Tetemeko laipiga Morocco, zaidi ya Watu 2000 wafariki Dunia, majeruhi waongezeka

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,321
24,228
1694270799460.png

SEPT 10, 2023

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani, hadi sasa Watu 2,012 wamefariki dunia huku wengine 2,059 wakijeruhiwa na 1,404 wako katika hali mbaya kiafya.

Shirika la Afya Duniani limesema zaidi ya Watu 300,000 wameathirika na Tetemeko hilo lililopiga maeneo kadhaa ya Jiji la Marrakech ikiwemo Kijiji cha Asni ambacho kielezwa kuharibiwa karibia nyumba zote

Ni Tetemeko la pili kusababisha maafa makubwa ndani ya mwaka mmoja ambapo Miezi 7 iliyopita, takriban watu 50,000 walipoteza maisha kwa kupigwa na Tetemeko Nchini Uturuki
============

SEPT 9, 2023

Wakati zoezi la uokoaji likiendelea, maafisa wamesema Watu wengi bado wamenaswa kwenye vifusi vizito na idadi ya waliopoteza maisha inazidi kuongezeka kwa kasi ambapo hadi sasa imefikia Watu 1037.

Pia, imeelezwa kuwa Miili ya Watu wengine iko katika maeneo ambayo ni magumu kufikika kwa urahisi huko Marrakech.

Usiku wa kuamkia leo Septemba 9, 2023, Morocco imepigwa na Tetemeko lenye kipimo cha Richa 6.8 ambalo kati ya Matetemeko makubwa kuwahi kutokea barani Afrika
============

09 September 2023
Marrakech, Morocco
Tetemeko kipimo cha Richter 6.8 laipiga nchi hii ya Kaskazini Magharibi ya Morocco muda wa saa 5 usiku tarehe 8 September 2023

===========

Tetetemeko kubwa limetokea usiku wa kuamkia leo Septemba 9, 2023 likiwa na ukubwa wa Richa 6.8 na kusababisha uharibifu zaidi katika Mji wa #Marrakesh na mingine kadhaa.

Inaelezwa vifo vingi vimetokea kwenye maeneo ya miinuko na milima ambapo ni vigumu kufikia, Ripoti ya Wizara ya Mambo ya Ndani imeeleza kuwa watu 153 wamejeruhiwa.
-
Miji mingine iliyoathiriwa na tetemeko hilo ni Al-Haouz, Ouarzazate, Azilal, Chichaoua na Taroudant.

2.JPG

1.JPG

3.JPG

1694235002204-png.2743738

Wizara ya Mambo ya Ndani ilitangaza katika ripoti ya muda kuwa watu 296 wamekufa kufuatia tetemeko la ardhi lililoikumba Morocco Ijumaa jioni na 153 kujeruhiwa.

Ripoti iliyochukuliwa saa nane usiku huu 9.9.23 inaonyesha uharibifu wa nyenzo kadhaa katika maeneo mbalimbali yasiyo na watu katika majimbo ya Al Haous, Marrakech, Ouarzazate, Azilal, Chichaoua na Taroudant yaliyopo milima ya Atlas

Taasisi ya Kitaifa ya Jiofizikia ilitangaza kuwa kitovu cha tetemeko la ardhi, kilichotokea kina kisicho kirefu toka ardhi ya juu takriban kilomita 8 chini ya ardhi, kilikuwa katika latitudo ya kaskazini ya digrii 30,961 na longitudo ya 8,413 ya magharibi, taarifa ilisema.


=============

MOROCCO: Idadi ya Vifo kutokana na Tetetemeko la Ardhi la ukubwa wa Richa 6.8 lililotokea Usiku wa kuamkia Septemba 9, 2023, imefikia 632, huku zoezi la Uokoaji likiendelea kwa waathirika waliofunikwa na vifusi.

Wizara ya Mambo ya Ndani Nchini humo imesema vifo vingi vimetokea katika maeneo ya Al-Haous, Marrakesh, Ouarzazate, Azilal, Chichaoua na Taroudant, na kuongeza kuwa Watu wasiopungua 329 wamejeruhiwa.

=================

Morocco earthquake live news: At least 632 killed in quake near Marrakesh

At least 632 killed and 329 injured, according to Moroccan state media.

Dr Hesham Kharmoudi told Al Jazeera from Marrakesh that the number injured people have been increasing.

“Authorities and volunteers continue working to reach those who need help and those injured,” he said, adding that some of the affected areas are hard to reach.

He also said: “All medical personnel and departments have been prepared [for disasters]. The only problem is running out of blood bags reserve, so we call on the people to donate blood.”

'In almost every single town in Morocco last night, people sat outside their homes'

People spent the night on the ground outside in Marrakesh, 8 September 2023

People in towns across Morocco have spent the night sitting outside their homes after the earthquake, a British journalist living in the country says.

Speaking to BBC Radio 4's Today programme, Martin Jay said: "There were reports coming through on Moroccan media warning people not to go back into their homes," he said.

"This was a nationwide message that was put out by the authorities.

"So you have this weird evening [in] almost every single town in Morocco, [where] most people are sitting on the ground outside of their houses or apartment blocks, because they were afraid of the second earthquake which they predicted would come two hours later."
 
Mamia ya watu wanahifiwa kufariki Nchini Morocco Kufuatia tetemeko Kubwa lenye Ukubwa wa 6.8 kwenye kipimo Cha Fitcher.Taarifa za punde zinaonesha takribani watu 300 wamefariki.

Mamia ya Majengo yametikiswa na kuporomoka kwenye Miji mikubwa kama Marrakesh huku tathmini ya athari ikiendelea kufanywa.

Waokoaji wanaendelea kuwatafita manusura.

 
Mamia ya watu wanahifiwa kufariki Nchini Morocco Kufuatia tetemeko Kubwa lenye Ukubwa wa 6.8 kwenye kipimo Cha Fitcher.Taarifa za punde zinaonesha takribani watu 300 wamefariki.

Mamia ya Majengo yametikiswa na kuporomoka kwenye Miji mikubwa kama Marrakesh huku tathmini ya athari ikiendelea kufanywa.

Waokoaji wanaendelea kuwatafita manusura.
Ritcher
 
Ikumbukwe Morocco ndio Wametujengea Msikiti mkuu wa BAKWATA pale Kinondoni

Sasa wamorocco wanaomba mchango wa Damu kufuatia WATU wengi sana kujeruhiwa kwenye tetemeko kubwa la ardhi

Nawatakia Sabato njema 😀

Kwani FaizaFoxy, The Boss na The Big Show
tatizo linaanzia hapo. Misikiti kila kona, inapokuja issue kama hii..............hakuna response. Naona hata hapa vijimadrasa vya vyumba viwili, vitatu kama njugu mtaani, lakini other social amenities hawana habari nayo kuwaletea/kuwajengea

Mnisamehe
 
Back
Top Bottom