Mkuu usichoelewa hapa ni nini!tayari kuna wakuu huko serikalini wameshajijua wana ma vyeti ya kufoji na wameshahisi kustukiwa kwahiyo wamebuni mpango ambao utawasaidia kupata vyeti vya chuo kikuu kihalali,std seven ambaye anafanya kazi ya kuajiriwa anapatikana wapi kama si wale wa mwaka 47 wanaokaribia kustaafu!Sina uelewa mpana wa mifumo ya elimu duniani, lakini kuna ka-harufu ka hatari kananukia nchi yetu. Yaani darasa la saba hili la Tanzania ya leo ambapo mtoto anashindwa kupata alama za kujiunga na shule za kata, then akasome chuo kikuu kwa mitihani ya masomo matatu? Sasa practically, huyu darasa la saba wa miaka hii 25 atapata udhoefu wa kutoka wapi, na fani ipi/ Kwa sababu nijuavyo mie, Serikali na waajiri wengi wanachukua kuanzia form 4, hawa Darasa la 7 wengi ni ma-house boy na house girl ambao hata hivyo wengi nao hawawataki siku hizi. TCU mnataka kutupeleka wapi, hebbu tunaomba wekeni hadharani utafiti mlioufanya ili tuone ikiwa kweli mko sahihi, lakini kama mnafanya kazi kwa ki-memo; kwa kweli Taifa laelekea kubaya sana. Nadhani ingefaa kuimarisha mfumo wa QT na VETA na kuifanya iwe lazima kwa anayeshindwa kuendelea na Kidato cha kwanza, badala ya hii mnayotaka kufanya, ni msiba huu. Kama watoto wadogo wa drs la saba na kidato cha 4 wanaiba mitihani, mnadhani hawa watu wazima wenye hela zao waliokimbia shule na sasa kutaka kuwa na veti vya chuo kikuu watashindwa kuiba mitihani?
Lakini pia Kwani utalaam na kulitumikia Taifa mpaka uwe na cheti cha elimu ya chuo kikuu pekee. Mbona tunao wasio na na vyeti vya chuo kikuu lakini wako vema kwa utambulisho wao huo wa Darasa la saba n.k. Whats motives behind this move? Jibu la watanzania kimya
haiwezi Ikawa Elimu Tena!!!!!!!!!
Tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania ( TCU) imeanza mchakato kwa watu wenye elimu ya darasa la saba kuweza kupata elimu ya shahada ya kwanza katika kozi mbalimbali hapa nchini. Ofisa Uhusiano wa TCU bwana Edward Mkaku amesema vyuo vitakavyotumika ni chuo cha Tumanini cha Dar es Salaam, UDSM na chuo kikuu cha Mzumbe! vigezo mwombaji lazima awe na umri wa miaka 25 na kuendelea, barua ya mwajiri, awe ana uwezo wa kuongea na kuandika kiingereza kwa ufasaha na utayari wa kusoma elimu ya juu.Alimalizia kwa kusema wameanzisha program hii kubaini vipaji vya watu walioshia darasa la saba.
Mi nadhani kuna njama za makusudi zinafanywa na viongozi wa hii serikali ili kuhakiki 2015 haiingii madarakani,kama hivyo ndivyo ni safi sana endeleeni tu ku-implement sera za mtindo huo na mkihitaji nyingine niambieni niwape!Tanzania kwa ngonjera mnafurahisha sana! wapo maelfu waliomaliza kidato cha sita na diploma na wamekosa nafasi za kujiunga na chuo kikuu kutokana na ufinyu wa mikopo na nafasi leo mnazungumzia darasa la saba,.Nyie viongozi wapanga sera mmeshatuona watanzania hatuna ubongo kabisa au vipi??
Ona mbele zaidi huu mfumo .unatumika Marekani ,Uingereza , Ufaransa e.c.t nyingi duniani ,Nimfumo mzuri sana kwa kukuza vipaji ,mfano hapo meru Arusha kuna kijana kaunda trekta ni darasa la saba ,unaonaje huyu akichukuliwa chuo kikuu kwa elimu zaidi ?