EPL: Man City yaibamiza Man Utd 3-1

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
1,397
3,492
Timu ya Man City imezidi kujiwekea mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wake wa EPL baada ya kuwafunga wapinzani wao wa Jiji la Manchester timu ya Man Utd kwa magoli 3-1.

Man Utd ndio walikuwa wakwanza kupata goli kupitia Rashford dakika ya 8.

Man City wakasawazisha dakika 56 kupitia Phil Foden kabla ya kuongeza goli la pili dakika ya 80 kupitia Foden tena.

Wakati Man Utd wakitafuta njia ya kusawazisha wakapigwa goli la 3 kupitia Haaland dakika 90+1 na kufanya matokeo kuwa 3-1.

Golikipa Andre Onana alikuwa katika siku bora leo na kujitahidi kuokoa michomo ambayo pengine kama ingezama wavuni kipigo kingekuwa kikubwa leo kwa Man Utd.

Man City amejikusanyia alama 62 huku akizidiwa na Liverpool alama 1 na wanakutana weekend ijayo pale Anfield katika mchezo utakaotoa mwelekeo wa ubingwa kwa msimu huu.
IMG_0139.jpeg
 
Back
Top Bottom