Pawaga
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 1,330
- 966
Haya yamezungumzwa na mh Tendwa kuwa upinzani unakuwa kwa kasi ya 40 asilimia na magamba yanaporoka. Kuna watu humu jamvini wakiambiwa huwa wanabisha sana nadhani sasa wataelewa maana hata hao wakubwa wao wanalijua hilo.
Source: Nipashe
Source: Nipashe
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, amesema matokeo ya uchaguzi mdogo wa Igunga ambao mgombea wa CCM alishinda kwa mara nyingine yametoa picha kuwa upinzani unazidi kukua na CCM inashuka.....
Akitoa tathimini ya uchaguzi huo, ambao ushindani mkubwa ulishuhudiwa miongoni mwa vyama vitatu wakati wa kampeni, CCM, Chadema na CUF, Tendwa, alisema alikwisha kusema tangu baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kuwa upinzani umekua kwa asilimia 40 ikilinganisha na ushindi wa kishindo wa CCM wa mwaka 2005. "Matokeo ya uchaguzi wa Igunga yanaonyesha kuwa upinzani unazidi kukua na CCM inashuka," alisema Tendwa alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari. Alisema hali hiyo inatokana na ushindani mkubwa wa kisiasa uliopo hivi sasa nchini kati ya vyama vya upinzani na CCM.
Kadhalika alitaja sababu za watu wachache kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, mkoani Tabora, ikilinganishwa na idadi ya walioandikishwa, kuwa ni pamoja na ujambazi wa kisiasa uliofanywa na baadhi ya wanasiasa kununua shahada za wapigakura.
Wakati Tendwa akitaja sababu hizo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo hilo, Protace Magayene, ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kubuni mbinu mbadala ya kuhakikisha wananchi wanajitokeza kupiga kura. Wapigakura walioandikishwa katika Jimbo la Igunga ni 171,019 na waliojitokeza kupiga kura mwaka huu ni 53,672 sawa na asilimia 31.3, kukiwapo ongezeko la asilimia 2.7 ikilinganishwa na idadi ya waliopiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, ambao walikuwa 49,013 sawa na asilimia 28.6 ya 171,077 waliokuwa wamejiandikisha.
Hata hivyo, Tendwa, alisema:"Uchaguzi ulikuwa wa amani na utulivu. Kura zilipigwa kwa amani, hakukuwa na msukosuko, ingawa kulikuwa na kasoro za kiutendaji. Kasoro hizo zimewaathiri watu wa Igunga kutokupiga kura. Aliongeza: "Athari hizo si kubwa, lakini athari ni athari. Idadi ya waliojitokeza kupiga kura Igunga inasikitisha … Nasubiri ripoti, lakini nimeambiwa kulikuwa na kununua kwa kadi za kupiga kura na baadhi ya wanasiasa. Huu ni ujambazi wa kisiasa."
Alisema sababu nyingine iliyochangia watu wachache kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo, ni kauli na vitendo vya vitisho vilivyotolewa na baadhi ya wanasiasa wakati wa kampeni. Tendwa alisema vitisho hivyo viliwafanya wananchi wa Igunga, ambao wengi wao wanaishi vijijini kuogopa kwenda kupiga kura, badala yake kuamua kwenda kutafuta mahitaji yao muhimu, kama vile maji..............
........Hata hivyo, alisema kila chama cha siasa, kikiwamo chama tawala (CCM), kinawajibika kubadilika na kuzingatia utawala bora, uongozi mzuri na uvumilivu wa kisiasa kwa vile hakiko peke yake katika medani za siasa.
Source: IPPMedia