buyegiboseba
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 535
- 145
Najua uko kazini,timiza wajibu, ukweli wa wazi ni kuwa CCM inaporomoka kwa kasi ya ajabu, na kwa bahati mbaya inaporomoka tokea mjini kuelekea vijijini,Strategy ya Upinzani nimeipenda ya kuwadhoofisha kuanzia mjini, believe me 2015 Dar es Salaam CCM itakuwa chama cha upinzani, zile sera zenu za kuwatisha watu kuwa ukichagua upinzani unaleta vurugu zimepruvu wrong, majiji yamekamatwa na upinzania na maisha yanakwenda bila vurugu.
Uungwa ni kukubali ukweli halafu ukajenga hoja. asilimia 80 ya urais hadi 60 ya kuchakachua wakati rais yuleyule si ya kujifanya huioni, mgombea mgeni anakomba 44.5 asilimia bado unajitutumua kuwa una nguvu
Samsoni yule wa biblia(samahani kama hujawahi kuisoma) aliponyolewe nywele nguvu zilimuishia alipoambiwa anavamiwa alikitutumua akidhani bado nguvu zipo,alichoambulia ni kutobolewa macho yote mawili
Mungu akikuweka hai 2015 utakuwa shuhuda wa kifo cha CCM, naomba tu JF idumu daima ili tuelezane ukweli humuhumu.
Sikio la kufa halisikii dawa.

Kitu kimoja kizuri sana ambacho kitaiendeleza Tanzania ni kuwa na upinzani wa kweli, hiyo ni faraja na neema kwa kila Mtanzania, lakini si upinzani kama wa CHADEMA, upinzani wa kuongelea watu badala ya sera.
Kwa kuwa Tanzania bado ni mwanjo mwanjo katika siasa za vyama vingi, kila mtu anawaona magamba kwa sasa wamaana sana kwa kuwa wanachokiona ni wao kwa mara ya kwanza ndio hicho cha kuongelea watu, Watanzania ni kama vipofu tilioona punda. Lakini, kizuri ni kuwa watu wameshaanza kujuwa siasa maji taka ni nini na siasa za maendeleo ni nini, siasa maji taka ni turufu ya ya garasa, turufu ya mali ni siasa za kuleta maendeleo kwa vitendo. Hakuna mpaka sasa chama pinzani kilichoonesha haswa namna yakutatuwa matatizo yanayomkabili Mtanzania kila siku, wapinzani kila kukicha, Rostam, Kingunge, Makamba, Januari, Februari. Ni nini hii?
Tunataka kusikia upinzani umeingia ubia na kampuni la kufuwa umeme wa bei poa, kama alivyojaribu Mrema. Tunataka kuona upinzani unajenga shule bora za kuigwa japo moja kila mkoa kwa kuanzia, tunataka kuona upizani unaanzisha viwanda vya mfano, ambavyo watasema haya ndio mnayakosa kwa kuichaguwa CCM.
Leo upinzani umekazana Rostam, Rostam, Rostam, Rostam. Huyo Rostam amekuwa mkubwa kuliko upinzani wote, anatisha kwa kutukuzwa na upinzani, kama mnajuwa ana madhambi mbona hatuwaoni mkampeleka mahakamani? au mnaogopa atawaadhiri kama alivyomwadhiri Mtikila?
Hakuna wa kusifiwa kwa kuuboresha upinzani katika Tanzania kama Kikwete, yeye ndio alioahidi kuikuza demokrasi na kweli anafanya hivyo, kwa wengine hatuoni ajabu, ila tunachostaajabu tunapoona upinzani umepewa fursa kubwa sana katika awamu hii lakini hawazitumii ipasavyo, wao wamebaki na ngonjera za Rostam.