TCRA yapiga stop wimbo wa Nay wa Mitego kuchezwa kwenye vyombo vya habari

Kitengo cha propaganda Cha CCM kimekufa? Serikali inaposhambuliwa wao wangekuja Kwa wananchi na vyombo vya habari kutoa ufafanuzi na kujibu mashambulizi ilikuitetea serikali ya chama chao. Badala yake wanatumika chawa ambao kiukweli hawana ufahamu wa maswala mengi ya uendeshaji wa serikali. Hii nchi imekuwa ni nchi ya kujipendekeza upate mlo au cheo. Nchi ya machawa.

Tukiacha unafiki kuna baadhi ya mambo aliyoyasema Ney je hayapo?,
Mfano wezi wanafanywa nini? kataja report ya CAG kama mfano.
Utendaji wa bunge letu ukoje?
Hili la bandari kuuzwa hapo kasema uongo, bado ni mapema kuhukumu
 
View attachment 2701756

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) impokea taarifa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuzuiya wimbo uitwao "Amkeni" uliopigwa na mwanamuziki Emmanuel Elibariki (Nay wa Mitego) kutopigwa katika mitandao ya kijamii na vombo vya habari.

Aidha, kwa mujibu wa BASATA, maudhui ya wimbo huo yana melekeo wa kutaka wananchi wasiwe na imani na Serikali, kuchochea wananchi kuwa na mapokeo hasi juu ya utekelezaji wa mipango ya Serikali yao kwa ujumla, na kuwa ni wimbo wa uchochezi baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi wake.

Hivyo, kwa barua hi, TCRA inaelekeza chombo chako cha habari kutopiga wimbo huo.

Tafadhali zingatia maelekezo.

Pia soma: Nay wa Mitego aitwa BASATA. Atuma Wanasheria wake
Too late, tunao tayari
 
Hata wasipopiga, maana tayari vibanda vya kuingiza nyimbo wanao.
 
Fear of the unknown...! Maneno ya Mungu yanasema: Mwenye dhambi hana raha..! (Yaani ni mtu wa kujistukia kila wakati)

Sent using Jamii Forums mobile app

Cha kustaajabisha ni kwamba hakuna hata mmoja katika makundi yote kati ya serikali na wananchi na wenyenchi asie na dhambi japo hata kiduchu. Hayupo.

Its a game of Chase, no move is wasted and the King is always protected.
 
Hii nchi tatizo ina viongozi washamba sana na hawana exposure. Marekani Nipsey Hussle aliwahi kuimba nyimbo ya “F*CK DONALD TRUMP” na bado hakukuwa na upumbavu wowote. Msikosolewe nyie ni nani..? Mnatembea ulaya huko kila siku ila akili zenu bado zipo fixed, exposure mnayoipata hata haiwasaidii.

IMG_6488.jpg

Viongozi wetu wanatokana na jamii zetu. Viongozi wetu ni matokeo ya jamii zetu.

Hata siku moja nazi haiwezi kuota kwenye mti wa mpera.
 
Muda wa nchi kuongozwa na mwanamke haujafika imekuwa bahati mbaya rais aliyechaguliwa kafariki. Nchi imeharibiwa sana.
Kweli kabisa.kila sehemu ya nchi hii inanuka uozo.huyu hastahili kabisa kuwa ...sema tu ndiyo hivyo katiba iliyowekwa na wabunge punguani imemweka madarakani
 
hizoo sababu TCRA wamezitoa hazina mantiki kungekuwa na mfumo wa chama kimoja ni sawa ila sio kwa mfumo wa vyama vingi.

kuna haja ya waandishi wa habari kuwahoji hawa TCRA kuhusu sababu walizo zitoa maana hazina maana.
 
Mbona wamekosea jina lake? Emmanuel Elibariki Kingu ndio jina lake 😜😂😂😂
 
View attachment 2701993

Viongozi wetu wanatokana na jamii zetu. Viongozi wetu ni matokeo ya jamii zetu.

Hata siku moja nazi haiwezi kuota kwenye mti wa mpera.
Again, tafuta exposure in real life na uachane na kupata exposure yako kwenye mitandao.
Nipsey was never killed kwa sababu za kisiasa, get your fact straight. Na Nipsey FDT haikuwa nyimbo yake ya kwanza kuikosoa serikali, he has several. Kwa nyie msiokuwa na exposure, let us tell you this, in America kufa kwa gunshot ni rahisi kuliko kufa na magonjwa ya aina yeyote. So yes, kufungia nyimbo za artists sababu wamekosoa serikali sounds like a thing did in 10th century huko.
 
View attachment 2701756

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepokea taarifa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuzuiya wimbo uitwao "Amkeni" uliopigwa na mwanamuziki Emmanuel Elibariki (Nay wa Mitego) kutopigwa katika mitandao ya kijamii na vombo vya habari.

Aidha, kwa mujibu wa BASATA, maudhui ya wimbo huo yana melekeo wa kutaka wananchi wasiwe na imani na Serikali, kuchochea wananchi kuwa na mapokeo hasi juu ya utekelezaji wa mipango ya Serikali yao kwa ujumla, na kuwa ni wimbo wa uchochezi baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi wake.

Hivyo, kwa barua hi, TCRA inaelekeza chombo chako cha habari kutopiga wimbo huo.

Tafadhali zingatia maelekezo.

Pia soma: Nay wa Mitego aitwa BASATA. Atuma Wanasheria wake
Very wrong move ya mamlaka.

Serikali imeshajiweka kwenye spotlight inavyopingana na UHURU WA SANAA ambapo dunia yote imeridhia.

Subirini mwangwi wake soonest
 
TCRA wasingehangaika kuufungia kwasababu ney mwenyewe na waliomfadhili kuutengeneza, ni yao ilikuwa kuurusha mtandaoni basi na walitarajia muda si mrefu utafungiwa. Matarajio yao hayakuwa uishi hata wiki kwenye vyombo bali urushwe, watu waudake, ufungiwe, ila ujumbe umeshafika.

Ningekuwa mimi ndio TCRA wala nisingehangaika kwenye ulimwengu ambao majority wanamiliki smartphones,wanao kwenye simu.

Na lazima kwa kuufungia kwao watu watatamani wausikilize wajue una nini hadi umefungiwa? Si huwa unaona mtu amepiga picha chafu, tcra imefungia porn ila watu wanatoa hadi pesa waone hiyo porn ipoje. Ndio ushetani,sembuse wimbo tu.

The truth is in this modern age huwez kufungia kitu 100% wasikipate. Wameshachelewa
 
Back
Top Bottom