TEC yashauri Viongozi wa Serikali wasiwe wasimamizi wa Uchaguzi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,790
218,420
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba, Katibu wa TEC Padri Kitima, leo 8/01/2024 Ametoa maoni ya Baraza la Maaskofu wa Kikatoliki ndani ya Bunge la Tanzania, kama Mchango wa Kanisa hilo kwenye Miswada ya Sheria za Uchaguzi.

TEC imesema kwamba Viongozi wa Serikali hawapaswi na iwe mwiko kwao kusimamia uchaguzi wowote , Kazi hiyo inapaswa kufanywa na Tume ya Uchaguzi tu.

Taarifa kamili hii hapa

Screenshot_2024-01-08-17-17-50-1.png

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limeshauri Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutowatumia viongozi wa Serikali katika kusimamia uchaguzi na badala yake wahusike wenyewe katika uchaguzi mkuu na wa serikali za mitaa.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa TEC, Padre Charles Kitima baada ya kutoa maoni yake kwa Bunge kuhusu miswada ya sheria za uchaguzi leo Jumatatu, Januari 8, 2024, Bungeni jijini Dodoma.
 
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba , Katibu wa TEC Padri Kitima , leo 8/01/2024 Ametoa maoni ya Baraza la Maaskofu wa Kikatoliki ndani ya Bunge la Tanzania , kama Mchango wa Kanisa hilo kwenye Miswada ya Sheria za Uchaguzi...
Wazo zuri ila watawala sidhani kama hii hoja kama wataikubali lazima wataipindisha iwe nzuri kwa upande wao, wanaweza kukubali ila wakaweka kipengele Dc ama ded wakawa wajumbe kwenye zio kamati kutokea maeneno yao
 
Nimekutana na timu mbili za watoto wanacheza mpira. Timu moja naona ilijipanga, imekuja na vifaa vyote vya kucheza mpira kuanzia jezi, viatu n.k pia mpaka refa imekuja nae.

Nikiangalia timu ya hawa watoto wengine haieleweki kabisa, naiona kama haiko siriazi na mpira maana hawana jezi, wala viatu wamebaki wanamlalamikia refa anapendelea atoke hivyo hawamtaki.

Walivyoniona tu wamenifata mimi mpita njia wananilalamikia nifanye kitu kuwaokoa kuhusu refarii ndio nikajua pia kumbe hata na huo uwanja wanaochezea hii timu iliyokuja fulu suti iliutafuta pia.

Imebidi niwaambie watulie kwanza wayaongee halafu nikasepa. Sijui kama hii timu nyingine ambayo haina viatu itasikilizwa.
#shabanrobert
#ngungiwathiong'o
#chinuaachebe
 
Tamko Kwa waumini kuhusu alichosoma Papa kuhusu kubariki wapenzi wa jinsia moja Hilo Baraza la Maaskofu TEC watatoa lini ?

Waumini wanasubiri nimekuja mbio nilikijua wametoa Hilo tamko
Unawasubiri TEC wakwambie njia ipi uifuate kwenye maisha yako?!

Kama una familia iko siku utaitoa sadaka kwa wanaojielewa wakulelee.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Tamko Kwa waumini kuhusu alichosoma Papa kuhusu kubariki wapenzi wa jinsia moja Hilo Baraza la Maaskofu TEC watatoa lini ?

Waumini wanasubiri nimekuja mbio nilikijua wametoa Hilo tamko
Papa hajabariki wala hajatoa tamko lolote kuhusu hilo.Sheria kali imepitishwa Vatican kukubaliana na hoja za Ushoga maana Mwenyezi Mungu hajawahi bariki dhambi na Kanisa Katoliki halina mamlaka ya kubariki dhambi.
 
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba , Katibu wa TEC Padri Kitima , leo 8/01/2024 Ametoa maoni ya Baraza la Maaskofu wa Kikatoliki ndani ya Bunge la Tanzania , kama Mchango wa Kanisa hilo kwenye Miswada ya Sheria za Uchaguzi .

TEC imesema kwamba Viongozi wa Serikali hawapaswi na iwe mwiko kwao kusimamia uchaguzi wowote , Kazi hiyo inapaswa kufanywa na Tume ya Uchaguzi tu

Taarifa kamili hii hapa

View attachment 2865560View attachment 2865561
ni ushauri mzuri sana japo hauishurutishi tume kuupokea na kuutekeleza kama ulivyo.....
Kwa maoni yangu bado watumishi wa umma ni Watanzania na wanastahili kusimamia uchaguzi kama ambavyo Watanzania wengineo wana haki hiyo pia.🐒
 
Nimekutana na timu mbili za watoto wanacheza mpira. Timu moja naona ilijipanga, imekuja na vifaa vyote vya kucheza mpira kuanzia jezi, viatu n.k pia mpaka refa imekuja nae.

Nikiangalia timu ya hawa watoto wengine haieleweki kabisa, naiona kama haiko siriazi na mpira maana hawana jezi, wala viatu wamebaki wanamlalamikia refa anapendelea atoke hivyo hawamtaki.

Walivyoniona tu wamenifata mimi mpita njia wananilalamikia nifanye kitu kuwaokoa kuhusu refarii ndio nikajua pia kumbe hata na huo uwanja wanaochezea hii timu iliyokuja fulu suti iliutafuta pia.

Imebidi niwaambie watulie kwanza wayaongee halafu nikasepa. Sijui kama hii timu nyingine ambayo haina viatu itasikilizwa.
#shabanrobert
#ngungiwathiong'o
#chinuaachebe
Sasa kama hiyo timu imeandaa mpaka Refari unafikiri kuna mchezo mzuri hapo?
 
Papa hajabariki wala hajatoa tamko lolote kuhusu hilo.Sheria kali imepitishwa Vatican kukubaliana na hoja za Ushoga maana Mwenyezi Mungu hajawahi bariiki dhambi na Kanisa Katoliki halina mamlaka ya kubariki dhambi.
Mabaraza ya Maaskofu ya nchi mbalimbali yaliyotoa matamko kuhusu Hilo tamko lake wakiwemo mabaraza ya maaskofu majirani zetu wa Zambia, Malawi na Kenya unawaonaje kuwa wajinga kuwa Wewe ndie mwerevu au?
 
Tamko Kwa waumini kuhusu alichosoma Papa kuhusu kubariki wapenzi wa jinsia moja Hilo Baraza la Maaskofu TEC watatoa lini ?

Waumini wanasubiri nimekuja mbio nilikijua wametoa Hilo tamko
Hilo wataishia kutoa matamko ya Askofu mmoja mmoja individual
 
Mabaraza ya Maaskofu ya nchi mbalimbali yaliyotoa matamko kuhusu Hilo tamko lake wakiwemo mabaraza ya maaskofu majirani zetu wa Zambia, Malawi na Kenya unawaonaje kuwa wajinga kuwa Wewe ndie mwerevu au?
Fuatilia Current issues za Mwaka huu 2024 uone kama nadanganya,unajua watu wengi huufurahia uovu kuliko ukweli.
 
Back
Top Bottom