KIDUNDULIMA
JF-Expert Member
- Aug 18, 2010
- 966
- 538
Kwa kweli nasema TCU hopeless kabisa maana wamedandia kazi ambayo hawaiwezi. Vyuo vimeshatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa lakini ukilog in kwenye website ya TCU sehemu ya selection status unakuta wameandika "pending" reason "selection not done". Kinachotokea ni kuwa ili uweze kujua kama umechagulia unalazimika kupitia website zote za vyuo ulivyoomba na bahati mbaya baadhi ya vyuo havijaweka taarifa zozote za selection kwenye website zao, vingine website hazifunguki na vingine ndo wana kulink TCU ambako majina hayapo (kama yapo ni yale machache ambayo wao wameita first batch). Option nyingine ni kununua magazeti ya kila siku na kuangalia ni chuo gani kimetoa majina. Ni Vyuo vichache kama UD,UDOM, RUCO, SEKUCO, SJ, SAUTI, SUA, ndio vimeweka majina ya waliochaguliwa kujiunga.
Kwa kweli TCU wamekula Sh 30,000 za applicants kwa kazi ambayo hawana uwezo nayo.
Kwa kweli TCU wamekula Sh 30,000 za applicants kwa kazi ambayo hawana uwezo nayo.