Gsana
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 4,383
- 1,321
Hivi kuna mtu huku jamvini leo 2011 hajui wala hataki kujuwa umuhimu wa kunywa maji wakati unatoa speech ndefu? Mkullo ametoa speech ya budget kwa zaidi ya saa 2! Kunywa maji kama mtu anatoa speech ndefu is a human-thing. Angalia wanasiasa wa nchi zingine wakati zingine.Maybe tufundishane nini umuhimu wa maji mwilini!!!!
mwaka 2010 mwanzoni nlikuwa natokea morocco kwenda studio ,nlipopita pale biafra nkasikia mhubiri Mwakasege anasema,Mungu kampa afya njema,ana uwezo wa kuhubiri masaa 10 bila kuomba maji wala kuanguka,wala sauti kukoroma,pia akasema hana kumbukumbu ya mtu mwenye afya yoyote anayeweza kuomba maji wakati anaongea mambo ya maana. Kwa kuwa sina imani naye sikukatisha safari yangu,nkatoweka ila maneno yake yalinikaa moyoni. Nimechunguza nkaona kweli,ebu jaribu kuchunguza ijumaa misikitini kama kuna mtu anaenda na maji ya kunywa,na hawa watu wanaongea sana na kwa msisitizo mkubwa. Pia hata makanisani mapadre au wachungaji hawaendi na maji wala hawasafiri na ambulance nyuma. Jumapili iliyopita nlipowasha tv sa4 asubui ikafunguka Trenet. Nkamsikia yule mzee mwenge, Mwingira akikejeli eti ktk msafara kutembea na ambulance nyuma ni kujihisi umarehemu umarehemu ivi. Mwenye kumbukumbu ataweza kudhibitisha aya. Tusichukulie vijineno ivi kama stori,watawala wetu wanaiga utaratibu mbaya ambao hata akina mch.mtikila urejea na kusema afya za watawala zinawafanya wasiwe na uwezo wa kufikiria maendeleo. Watawala wasizoee utaratibu huu waweza kuleta taswira isiyo halali ktk jamii.