Tetesi mbalimbali barani Ulaya na dokezo muhimu

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
01/04/20

> Mkongwe Antonio Cassano akiwachambua Maradona na Messi anasema mkongwe Hugo Maradona amefanya mambo ambayo hayajawahi kuonekana katika soka kwa miaka 4 au 5 (yaani kandanda safi) lakini Messi amefanya vitu hivyo hivyo kwa miaka 15..mashabiki wa Maradona hawajahawi kukubaliana na hilo Ila kuna MTU aliyemweka kando..

> Je, nani kushinda tuzo ya mchezaji bora wa PL msimu huu kati ya hawa;

Kevin De Bruyne
Jordan Henderson
Sadio Mane

> Vilabu vya Ujerumani Dortmund & B.Leverkusen vimedhamiria kusimama kidete juu ya thamani ya makinda wao mahiri wanaowanyima usingizi vigogo J.Sancho & K.Havertz ambayo ni zaidi ya £100m.

vilabu hivo vinasema vipo teyari kusubiri had I 2021 ili kuwauza nyota hao, ambao wore watakuwa wamebakiza mwaka mmoja katika mikataba yao.

> Mkongwe Rio Ferdinand anataka Man Utd iwasajili Kane & Sancho.

"Harry siku zote amekuwa mkimya na anaporejea ,amekuwa mtu muhimu, najua Man Utd watamuangazia.

" ninamtaka Sancho aende katika timu atakayoweza kucheza,kujiimarisha na kushinda mataji..ninafikiri Utd ni sehemu take sahihi."

> Nae mkongee Totti anasema ofa iliyokuwa ngumu kwake ni ile ya kuondoka Roma 2004 na kujiunga na Real Madrid..niliamua kuliko nipate hela nyingi, ni kheri nivae jezi moja tu milele..kwangu Mimi mapenzi na upendo ndio kilikuwa kitu cha thamani zaidi kuliko hela au mataji."(watu na mapenzi yao)

> kocha wa Brazil bwana Title akiongea na kituo cha France Football kuhusu Neymar anasema;
"Neymar anakuhakikishia wewe mambo ambayo huyatarajii katika mchezo kama skills zake binafsi au njia ya ujumla ambayo wengine hawana, na kuwa nae ni faida kwa timu kuna kuwa na utofauti kwa sababu ni machachari na msumbufu..ila namwongelea yule Neymar ambaye yupo tulivu kiakili na kimwili..Neymar ni muhimu lakini pengo lake halizibiki.."

> Mkurugenzi wa B.Munich K.H.Rummenigge akiongea na kituo cha Tz huko ujerumani kuhusiana na mabadilishano ya wachezaji kati ya beki wao Alaba na winga kinda Sane anasema;
"kama nilivyosikia huo uvumi uliosambaa kwamba kuna ishu ya kimabadilishano na Man city..kwa kuongezea tu niliweke sawa hilo ,ni ngumu na hakuna lolote kuhusiana na huo uvumi na hilo sio pendekezo la B.Munich kiujumla, hatupo katika sokoni sisi..

> Kipa wa zamani wa Man Utd Mark Bosnich akiongea na mtandao wa Goal kuhusiana na hali ya magolikipa Klabun pale anasema Kipa Henderson amekuwa imara na kulithibitisha hilo mwenyewe kwamba ni golikipa mzuri..kwa sasa De Gea amefanya makubwa na Man Utd kwa muda mrefu licha ya mushkeli za hapa na pale ambayo ni hali ya kila kipa,hakuna mashaka katika hilo..unapokuwa katika klabu kubwa kuna mambo unakuwa unayaongeza kiufundi,na kwa wakati huu, nitaendelea kumpa karata yangu De gea...Dean Henderson bado ataendelea kuwa benchi na kutolewa kwa mkopo.

> Fahamu hili-Kipa wa Juventus Wojciech Szczesny amefichua kuwa Cristiano Ronaldo alilazimika kuwanunulia wachezaji wenzake wote wa Juventus Kompyuta aina ya iMac baada ya kupigwa kadi nyekundu katika mechi ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Valencia Septemba 2018.*

Ronaldo alifanya hivyo kufuatia sheria iliyokuwa imewekwa na kocha Juventus kipindi hicho Massimiliano Allegrii, ikisema kuwa kila mchezaji atakayepata kadi nyekundu atalazimika kukipa kikosi chote zawadi....


> Mkongwe Robin Van Persie akiongelea walivyoitwa na mzee Fergie baada ya kufungwa na Man city;
"Siku moja baada ya mchezo (ambao tulifungwa) Sir Alex alikuwa na picha ambazo alizibandika katika ukuta wa chumba cha kubadilishia nguo ,ambazo ziliwahusu wachezaji wawili waliopigwa usiku katika kumbi za starehe..alituambia kikosi kizima kwamba " hao watu endapo tusiposhinda ligi in kwa sababu ya hao watu wawili."

> Man Utd inafikiria kuelekeza nguvu zao kwa Leicester city juu ya kiungo Muingereza James Madison 23 ,baada ya dili la muda mrefu la nahodha wa Aston Villa Jack Grealish 24yrs kuingia doa..

> Liverpool hawana mpango na kiungo wao wa zamani Phillips Coutinho 27yrs,ambaye bado yupo kwa mkopo Bayern Munich akitokea Barcelona...

> Miamba Real Madrid wanamfukuzia kwa kuaribu kaka mpya wa Sao Paulo ya Brazil Igor Gomes 21yrs, huku Barcelona, Sevilla & Ajax pia vikihusishwa na kinda Huyo wa Brazil...

> kiungo wa Chelsea na Brazil Willian 31yrs anafikiria kuendelea kucheza katika PL endapo ataondoka darajani msimu huu, huku Arsenal & Spurs zikimtolea macho kwa ukaribu...

> Arsenal,Spurs & West ham zote zinamwinda beki mcroatia wa Liverpool Dejan Lovren 30yrs, ambaye hana mustakabali mzuri wa kiuchezaji Anfield..

> Kiungo Dani Ceballos 23yrs aliye kwa mkopo Arsenal amesema yupo teyari kurejea Real betis kuliko kubakia dimba la emirates, kama klabu take miliki Haiti mrejesha...

> kocha wa Burnley bwana Sean Dyche yupo teyari kuunga mkono hoja ya kumalizia msimu bila mashabiki katika michezo iliyobakia PL...

*PIA KATIKA TAKWIMU NAKO KWA UCHACHE*

• Tunaambiwa Romelu Lukaku ni mchezaji wa 5 mdogo katika historia ya PL kufunga magoli 100 katika shindano hilo...akifanya hao na vilabu hivi

WBA 17
Everton 68
Man Utd 28

(akiwa ndie kinda wa nje ya Uingereza kuwahi kufanya ivyo)

• Pia mshambuliaji Robert Lewandowski aliwachabanga magoli 3 (hat-trick) klabu yake ya zamani B.Dortmund siku kama ya Jana 2018 katika ushindi wa 6-0...(unaambiwa ushindi huo in mkubwa zaidi kuwahi kutokea kwa mahasimu hao tangu 1971 ,Bayern ilipowachapa tena kichapo cha mbwa mwizi 11-1 (Bayern Munich mwamba wa Bundesliga huu)

• Vilevile tunaambiwa mashuti ya Cr7 katika ligi yapo katika uwiano mkubwa mno katika kipindi cha misimu 5 iliyopita sawa na 16.2% tangu alipofunga magoli 48 msimu wa 2014/15 katika Msimu wa La Liga....(nguvu bado ipo mguuni sema uchu wa huyu jamaa ni mkubwa mno aongeze utulivu na kutengenezea wengine mashuti mengi lakini ana goli 21 Series A)

• Pia siku kama ya Jana 31/03/2007 , mkongwe na kocha wa Man Utd sasa Ole Gunnar Solskjaer alifunga goli lake la 91 katika PL..(idadi ya juu katika katika orodha ya wafungaji kwenye ligi hiyo, huku pia goli lake la kwanza na la mwisho akiyapatia katika mpinzani yule yule ambaye ni Blackburn.

• Nae mkongwe Peter Crouch siku kama ya Jana 2007 aliifungia Jogoo (Liverpool) perfect hat-trick katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Arsenal dimbani Anfield yaani na

Mguu wa kulia
Kichwa
Mguu wa kushoto (Wana mtutu walijaa kwenye mifumo ya watu)

• Vilevile nikihitimisha na hii kwa Leo tunaambiwa katika msimu wa 2001/02 mkongwe kiungo wa nguvu Thomas Rosicky akiwa ujerumani na B.Dortmund alikuwa na umri wa miaka 21, embu tuzitupie jicho namba zake zilivyokuwa katika huo msimu:

Michezo 49
Magoli 6
Assists 20

(Anatajwa kama miongoni viungo bora katika hii karne ya 21 mtaalamu huyu aliyekuwa akizijali nywele zake na fundi mkubwa wa kubadili mchezo)

Mpaka hapo sina la ziada kwa Leo wadau wenza wa kabumbu..Ahsanteni...

PRAY FOR WORLD AGAINST CORONA CRISIS




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungekuwa unatujuza yanayojili juu ya michezo kupitia huu uzi mara kwa mara. Hilo ni ombi langu kwako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom