ongeze muscles kidogo hasa mabegani na mikononi.

Halafu we Max...safari ijayo ukiwa unapigwa picha hakikisha mkono wako uko mbali na crotch yako. That's not very tasteful.

Kwa bahati mbaya viatu alivyovaa havionekani. Ningependa kujua alivaa viatu gani.
 


SliDing Roof Una la kusema tena hapa?

Lipo...

1. Suiti hiyo ni very cheap quality kwa kuitazama fabric yake inaonekana kuwa ni kama zile suti za kutungua za lile duka la Mtaa wa Azikiwe...opposite Empire cinema ya zamani...beside ile Petrol station kama hujafika Jengo la IPS


2. Number 2 suspect itakuwa ni MARIEDO kwani inafanana sana na suti za staff wa mfuko fulani wa jamii


3. Suti yake bwana mkubwa iko oversized na hiyo nayo ni problem pia...the same applies na hiyo siruali yake


4. Body language inaonyesha kuwa he was more exited kuchomekwa mle kwenye picha than anything else wakati huyu bwana is a CEO of an influential website in Tanzania...anaonekana ana woga na pia possibly embarrassed for some reasons...(steeve Dii atatufanyia analysis zaidi)


5. Shati lake nalo linaonekana kuwa linampwaya na mfano mzuri ni kola ya shingo inaonekana kuwa ni kubwa na imekaa ki wanafunzi wanafunzi tuuu


6. Kuna issue ya Tie, ambayo to be honest sio mbaya sana ila inaonekana ni ya kiofisi zaidi kuliko social event alyotuwakilisha bwana mkubwa


7. Mkanda wake nao unaonekana ni cheap quality na haihitaji kuelezea zaidi


8. Saa nayo itabidi niwe mkweli siijui lakini I wouldnt be surprised ikawa nadio zile zile za pale Mariedo lakini kama nimekosea naomba akija anikosoe lakini its certainly not a TAG or OMEGA or ROLEX or a BREITLING na of course its not even a SEKONDA...anaijua mwenyewe ni saa gani


9. Angeenda kwenye function lakini bila tie angeachia tuu shati na blazer la maana na sio hizi suti kwa mafungu za MARIEDO


10. Mbona hajaweka kitambaa kinachoendana na rangi ya tai kwenye mfuko wa kifua wa Koti?



That said naona kuna improvement kiasi kwa sababu zifuatazo:

1. walau bwana mkubwa ana attend social functions

2. Mwili kiasi unarudi nahisi ile picha ya awali iliyotumika na jamaa wa techmtaa ni ya zamani kwani nina suspect Steve Dii keshaanza kumuuzia yalee madude ya BARRY BONDS...

3. Ameachana na T Shirt ya michuzi



uatavyo

collar_78_450.jpg


Lakini akiamua kupiga suti basi idea za kupendeza zaidi ni kama hivi:

ZEdet.jpg
2ywtkp4.jpg
usher-VIP-perfume.jpg



Kama nilivyosema bado kuna room for improvement
 
Hivi kwanini watu wanatumia muda mwingi kujadili mavazi ya Max na sio mchango wake kwa taifa? Kwani angevaa batiki lake zuri au shati la kitenge cha urafiki linampunguzia vipi thamani yake katika ubora wa kile anachobuni, kukifanya na kukiendeleza!
Nilidhani watu wangejadili jinsi ya kuboresha mtandao huu au kwenda Next level, badala yake tumejikita kujadili mtu na si issue.

Ni maoni tu.
 
Hivi kwanini watu wanatumia muda mwingi kujadili mavazi ya Max na sio mchango wake kwa taifa? Kwani angevaa batiki lake zuri au shati la kitenge cha urafiki linampunguzia vipi thamani yake katika ubora wa kile anachobuni, kukifanya na kukiendeleza!
Nilidhani watu wangejadili jinsi ya kuboresha mtandao huu au kwenda Next level, badala yake tumejikita kujadili mtu na si issue.

Ni maoni tu.

I know you are entitled to your opinion and all but it's okay to loosen up every once in while and have room for some levity. You can't be serious all the time. Otherwise life would be so boring.
 
I know you are entitled to your opinion and all but it's okay to loosen up every once in while and have room for some levity. You can't be serious all the time. Otherwise life would be so boring.

Umenena vyema mkuu,
 
Hongera sana wakuu!!\\JF inapaaaa.....

I will do my part by at least having two new members!!!
 
4. Body language inaonyesha kuwa he was more exited kuchomekwa mle kwenye picha than anything else wakati huyu bwana is a CEO of an influential website in Tanzania...anaonekana ana woga na pia possibly embarrassed for some reasons...(steeve Dii atatufanyia analysis zaidi)[/IMG]

Kama nilivyosema bado kuna room for improvement
Umenifanya nicheke sana.

Hii picha nakumbuka nilipigwa 'ghafla' na Michuzi Jr na hapo alikuwa aniongelesha nikacheka.

As you've said, there's always a room for improvement.

NOTED
 
lets wait for the next picture...
Nyingine ntapiga na wewe tukiwa lile eneo letu, then wadau hapa watulinganishe...

Picha ya kwanza nilikuwa home office, hata nikiweka hizo trays nilizoona watu wananishauri niweke za IN and OUT naweza kushindwa ku-manage.

Rev Masanilo alishafika ofisi ambayo si ya nyumbani, anaweza kuelewa mpangilio wa ofisini upoje
 
Hapo amekaa! Akisimama ni Peter Crouch....

Steve D ndio mambo gani tena hayo...!? Hata kama ndivyo alivyo lakini uoni kaanzisha kitu chenye urefu na mapana yasio mithirika?

Ah ah ah, ndio maana na wewe baada ya kuona jina lako Steve D ni fupi ukaongeza dabo i, sio?

Aaaah wewe umeona hivyo?

Au kwenu mnapima urefu hata kama mtu amekaa? Huyo bwana huwezi kusema eti kijamaa kifupi, ni mtu wa kati yaani si mrefu wala si mfupi!

Hongera sana Max kwa kujaribu. Hayo ni mafanikio unayopaswa kumshukuru MUNGU kwa kukupa uelewa wa hivyo vitu!! Hongera sana na MUNGU akuzidishie hekima, busara na uchapa kazi!!

Kichwa cha sredi hii ni "TGIF - ujiko tunajipa wenyewe.." It is a humorous title to begin with. Kwangu mimi na wengine humu, kuongezea katika hilo, ni kwamba "ujiko tunajipa wenyewe na madongo tunatupiana wenyewe". Watu lazima tuoneshe kukomaa, matani kidogo kwenye thread yenye shamrashamra si jambo geni. 'Matter of fact, kuna jamii hapa Bongo wanataniana hata kwenye misiba.

Urefu wa Maxi unajulikana, wembamba au unene wake nao pia unajulikana. Kuna picha zilishawekwa hapa (kama sikosei, za harusi zilishawahi wekwa hapa pia), pia picha yake mwenyewe alishaitumia kama avatar. Kuongezea, kuna video yake hapa akiwa katika kuhamasisha watu wapige kura. Nami bila kuchelewa nilirusha dongo...

Thread: https://www.jamiiforums.com/tanzani...xence-live-on-eatv-uchaguzi-express-live.html



Watu bana eti status ya mtu ni kuvaa suti viatu sijui vya Italy na designer. Jamani tujifunze Uzalendo na tuwe mfano. Kweli Japo wakoloni bado wameondka w bado wanatutawala kifikra.

Tena wewe Maxence Chongesha Viatu vyako vya skuna/moka kwa wapare ukuze ajira. Ukitaka suti ya kwendea harusini Shonesha kwa mafundi wakali wa ndani. Then uje utumbie hapa ili na sisi tuwasupport watanzania wenzetutu. Tuachane na kutawaliwa na ukoloni.


Kwa nchi zetu ambazo ni Joto almost throught out the year kwanza nashangaa wa nini eti suti iwe ndo Vazi ramsi tena la kiofisi . Pili mtu kama Profession yake ni Civil engineer au Technician kwa nini Ulazimishe avae suti. Hii inaonesha kunabaadhi ya watu ngi mawazo yetu yako kisiasa siasa tu.

Max Hizo Pamba unazopiga hazina tatizo kabisa . Usiwasikilize wanasiasa. Nakupa Ushauri nenda mbali zaidi Moka zako chongesha hapa hapa bongo. Trouugh watu kama nyie industrykama "Bora" zinaweza kufufuka teh tehe teh


Nawasilisha

Mtazamaji, Nakubaliana na yote uliyoyasema. In fact, nami nilishayaongelea hapa jamvini mara kadhaa. Ni proponent wa kuona Watanzania tunavaa nguo tulizo buni na kutengeneza sisi wenyewe. Isitoshe, malighafi karibia yote tunayo. Tumeshindwa kuendelezana tu kwani, wengi wetu; haswa viongozi, wameshindwa kuonesha msimamo wa kuthamini vitu vyetu. Mh. Rais anavaa masuit na mashati kutoka nje na kwenda kuombeleza huko huko nje! Joho la Spika wetu linanunuliwa nje badala ya kushoneshwa hapa Tanzania na kukuza talent zilizopo.

Kwenye hii thread, nime comment hivyo kwani thread inahusiana na JF, plus ina beba mwonekano wa TGIF.

Kama una muda unaweza kufatilia msimamo wangu kwenye thread zifuatazo:



https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-na-siku-za-usoni-nunua-made-in-tanzania.html

https://www.jamiiforums.com/sports-...mbi-vya-kombe-la-dunia-lilipotua-bongo-4.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-na-viongozi-wa-kiimla-na-ukurupukaji-5.html





akivaa suti mtasema anaringa na ni fisadi ...amevaa casual wear mnasema hajui kupiga pamba ...

engineers always dress in casual wear

Tukomae ndugu zangu, some criticism is there to build na kwa kwa ajili ya humor!


sikutegemea premier member kama wewe utoe comment kama hii

U- premier wa member usitumike kusiliba mawazo ya mtu! Tukomae na kuwa watu wenye kuweza ku-deal na challenge za aina mbalimbali, hata zinazoelekezwa kwetu na wale tuwathaminio.

Kwa kweli kuna vitu nimejifunza na ninaendelea kujifunza - kweli kabisa kama angevaa mabatiki si ndio angeonekana hafai kabisa.

Some of the things said here are purely mean and diabolically insensitive. Watu wanapitisha hukumu ya mtu kwa maisha yake yote kwa picha moja na kusema vitu ambavyo are totally inappropriate. Wekeni na picha zenu basi na nyinyi tujue mnavyojua kuvaa na kujipamba. Iiish!!

Kaka, nadhani umeichukulia thread kivingine kabisaa, mbali na jinsi ilivyopokelewa na jinsi title ulivyoiweka!


Mkuu, nilikuuliza kiutani mwanzoni, mwenyewe Mkuu Max kakuruhusu kutumia taswira yake, nikaambiwa niishughurishe akili yangu...! Ona sasa jinsi walivyoshupalia hiyo picha...! Yaani wala hawajui may be ni siku ya Jumamosi/pili na ofisi inaruhusu siku hizo kuvaa vile unapenda...! I don't know.

easy easy!......dude don't take it serious............just learnt that JFs are happy to see the real Max.......i see nothing personal......TGIF just having fun...........

Exactly, my sentiments!!

basi unadhani wanaweza kuja na kutoa compliment? noo.. hawakubali kukosea au hata in the same good "humor" kuonesha kuwa they were unnecessarily harsh. Bwana mdogo katoka kiukweli.

Mkjj, this was meant to be a humorous thread, there is really no need to be so up beat about it. Even if that wasn't the intention, we sometimes have to go with the flow and let it be...


I am so pro Batiki and an extreme pro-made-in-Tz you know that.
Kuna thread nilisha anzisha kuongelea wanamitindo wetu na mavazi yetu, nikijitahidi kutafuta uwiano ili kupata nguo rasmi ya kitaifa, kwa wakinamama and possibly akina baba. Uganda wanayo, ukiona rangi tu unajua, Kenya hawana, haimaanishi tuwafate, Wanaijeria wanazo, Wagana wanazo, ukiona tu mtu unajua hii nguo ya wapi.

Kuna thread hii hapa yaweza kukukumbusha:


https://www.jamiiforums.com/sports-...-hizi-vimeenda-shule-unakubali-haukubali.html





Hivi kwanini watu wanatumia muda mwingi kujadili mavazi ya Max na sio mchango wake kwa taifa? Kwani angevaa batiki lake zuri au shati la kitenge cha urafiki linampunguzia vipi thamani yake katika ubora wa kile anachobuni, kukifanya na kukiendeleza!
Nilidhani watu wangejadili jinsi ya kuboresha mtandao huu au kwenda Next level, badala yake tumejikita kujadili mtu na si issue.

Ni maoni tu.

Thread inaongelea JF na waasisi wake. Kuna picha imewekwa, kauli mbiu ya JF ni kuongelea mambo kinagaubaga, sioni kama watu wamekiuka kwa kiwango cha kupitiliza katika kuongelea haya kwenye thread kama hii. TGIF comes with humor jamani!

Msimamo wangu, kama nilivyosema awali, ni kuona tunaendeleza yaliyo yetu na yanayotokana na ubunifu wetu, malighafi yetu. Lakini pale tunapovaa za "kuletwa", basi tuwe tayari kukosoana, si kwa nia mbaya, bali kwa ajili ya kujipa mwanga na kuendelezana. At the end of the day, kipendacho roho bana...
 
Back
Top Bottom