TCU: Darasa la saba sasa kujiunga na chuo kikuu moja kwa moja

"....b a a d a y a k u o n a k u n a wa t u we n g i wa n a o p e n d a k u e n d e l e a n a ma s omo y a e l i mu y a j u u , l a k i n i wame s h i n dwa k u t o k a n a n a k u t o k uwa n a v i g e z o , T C U i me amu a k u a n z i s h a m i t i h a n i h i y o ma a l umu .".
Je hao watu wengi walionekana vipi???? Bila ya tafiti kufanyika. Mbona ni sababu dhaifu sana.
Nilivyoelewa, kuna watu wachache wenye ushawishi, hususani kiuchumi na kisiasa, wamepiga hesabu na kuona upepo ni mkali. Hivyo wakashawishi mfumo huu unaotumika nchi zilizoendelea, bila ya kufanya tathmini, ili kulinda maslahi yao na ya ndugu zao wenye vyeti bandia, au walio hatarini kuondolewa kazini kwa kigezo cha Elimu duni. Na wala si kwa maslahi ya taifa. Pia kati ya hao wenye ushawishi, naamini, kuna wakuu wa vyuo vikuu binafsi wanahusika. Nasema hivyo kwa kuwa , kutoka na ufaulu mbovu wa Kidato cha Nne 2012, wanasugua vichwa ili kunusuru biashara siku za usoni.
MTIZAMO WANGU. Kama kweli serikali inao mpango mzuri wa kuboresha Elimu ingeboresha ngazi ya VETA. Kutokana na ukiritimba katika taifa......tusubiri matokeo. Ikiwa kama shule za Kata zimedhihirisha kushindwa , sitarajii tofauti.
 
Wakuu..
Nimesoma hii habari kuwa Watu waliofika kuanzia darasa la saba na kuendelea ambao hawakuweza kujiendeleza lakini wana uzoefu kazini watapata Nafasi ya kusoma Digree katika Vyuo hapa TZ.
Habari hii ni Nzuri lakini pia ni Mbaya.
Ubaya ni kuwa sasa Digrii Itakuwa kitu cha Kawaida sana,Kiasi kwamba Mtu mwenye Bachelor Degree atakuwa kama vile Mtu wa Form Four kwa Sababu itakuwa ni Yeboyebo.
Nachelea kusema kuwa UPATIKANAJI WA AJIRA UTAKUWA MGUMU SANA Kwa sababu karibu kila mtu sasa atakuwa na Digrii.

Cheki hii link hapa ya gazeti la Mwananchi kwa Info zaidi...

Dar es Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.

Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.

Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.

Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.

Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning' (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.

Sifa zinazotakiwa
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.

"Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.

Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,"alisema Dk Maronga na kuongeza:

"Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo."

Vigezo
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.

Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.

"Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa kupata wastani wa daraja ‘B' na somo husika la fani yake atatakiwa kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha kuendelea na masomo yake,"alisema Dk Maronga.

Alibainisha kuwa mitihani itakayokuwa ikitumika kudahili watahiniwa itakuwa ni wa somo la Kiingereza na Hisabati utakaokuwa na alama 30.

Mtihani wa Pili utakuwa na alama 30 ambao ni mtihani wa Maarifa na wa tatu utakuwa na alama 40, utakaokuwa ukitokana na fani husika ya mwombaji.

"Mfano mtahimiwa anataka kusomea sheria au uandishi wa habari, atatakiwa kufaulu kwa asilimia 50 somo husika, hivyo endapo atakosa kupata asilimia 50 ya somo lake hatapata cheti kitakachomwezesha kuendelea na elimu ya juu,"alisema Dk Marango na kuongeza:

"Cheti tutakachompatia mtahiniwa kitakuwa halali kwa kipindi cha miaka mitatu na baada ya hapo mwombaji atatakiwa kufanya upya mitihani hiyo."

Viambatanisho
Kutokana na maelezo ya TCU, mwombaji anatakiwa kuambatanisha cheti cha kuzaliwa au hati ya kusafiria,wasifu wake pamoja na vyeti vya ushiriki mzuri kutoka sehemu anayofanyia kazi.

Vingine ni nakala za vyeti vya taaluma, picha ndogo ‘passport size, nakala za vyeti vya taaluma za masomo ya hapo awali, ripoti ya tathmini ya utendaji kazi wake kazini kwa walioajiriwa kutoka kwa mwajiri na nakala ya kozi za awali alizokwishafanya.

Vituo vya Mitihani
Mkurugenzi huyo alisema mitihani itafanyika kati ya Mei na Juni mwaka huu katika vituo vinne vilivyoandaliwa katika vyuo.

Alisema kuwa chini ya mfumo huo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kitahusika na masuala ya Elimu huku Chuo Kikuu Tumaini Makumira cha Dar es Salaam (TUMADARCo) kikihusika na Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma.

Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA), kitahusika na Kilimo na Wanyamapori wakati Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU) kitahusika na masuala ya usimamizi na utawala,uhasibu, sheria na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

"Kwa kuwa ndiyo tunaanza, tumeamua kutenga vituo vinne, lakini mwakani tunatarajia kuongeza viwe vingi ili kukidhi mahitaji ya wananchi walio wengi,"anasema Dk Maronga.

Nawaonea huruma sana hao Wahadhiri. Kuna wanafunzi wenye wa BBA - Evening Class ambao wanao uzoefu katika fani zao za biashara; huwa wnapata tabu sana katika masomo yao, ilihali walikidhi viwango vya kitaaluma vivyomo. Kama mtu anajiamini anao uwezo na ajilipue katika huu mfumo, pia akidisco, pia asiogope kusema.
 
Mh. Lema, Mh. Sugu na Mh. Mbowe wachangamkie nafasi hiyo. Bahati haiji mara mbili.

Mbona huwataji Lusinde na Prof. Maji Marefu? Ulisha aambiwa darasa ö
la saba. Wote ulio wataja ni above o-level.
 
Duh! Serikali ya MAGAMBA haikosi maajabu. Kila kukicha lazima liundwe AJABU ambalo si la kawaida. Yaani mtu kafeli darasa la saba, akamudu elimu ya Chuo Kikuu?? Naamini kuna haja ya kuangalia nini agenda ya hili. kama sio mpango wa kuongeza idadi ya wajinga ndani ya hii nchi.
 
Hongera tcu, Maisha bora kwa kila Mtanzanzania. Lazma kila mtanzania awe na degree.

.... Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.
 
1. Hivi ni kweli kama umeshindwa kusoma O level kwa Miaka miwili, ukapiga Certificate then Diploma, alafu degree, je kweli utaweza kusoma hiyo Degree ?

2. Hivi kuna chuo kina dahili watu wa Kuingia kusoma Degree kinachotambua haya madaraja ya B+ ?

3. Hivi kuajiri watu wengi ni Kigezo cha kukuwezesha kuingia chuo kikuu? au ndio kukataa AKILI NDOGO, KUajiri AKILI KUBWA?
 
let us name this as a 'paradox of knowledge'.
hawa TCU huenda wamekaa wakaangalia kwa undani ni jinsi gani hawa watu waliopitia mfumo wetu wa 2-7-4-2-3 wanavyodidimiza nchi na sasa wanaona watoe nafasi hata wale walio waaminifu walioishia STVII waonyeshe uaminifu wao baada ya muda mrefu wa 'Doctorates' kuonyesha udanganyifu wao. Bado hili ni swali na tunahitaji kufikiri lakini lililo bora ni kujaribu kuliko kuacha kabisa
 
STOP SHOUTING !

Binafsi sitaacha kupambana na wasomi wapumbavu tena baadhi yao wemeendelea kuwa victims mpaka hapa JF bila kufikiria kuwa this is the home of great thinkers.

Theres no any problem with RPL System na kwa mtu mwenye ubongo wenye afya ni muda wa kujilaumu kwanini mfumo huu haukuwepo tangia miaka 10 iliyopita.

wanao lalamikia kuwa ni kitendo cha kuhalibu mfumo wa elimu ni wale wote waliopoteza a lot o years o level & Advance Thats Stupid, hebu tizama tafsiri ya RPL according to Wikipedia

Recognition of prior learning
(RPL), prior learning assessment (PLA), or prior learning assessment and recognition (PLAR), describes a process used by colleges and universities around the world to evaluate learning acquired outside the classroom for the purpose of assigning academic credit. Common ways individuals have acquired college-level learning include: corporate or military training; work experience; civic activity; and independent study.

Methods to assess prior learning are varied and include: standardized exams such as those delivered by the College Board, the Excelsior College Examination Program or DANTES Subject Standardized Tests Program; American Council on Education (ACE) Guides to credit recommendations for civilian and military training programs; evaluations of local training programs by local colleges, campus challenge exams; and portfolio assessments of experiential learning.
Prior Learning Assessment programs should not be confused with so-called life experience degrees, which purport to offer academic recognition of work experience but do not in fact have degree status and are illegal in many jurisdictions.

mfumo huu utamuwezesha mzee ilasi mfanya biashara mkubwa Mbozi mwenye mashule na mahospitali na mabasi ya mikoani huku akiwa na elimu ya darasa la saba kwenda kusomea business admistration na kuwa mtu mwenye ujuzi zaidi, na uwezo wa kufanya makubwa zaidi.

HONGERA SANA TCU TENA SANA hii itasaidia sana pia katika kuleta development competition baina ya wasomi katika jamii, wale wenye degree magamba inabidi watumie degree zao kufanya changes au la Watajuta.
Kitendo cha kuja na quote ya Wikipedia tu ni udhaifu wa ajabu huu-wikipedia si definition tu zisizo hakika hata wewe ukitaka unaweka, lete research findings zinazoonyesha "applicability" ya mfumo huu kwa Tanzania, hatupingi mfumo tunapinga utendekaji wa mfumo huu kwa mazingira ya Tanzania, kwani kama huyo Mfanyabiashara wa Mbozi anayetaka kujua biashara yake sehemu nzuri wapi, si aende technical colleges akachukue Biashara na Uhasibu, si ziko nyingi tu siku hizi tatizo nn. Huwezi ukalinganisha matumizi ya mfumo flani wa elimu unaotumika Marekani au Uingereze, Australia, Korea ukaulete Tanzania, kwa sababu Tanzania tuna-strive kufuta ujinga hizo nchi hazi-strive kufuta ujinga, bali zinasomea specialized taaluma. Hebu jaribu kufikiria unadhani primary holder wa Marekani au Uingereza ukamfanishe na primary holder wa Tanzania? Huyu anayesomea shule mwembeni? Nyie watu wa ajabu sana mkienda nje yale mazuri hamuyachukui yale msiyoyaweza ndio mnakuja nayo completely viseversa. Nimalizie kwa kukuomba tuwekee analytical arguments inayoainisha pros & cons za mfumo huu KWA TANZANIA
 
Nmeshtuka sana sana kuona hii habari kwa kweli elimu yetu imeteketea haiji akilini mtu wa darasa la saba kwenda chuo kikuu tunajua chanzo ni kutaka kuwahadaa watanzania baada ya wanafunzi kufeli kwa asilimia 90% na wazri mkuu na wazri wa elimu kugoma kujiuzulu hii serikali ya ccm inapeleka elimu yetu jehanamu tcu wameshapewa maagzo na serikali...eehh mungu tutaingia kwenye ushindani kweli kwa elimu hii inayoangamizwa kwa nini awamu hii ya nne tu ndo mambo yanaenda mrama hiviiiiiiii........na awamu ya pili mambo yaliharbka hivihivi mkapa akaja kuokoa jahazi sasa limezamishwa tena zaidi awamu hii ya nne zaidi ya awamu ya pili...eehh mungu awamu hii iishe haraka iwezekanavyo...watanzania tusikubali ujinga huu
 
Mfumo huu unatumika UK,USA,france etc binafsi nina degree ya biashara through mfumo huu kwa taaarifa zaidi soma gazet la mwananchi la leo
 
Tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania ( TCU) imeanza mchakato kwa watu wenye elimu ya darasa la saba kuweza kupata elimu ya shahada ya kwanza katika kozi mbalimbali hapa nchini. Ofisa Uhusiano wa TCU bwana Edward Mkaku amesema vyuo vitakavyotumika ni chuo cha Tumanini cha Dar es Salaam, UDSM na chuo kikuu cha Mzumbe! vigezo mwombaji lazima awe na umri wa miaka 25 na kuendelea, barua ya mwajiri, awe ana uwezo wa kuongea na kuandika kiingereza kwa ufasaha na utayari wa kusoma elimu ya juu.Alimalizia kwa kusema wameanzisha program hii kubaini vipaji vya watu walioshia darasa la saba.
Du inachanganya kidogo maana kama mtu alisoma shule zetu hizi za kata kuongea kiingeleza kwake itakuwa ngumu
 
katika vitu tumeamua kuchezea na vitakuja kutufanya tujute sana kama taifa ni ELIMU!
 
Ndugu Revocatus Kashaga tafadhali rejea jamvini hapa utufafanulie zaidi hiyo "programme" mpya ya TCU, title na habari yako kwa ujumla havijitoshelezi. Wahitimu hao wa darasa la saba watajiunga na vyuo hivyo katika ngazi gani ya masomo? Maana Vyuo vikuu mbali na shahada pia hutoa mafunzo ya cheti na stashahada. Tafadhali tufafanulie hiyo "programme" ambayo mwenzetu umebahatika kuisikia/kuiona.

Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.

Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.

Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.

Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.

Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning' (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.

Sifa zinazotakiwa
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.

"Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.

Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,"alisema Dk Maronga na kuongeza:

"Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo."

Vigezo
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.

Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.

"Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa kupata wastani wa daraja ‘B' na somo husika la fani yake atatakiwa kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha kuendelea na masomo yake,"alisema Dk Maronga.

Alibainisha kuwa mitihani itakayokuwa ikitumika kudahili watahiniwa itakuwa ni wa somo la Kiingereza na Hisabati utakaokuwa na alama 30.

Mtihani wa Pili utakuwa na alama 30 ambao ni mtihani wa Maarifa na wa tatu utakuwa na alama 40, utakaokuwa ukitokana na fani husika ya mwombaji.

"Mfano mtahimiwa anataka kusomea sheria au uandishi wa habari, atatakiwa kufaulu kwa asilimia 50 somo husika, hivyo endapo atakosa kupata asilimia 50 ya somo lake hatapata cheti kitakachomwezesha kuendelea na elimu ya juu,"alisema Dk Marango na kuongeza:

"Cheti tutakachompatia mtahiniwa kitakuwa halali kwa kipindi cha miaka mitatu na baada ya hapo mwombaji atatakiwa kufanya upya mitihani hiyo."

Viambatanisho
Kutokana na maelezo ya TCU, mwombaji anatakiwa kuambatanisha cheti cha kuzaliwa au hati ya kusafiria,wasifu wake pamoja na vyeti vya ushiriki mzuri kutoka sehemu anayofanyia kazi.

Vingine ni nakala za vyeti vya taaluma, picha ndogo ‘passport size, nakala za vyeti vya taaluma za masomo ya hapo awali, ripoti ya tathmini ya utendaji kazi wake kazini kwa walioajiriwa kutoka kwa mwajiri na nakala ya kozi za awali alizokwishafanya.

Vituo vya Mitihani
Mkurugenzi huyo alisema mitihani itafanyika kati ya Mei na Juni mwaka huu katika vituo vinne vilivyoandaliwa katika vyuo.

Alisema kuwa chini ya mfumo huo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kitahusika na masuala ya Elimu huku Chuo Kikuu Tumaini Makumira cha Dar es Salaam (TUMADARCo) kikihusika na Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma.

Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA), kitahusika na Kilimo na Wanyamapori wakati Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU) kitahusika na masuala ya usimamizi na utawala,uhasibu, sheria na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

"Kwa kuwa ndiyo tunaanza, tumeamua kutenga vituo vinne, lakini mwakani tunatarajia kuongeza viwe vingi ili kukidhi mahitaji ya wananchi walio wengi,"anasema Dk Maronga.

Darasa la saba sasa kujiunga vyuo vikuu - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
kama itakua ivyo, nachana vyeti vyangu vyote, upumbafu sasa huu....

Kwa sababu wewe unafikiri elimu ni vyeti! (Mawazo walionayo watanzania wengi). Mtu anatambulika kuwa amesoma kwa sababu ya matendo na sio vyeti.
 
Awe na miaka 25? Peleka kwenye utani hii kitu!!!!!!

Source please!

Je watapewa boom? Je utamjuaje mtu mwenye kipaji? Au, je vyuo vitakuwa na wataalamu wa uanishaji wa vipaji vya waombaji mbalimbali? Kama ni hivyo, hata wale waalimu wa UPE wanastahili kusoma shahada kwa kuwa wanavipaji vya kufundisha. Je watapewa boom? Je huu mfumo umetoka nchi gani? Maswali yanazaliwa kila dakika nikifikiria juu ya uendeshwaji wa mpango huo. Naomba mnaofahamu vizuri mtupe majibu, kwa kuwa jamii inahitaji ufafanuzi wa kina.
Soma post namba 46
 
Back
Top Bottom