Tendwa utapona kweli au wakribia ku staafu au unatuzuga kwamba huko nao jamaa wanunua shahada ? Polisi walisema si kosa mkakaa kimya leo baada ya kila kitu kuwa wazi ndiyo mnakurupuka ? Kweli Tanzania ina maajabu .
Wakati Tendwa akitaja sababu hizo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo hilo, Protace Magayene, ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kubuni mbinu mbadala ya kuhakikisha wananchi wanajitokeza kupiga kura. Wapigakura walioandikishwa katika Jimbo la Igunga ni 171,019 na waliojitokeza kupiga kura mwaka huu ni 53,672 sawa na asilimia 31.3, kukiwapo ongezeko la asilimia 2.7 ikilinganishwa na idadi ya waliopiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, ambao walikuwa 49,013 sawa na asilimia 28.6 ya 171,077 waliokuwa wamejiandikisha.
Source: IPPMedia
Kadhalika alitaja sababu za watu wachache kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, mkoani Tabora, ikilinganishwa na idadi ya walioandikishwa, kuwa ni pamoja na ujambazi wa kisiasauliofanywa na baadhi ya wanasiasa kununua shahada za wapigakura.
Ndege njanja hunaswa kwenye tundu bovu. Idadi ya waliochoshwa na uchakachuaji na ujambazi wa kisiasa inazidi kuongezeka, hadi 215 njia itakuwa nyeupe na taratibu za wapiga kura kufanyia marekebisho.