TCU wamezidiwa uwezo?

smwansasu

Member
Aug 19, 2009
14
3
Baada ya kuhairisha kutoa majina ya waliochaguliwa kuingia vikuu kwa mwezi mmoja sasa TCU wameanza lakini kwa matatizo makubwa. Website yao haipatikani kabisa uwe nje au ndani ya Tanzania. Kwa nini wasitumie ujanja wa baraza la mitihani la taifa, NECTA ambao huweka matokeo sehemu mbalimbali ili kuondoa msongamano kwenye mtandao? NECTA huweka website za wizara ya elimu na website ya serikali hivyo watu huwa na uchaguzi wapi wayapate.​
 
Yaani ni usumbufu tu hawa jamaa. Mimi kuna mtu huko kijijini anapiga simu kila baada ya nusu saa. Nimemwambia mtandao haupatikana wala hanielewi. That is TCU!
 
Unajua majina yaliyotoka ni first batch tu ambayo inahusisha institution 10. Nimejaribu sana kupata hayo majina ila website yao hai respond imeshindikana kabisa, wacha nitajaribu na leo nione itakuaje.
 
Ndugu Gama, SAUT wametoa majina ya waliochaguliwa kujiunga na chuo chao tu. Ningetegemea vyuo vingine afuate mfano huo na msongamano website ya TCU usingekuwepo.
 
Back
Top Bottom